JE KUCHUNGUZA SIMU YA MPENZI WAKO NI SAHIHI AU UJINGA?
Read More
Penzi lilojaa furaha na
lenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kwa wengi ni kitendawili kigumu sana. Na
kwa sehemu kubwa ugumu huo hutokana na ukosefu wa uwazi na ukweli.KUKOSEKANA
kwa mazingira ya uwazi na ukweli
husababisha ubinafsi wa hali ya juu
ambao ukiachiliwa kuendelea hufikia kiwango cha ukatili tunouona katika
usaliti na vifo vya mahusiano mengi.Kwa wenye magari ili gari lako liweze
kudumu muda mrefu unaagizwa kuangalia kiwango cha maji na oil katika gari yako
mara kwa mara na kushindwa kutii agizo
hilo gari lako halitaweza kudumu. Katika mahusiano ya kimapenzi kwa wale wenye
malengo ya muda mrefu kuhakikisha kuwa mpenzi wako ni wako peke yako ni jambo
la msingi katika ulimwengu huu wenye michepuko ya kila rangi. Tafiti nyingi
zinaoonyesha kuwa mahusiano yenye uwazi wa kiwango cha juu yanakuwa na furaha
zaidi na hudumu kwa muda mrefu sana ukilinganisha na mahusiano yenye mazingira
ya usiri na ubinafsi.
Uwazi unasaidia
kumfahamu mpenzi wako vizuri zaidi na hivyo kuwez kumsaidia katika maeneo yenye
mapungufu au udhaifu kwa kuwa hakuna aliye makamilifu mara nyingi udhaifu
usipogunduliwa mapema majanga hujitokeza. Kuna mambo mengi yanayochangia kufa
kwa uhusiano na usaliti ni moja kati ya mambo makuu katika hayo. Ili kuweza
kuepuka moja kati ya mambo yanayosababisha usaliti ni vyema kuangalia upya
matumizi ya simu kwa uangalifu sana kwani
matumizi mabaya ya simu yamewaletea wengi majanga. Simu ni chombo kizuri
ambacho kinaweza kuchangia katika kuboresha penzi na kulinda penzi. Kwa kuwa
simu hutumika sana katika kuanzisha na kuendeleza usaliti upo umuhimu wa wapenzi
kupeana uhuru wa kupekuliana simu zao bila hofu yoyote.Watu wengi wanapingana
na hilo jambo ambalo linathibitisha kuwa
mahusiano mengi hayana amani ya kweli.KUMBUKA KUWA HUWEZI KUWA NA AMANI YA
KWELI KAMA HUNA UHURU.Mfungwa hata awe kwenye gereza la dhahabu na kula chakula
kwenye sahani za dhahabu ha hata akiende chooni na choo kikawa cha dhahabu
kwakuwa hana uhuru hana raha kabisa.Kwanini uendelee kuwa katika uhusiano ambao
hauna uhuru?Ni wakati wa kufurahia maisha sio kuishi kwa kuvumiliana,upo
umuhimu wa kutumbua majipu ili furaha na maendeleo ya furaha yaonekane.
Moja kati ya dalili ya
kwamba mpenzi wako ana mpango wa kukusaliti au tayari amekwisha anza usaliti ni
kudai kuwa simu yake ni yake binafsi na
hakupi uhuru wa kuipekua. Dalili
ya pili ni ile mpenzi wako anaposhindwa kutoa maelezo yalionyooka juu ya mahali
alipokuwa au alipo mbali na masaa ya
kazi.Dalili ya tatu ni kuwa na ukaribu wa kimaongezi na mtu wa jinsia tofauti
na yake. Dalili ya nne kupunguza kiwango na wingi wa uchezaji awa ngoma ya
wakubwa. Dalili ya tano ni hapendi kukaa na mpenzi wake kwa maongezi kwa muda
mrefu na mawasiliano ya simu ni machache. Iwapo wewe humpi mpenzi wako sababu
ya kuwa na wasiwasi na wewe katika maeneo
hayo huna saababu ya kuhofia pale mpenzi wako anavyopekua simu yako.
Tafiti iliofanywa na
shirika la ulinzi kwenye mitandao ya internet inasema kuwa asilimia 46 ya wake
kwa waume hupekua simu za wapenzi wao. Mtu huanza kupekua simu yako pale aonapo
dalili kuwa penzi kati yenu limepungukiwa furaha na msimsimko uliokuwepo
mwanzoni na mpenzi wako anapoanza kupekua simu yako anatafuta jibu ya hali hiyo
mbaya.
Kwanini
watu hupekua simu za wapenzi wao na kwa nini wengine hawataki wafanye hivyo?
Hebu angalia hili,
iwapo wewe ni mmoja wapo wa wale wasiotaka kupekuliwa simu zao. Mpenzi wako
akapekua simu yako na asikute lolote baya si atajiona mpumbavu? Je, na pia
akiacha kupekua simu yako na baada ya miaka miwili anasikia umempa
mimba mfanyakazi mwenzio pia si atajiona mjinga na mpumbavu? Atajiona mpumbavu
kwa kuwa kama angekua anapekuwa simu yako mapema angegundua mapema?HALI kama hiyo imemkuta dada
mmoja baada ya kugundua kuwa mtu aliekuwa anaamini kuwa mume mtarajiwa
tayari alikuwa na mke na hapo hapo alikuw ni mjmzito.INAUMA sana mtu
kukupotezea muda wako na hukuwa na uwezo wa kugundua kuwa unadanganywa.SIMU
INAKUPA UWEZO HUO.
Ukweli ni kwamba
kutokana na udhaifu wa kibinadamu iwapo mtu ataachiwa kufanya kama anvyopenda
upo uwezekano mkubwa wa kufanya mambo mabaya yatakayowaumiza wengine na ndio
maana kuna polisi na mahakama. Ukitaka kupingana namimi kuwa upekuaji wa simu
ya mpenzi wako sio kitu kizuri naomba uangalie yafuatayo. Je, hujawahi kusikia viongozi wakubwa wa
serikali wamefanya mambo mabaya? Hujawahi kusikia viongozi wa dini wamefanya
mambo mabaya? Je, watu ambao wanakamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani wote
ni vichaa au ni watu wenye heshima zao ukiwaona katika hali ya kawaida? Bila
shaka hapo utapata ushahidi kuwa ipo haja kubwa ya kulinda uhusiano wa
kimapenzi na kupekua simu ya mpenzi wako ni moja kati ya njia nzuri ya ulinzi
huo .Tafiti zinaonyesha kuwa asilimi 60 ya wanandoa wameshawahi kusaliti na
hiyo ni idadi kubwa na maumivu kwa yule asie na hatia ni makubwa sana. Hata
kama hakuna dalili za usaliti, kumpa uhuru mpenzi wako kupekuka simu yako ili
ajiridhishe ni jambo la muhimu kwani inakusaidia wewe uanepekuliwa kuongeza
bidii kuendelea kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na kupiga vita vishawishi vyote
vinavyotokeza. Kutokana na ukweli huo ni vyema mfanye kupekuliana simu kama
mchezo uletao burudani kati yenu badala ya hasira.
Mkiweza kueleweshana
juu ya mchezo huo na kupeana kanuni za mchezo huo kupekuliana simu hakuwezi
kuwa tishio kabisa. Iwapo utafanya jitihada za kuonyesha penzi motomoto kwa
mpenzi wako utampunguzia mpenzi wako haja ya yeye kupekuwa simu yako. Usimseme
vibaya mpenzi wako kwa kupenda kupekua simu yako mara kwa mara mthibitishie
kuwa unampenda na huwezi kumsaliti kwa kumpa uhuru wa yeye kupekuwa simu yako.Huoni
kuwa hiyo ni njia rahisi ya kumthibitishia uaminifu wako Yule
umpendae?NDIO unaweza klusema kuwa
atakuwa anafuta meseji zake, sawa hilo lipo lakini iko siku atajisahau na atatumbukia mtegoni.
Iwapo unajitahidi kuondoa sababu zote ambazo
zinamfanya mpenzi wako awe na wasiwasi utaleta amani na furaha kati yenu badala
ya migogoro. Unajua nini? Hata kama mpenzi wako atakuta mambo ambayo wewe
unayaona ya utani wa kawaida lakini kwake yakawa yanamletea wasiwasi ichukulie
hiyo kama fursa yakuelewa udhaifu na uelewa wa mpenzi wako na niwajibu wako
wewe kumsaidia mpenzi wako katika hayo bila ya kuonyesha dharau yoyote au ukali
wowote ule. Hata kama utakuwa umefuta meseji zote zile ambazo unaziona kuwa
zina uwezo wa kuleta hali ya kutoelewana lakini pale unapompa mpenzi wako uhuru
wa kupekuwa ile hofu ya kwamba huenda kuna meseji ulisahau kuifuta itakusaidia wewe kuona jinsi gani usaliti ni
wa hatari katika uhusiano wenu iwapo kweli unampenda mtu ulie nae. Iwapo kweli
unampenda mtu ulie nae hakuna gharama ilio kubwa itakayokushinda kuitoa kwa
ajili yake. Iwapo humpendi mpenzi wako huwezi
kuona hatari ya kumuumiza au kumpoteza mpenzi wako lakini iwapo unampenda
utajiona kuwa unao wajibu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa mpenzi wako ana amani
na wewe wakati wote.
Hebu fikiria, je kuna
njia gani rahisi ya kumkamata mpenzi wako anapokuwa amechepuka na kuwa na mtu
mwingine kimaapenzi zaidi ya simu? Kama hiyo ni njia rahisi kwa nini isitumike
kulinda penzi mnalolithamini?Mtu anaekataa kutumia simu kama njia ya kulinda na
kutunza penzi hana mapenzi ya kweli.
Wengi hutumia
kisingizio kuwa kupekuwa simu ya mpenzi wako ni sawa na kuingilia uhuru wa
taifa jingine, sio kweli kabisa kwani iwapo naweza kuzishika sehemu zako za
siri kwa uhuru wote ni sahihi kabisa kwa
mimi kuwa na haki ya kujua siri zako zote zilizomo kwenye simu yako. Kinyume na
hapo ni kudaganyana kabisa. Unajua nini? Kwa sababu yoyote ili mpenzi wako
anapoanza kuwa na wasiwasi na wewe ni wajibu wako wewe unaedai kuwa unampenda
kumsaidia kuondoa wasiwasi huo.Wasiwasi wake hauwezi kuondoka wenyewe bila ya wewe
kumsaidia. Na kama huwezi kumsaidia katika hilo ni dhahiri kuwa humpendi hata kama unampa mamilioni ya
pesa kila siku. Kwa watu ambao hawajawahi kusalitiwa hawawezi kuona ukubwa wa
wasiwasi wa kuwepo kwa uwezekano wa
kujeruhiwa kama wale ambao ambao
walikwasha salitiwa huko nyuma.Watu ambao wameshawi kuumizwa na usaliti au
kuona marafiki zao wa karibu wameumizwa wanakuwa na wasiwasi mkubwa sana na ni
wajibu wa wapenzi wao kuelewa chimbuko la wasiwasi huo.
Watu wengine
wanajifariji kwa kusema kuwa sitaki kupekua simu ya mpenzi wangu kwani inaweza
kuniumiza vibaya na hivyo kuepuka maumivu wanaogopa kushika simu za wapenzi
wao. Huo ni umpumbavu kwani ni sawa na kusema kuwa “Nakuruhusu unisaliti lakini sitaki kujua kama unaisaliti”.
Unaposema hivyo na
kukubaliana na hilo moja kwa moja unapoteza haki ya kuuliza maswali pale mpenzi
wako anapokuwa amechelewa kurudi nyumbani, huna haki ya kuuliza swali lolote
pale simu yako isipopokelewa au unapokuta simu ya mpenzi wako imezimwa . Je
hapo kuna mazingira ya furaha katika
uhusiano huo? Haiwezekani kuwa na furaha kwa kuwa unayo maswali halali lakini
ukiuliza mwenzio nakuwa mkali na kutoa maneno mabaya. Usishangae kuona hali
kama hiyo kwani kwa wewe kuogopa kusisitiza uwazi kati yenu mpenzi wako
ameingia kwenye mahusiano mengine ambayo anayathamini zaidi ya wewe.
Hivi karibuni dada
mmoja mzuri mwenye kazi nzuri alinisikitisha kwa kuniambia kuwa anatembea na
mume wa mtu ambae anataka ampeleke akamtambulishe nyumbani kwao. Dada huyo anadai kuwa mume wa mtu anampenda kwa kuwa
anaweza kukaa kwake hadi saa nane za usiku na umuulizapo kuwa mbona muda
umekwenda sana mkeo hatakushambulia. Dume hilo linamjibu kwa kumwambia “wewe
nione kama vile sina mke na wewe ndio mke wangu “ Dada huyo mwenye elimu nzuri ameamini maneno hayo bila kutambua kuwa
mwanaume huyo anamuonyesha ni jinsi gani alivyo mkatili na sio kuwa ana upendo
mwingi.Kama anaweza kukaa na mwanamke mwingine hadi saa 8 za usiku bila kujali maumivu ya mkewe
anafikiria ukatili huo hautafika kwake yeye? Usidanganyike sisitiza penzi la
kweli na lenye uwazi mkubwa.
Hebu fikiria, lipi
bora, kugundua kuwa mpenzi wako anakusaliti au kugundua kuwa amekuambukiza
UKIMWI? Kama ungejua kuwa kupekua simu ya mpenzi wako kungekuepusha na ugonjwa
wa UKIMWI usingefanya hivyo kwa bidii zaidi? Lipi bora, upekuwe simu ya mke
wako na ugundue kuwa ni msaliti au uje ugundue kuwa mtoto ulieamini kuwa wewe
ndie ulisababisha ujauzito sio mototo wako bali ni wa mwanaume mwingine (
mkemia mkuu wa serikali anasema zaidi ya asilimia 40 ya watoto wanawaita baba
watu ambao sio baba zao).
Simu
ni kama moto, moto ukiutumia vizuri utachangia katika kufanya maisha yako yawe
matamu zaidi lakini ukiutumia vibaya unaweza kuleta majanga. Kwa hiyo basi kwa
kadri tunavyokuwa waangalifu katika matumizi ya moto lazima tuwe waangalifu
katika matumizi ya simu. Hebu jiulize maswali yafuatayo.
1. Je, kuna mambo ambayo hupendi mpenzi
wako ayakute kwenye simu yako? Kwanini hutaki ayaone?
2. Je, unapokuwa mbali na simu yako na
ukawepo uwezekano wa mpenzi wako kusoma yaliyomo kwenye simu, je unakuwa na
wasiwasi kuwa huenda mtu mwingine anaweza kutumia ujumbe mfupi utakao fichua
uovu wako?
3. Je, umeshawahi kufuta meseji kwenye
simu yako kwa kuogopa kugunduliwa na mpenzi wako?
4. Je, umeshawahi kutumiwa picha
ambazo unadhani zitamkasirisha mpenzi wako.
5. Je, una mawasiliano na mtu mwingine
ambae usingependa mpenzi wako ajue juu ya mawasiliano hayo?
Iwapo
moja kati ya maswali hayo kwako umejibu “NDIYO” ni wakati wa kuangalia upya
iwapo kweli unampenda mpenzi wako kwa moyo wote au la.Na kama unaona umemnyima
uhuru anaohitaji kweli unampenda au unamytumia tu?
Utakuwa
unamtesa mpenzi wako kwa kumkataza asishike simu yako kwani hata wewe mwenyewe
unajua kuwa sio kitu rahisi kuishi katika hali ya wasiwasi.Ni wajibu wako
kutengeneza mazingira ambayo yatamletea amani mpenzi wako kwa kumpa uhuru wa kushika simu yako.
Hebu
fikiria, mpenzi wako yuko bafuni na ameacha simu kitandani na mara unasikia
meseji zinaingia mfululizo,kwa hali ya uanadamu unapatwa na hamu ya kutaka
kujua kuna nani anayetuma meseji hizo. Dada mmoja aliamua kufanya utafiti
miongoni mwa marafiki zake kwenye facebook na kuona kuwa wengi wanaliona hilo
kuwa jambo baya lakini wengi wao wanasema bado wanajikuta wnachungulia kuona
kuna nini kwenye simu za wapenzi wao bila ya kupewa ruhusa ya kufanya hivyo.Kwanini
watu ambao wanasema sio vizuri kupekua simu za wapenzi wao wanajikuta
wanashindwa kujizuia na kupekua simu hizo pale wanapoamini kuwa wapenzi wao
hawawezi kugundua?WATU HAO HUFANYA HIVYO
KWNI NI HALI YA UANADAMU WETU KUTAFUTA
UHAKIKA WA MAMBO ili kuwa na amani.
Pale
unapopewa uhuru wa kupekua simu ya mpenzi wako lazima uwe na uhakika kuwa unao
uwezo wa kukabiliana na madudu ambayo unaweza kuyakuta yamezaliana kwenye simu
ya mpenzi wako. Na usishangae utakapoonyesha kuwa umaumia kukuta madudu yenye
sura zinazotisha na hapo hapo ukasikia mpenzi wako akisema “shauri yako umeyataka
mwenyewe, usingepekuwa simu yangu hayo yote yasingekukuta na hata pole sikupi”.
Watu
wengine wanaopigia debe haki ya kuheshimu uhuru wa mpenzi wako wanasema kuwa
iwapo una wasiwasi na mpenzi wako badala ya kupekua simu yake mueleze juu ya
wasiwasi huo. Ukweli ni kwamba unapomuuliza mpenzi wako upo uwezekano mkubwa wa
kudanganywa kwa maneno na ni rahisi kupata ukweli kwa kupekua simu.
Pamoja
na yote niliongea katika mada hii napenda nitoe thadhari. Uanzapo kuwa na uhuru
wa kupekuwa simu utajikuta umekuwa aina fulani ya mlevi na huwezi kutulia mpaka
umepekua simu yake jambo ambalo kwa mtu ambae sie muelewa anaweza kukuona kuwa
ni mtu unaeboa na huna jambo jipya la kusisimua. Unapokuwa mlevi wa kupekua
simu ya mpenzi wako utajikuta huna raha mpaka utakapomaliza kupekuwa jambo
ambalo lina uwezo wa kupunguza uwezo wako wa kuonyesha mapenzi ambayo yatakufanya
umpende zaidi. Katika mazingira kama
hayo utakuta unaharibu uhusiano badala ya kujenga. Dada mmoja alijikuta amekuwa
mlevi wa kupekuwa simu za mpenzi wake na akaona hiyo haikutosha akaanza pia
kupekua simu ya baba ya mzazi.Ni jambo
jema lakini lazima uwe na hekima usije
ukabomoa penzi lenu.
Pamoja
na hayo yote utajikuta unakosa raha kila unaposikia mlio wa meseji inayoingia
katika simu ya mpenzi wako na hapo hapo unajikuta unatamani uikwapue simu yake
uwe wa kwanza kuisoma meseji hiyo jambo ambalo litkufanya uwe huna raha mara
kwa mara na hivyo kumboa mpenzi wako.
Kusema
kwamba unapaswa kumuamini mpenzi wako na uache kupekuwa simu yake sio sahihi.
Ili uweze kumuamini mtu lazima akupe ushahidi wa kutosha kuwa anastahili
kuaminiwa. Kama kweli mpenzi wako anakupenda atakupa uhuru wa kupekua simu yake
na pale unapoona hukuti jambo lolote
baya wewe mwenyewe utaona aibu na utalazimika kuacha labda pale ambapo kiwango
cha penzi kimepungua sana kati yenu na
hujui sababu ya hali hiyo.
Pale
uonapo mpenzi wako ana tabia ya kupekua simu yako jitahidi kuwa muelewa badala
ya kuchukia. Iwapo huko nyuma aliamini mtu na mtu huyo alimsaliti anayo haki ya
kujilinda asiumie tena. Wala sio hilo tu huenda rafiki yake wa karibu
alishawahi kusalitiwa na mwanaume mwingine
baada ya kukuta meseji inayomsema vibaya kwa mtu mwingine.na akaumia
sana. Hebu fikiria uwe na rafiki wako wa karibu sana akuletee mkasa uliomkuta
baada ya kupekuwa simu ya mpenzi wake. Hebu sikia maneno kama haya “John
usiamini wanawake bwana, unaweza kuamini kuwa awitness alikukwa anatembea na
wanaume wawili kwa mpigo? Jumapili ametoka kwangu saa 8 mchana anasema anaenda
discussion na wanafunzi wenzake na kesho yake nakuta meseji ya jana inayosema
alienda NORTH HOTEL na mwanaume mwingine. Nilimwona WITNESS mtu mpole sana na anaejiheshimu na
nikamuamini sana lakini bada ya kusoma meseji hiyo niliumia sana na sijui kama
nitaweza kumuamini mwanamke mwingine tena” itakuwa mbaya zaidi iwapo rafiki
yako huyo atakusimulia mkasa huo huku akitoa machozi mengi na akakupa kazi ya
kumfariji.
NDUGU
yangu, jitahidi kutumia simu yako kumletea mpenzi wako furaha na sio
wasiwasi.KWA kadri utakavudhamiria kutumia simu yako kujenga na kupamba penzi
kwa kumpiga mpenzi wako, kutuma mesejei tamu za kimahaba itakuwa vigumu kwako kufanya hayo kwa mtu
mwingine tofauti .Wakati umefika wa wewe na mpezi wako kufanya bidii za
makusudi kuongezea kiwango cha furaha na msisimko kati yenu kwa kutumia simu za
mkononi.
Kabla
ya kumaliza naomba nikusomee maneno ya dada mmoja yanayothibitisha umuhimu wa
kupekuwa simu ya mpenzi wako.
“Nimejikuta kuwa nashindwa kuacha
kupekua simu ya mpenzi wangu baada ya mwanaume wa kwanza maishani mwangu
kunisaliti. Niligundua kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana
wawili tofauti, wakati tayari alikuwa amekwisha nitolea mahari. Natamani ningesema
kuwa najuta kupekua simu yake lakini sijui hata kidogo. Sijuti kwa kuwa kama
isingekuwa kwa kufanya hivyo ningeendelea kuamini kuwa mwaminifu kumbe yeye
ananiona bwege kwa muda mrefu sana. Niliumia sana lakini nilijifunza somo moja
muhimu sana . Kupekua simu ndio njia pekee ya kupata uhakika na majibu sahihi
muda wangu ni wa muhimu sna na sitaki mwanume yeyote anipotezee muda wangu”.
0 Response to "JE KUCHUNGUZA SIMU YA MPENZI WAKO NI SAHIHI AU UJINGA?"
Post a Comment