MPENZI ASIYEKUPENDA
Read More
(1) Haonyeshi
(2)
Haonyeshi
hamu ya kuboresha uhusiano wenu katika maeneo mbalimbali. Hakuna mambo mapya
yanayoweza kuongezea utamu katika uhusiano wenu.
(3)
Huanzisha
mzozo ugomvi bila kujali athari yake kwa uhusiano wenu kwa ujumla.Anajua vitu
ambavyo huvipendi lakini bado anaendelea navyo bila kujali hisia zako. Kwa
mfano anajua hupendi ukipiga simu isipokelewe lakini zaidi ya mara 2 imetokea
hivyo. Asikudanganye kuwa alisahau sebuleni kwani anaekupenda atathamini mawasiliano
na ni muhimu kwake atarajie kupigiwa na wewe.
(4)
Mara
nyingine hukwepa kuzungumzia mambo ya sasa na kupendelea kuzungumzia mambo ya
baadae kama vile kufunga ndoa au miradi mingine ya kimaisha.
(5)
Wazazi
wake hawakufahamu vizuri au hakusifii kwa wazazi wake au marafiki zake.
(6)
Mara
nyingi husema kuwa hana uhakika juu ya mambo ya mbele ya uhusiano wenu na
kutumia lugha ya “ni mapema sana” au kusema hajui la kukuambia juu ya maisha au
mwenendo wake wa baadae.
(7)
Hakuamini
vya kutosha na hivyo kuonyesha wasiwasi katika maeneo mengi jambo ambalo
linakukosesha raha.
(8)
Unapata
shida kuongelea juu ya mambo ambayo ni ya muhimu sana kwako kwa kuwa huenda
atayapuuzia au kutoonyesha ushirikiano. Hii ni moja kati ya dalili kubwa sana
ya kuangalia.
(9)
Huwezi
kuanzisha mazungumzo juu ya mapungufu unayoyaona katika uhusiano wenu bila ya
kuanzisha ugomvi.
(10) Anaweza kukutukana
au kuonyesha dharau kwako mbele za watu na hata kama ni utani tambua kuwa anaonyesha
kuwa hupendwi na huheshimiwi.
(11) Tendo la ndoa ni kwa
ajili yake pekee na hajali haja yako au kuridhika kwako katika tendo hilo.
(12) Hayuko tayari
kukufanyia mambo mazuri sawa na yale unayomfanyia wewe.ANAPENDA na kusisitiza
kuwa anastahili hili na lile lakini hathamini
haja za moyo wako.
(13) Haonyeshi kwa watu
wengine kuwa kwake wewe ni muhimu na wa kipekee na hukwepa kuonekana na wewe
mara kwa mara.
(14) Mara nyingine
anapenda kutoka peke yake na hahangaiki kutafuta muda wa kukaa nawe. Kama
mahali mnapokuwa pamoja ni kitandani tu fahamu kuwa hakupendi hata kama
anakuimbia wimbo wa NAKUPENDA kila sekunde.
(15) Anakasirika kwa
urahisi sana awapo na wewe. Uonapo anapokasirika mara kwa mara husema maneno ya
dharau au kukutukana basi juwa kwamba hupendwi
bali anakuvumilia tu.
(16) Anapata shida
kuomba msamaha anapokosea kwa kuwa kwake unaonekana kuwa upo katika maisha yake
kimakosa, yaani unakosea kuendeleza uhusiano wenu.
(17) Anapata shida
kuendeleza maongezi anapokuwa na wewe peke yenu.
(18) Sio mwaminifu kwako.
(19) Hufanya utani juu
ya mambo ambayo anajua kuwa ni muhimu kwako.
0 Response to " MPENZI ASIYEKUPENDA "
Post a Comment