DALILI ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA
Read More
DALILI
ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA
(1)
ANAKUTAZAMA
MARA KWA MARA
Mara
nyingi wanaume huanzisha hisia zao za kimapenzi kwa kutumia macho yao na hivyo
uonapo mwanaume anakutazama mara kwa mara na macho yenu yanagongana anageuza
kichwa ujue tayari ameanza kuona uthamani wako kama mpenzi.
(2) ANAJIVUTA KARIBU NAWE
Uonapo
mwanaume anatafuta kila sababu ya kutaka kuongea nawe mara kwa mara ni dalili
ya kwamba anapenda uwe sehemu ya maisha yake.Simu za mkononi inaweza kuwa
chombo muhimu sana katika eneo hili.
(3) ANAKUFAGILIA SANA
Mwanaume
anapokuwa ameona mwanamke ambaye anatamani awe mpenzi wake na mwishowe awe mke
ataanza tabia ya kumsifia mwanamke huyo sio hilo tu bali pia atajitahidi kumtia
moyo mwanamke huyo kumsogeza mahali ambapo mwanamke atajiona kuwa ni wa muhimu na
anaestahili mema na mafanikio.Hivyo basi
kumfanya mwanamke huyo kuhusisha mafanikio yake na mtu ambaye amekuwa
akimtia moyo na kumwona kuwa anaweza kushinda vikwazo vyovyote vile.
(4) MTOA ZAWADI
Mwanaume
anaekupenda atajitahidi kukutafutia zawadi nzuri wakati ambapo hakuna tukio
lolote la kisherehe. Kwa kufanya hivyo anamuonyesha mwanamke kuwa yuko ndani ya
moyo wake na ni wa muhimu kwake.
(5) MNATOKA KWA KIWANGO KIKUBWA
Mwanaume
anayependa mwanamke atajitahidi kumtoa mpenzi wake kwenda nae katika hoteli nzuri
au maeneo ya starehe yenye hadhi kubwa. Mwanaume huyo hataangalia gharama za
hayo yote na mwanamke aonyeshapo kuwa haoni umuhimu wa matumizi makubwa
mwanaume huyo atapuuzia kabisa maneno yote. Mwanaume huyo ataonekana kutokujali
muda mnaokuwa pamoja na hatakuwa na haraka ya kuondoka.
(6) HASHOBOKI
Mwanaume
ambae anakupenda atajitahidi sana asiwe anakodolea macho wanawake wengine
(hashobokei wanawake wengine na hana time na vicheche). Asilimia kubwa ya
wanaume wana udhaifu wa kukodolea macho wanawake wengine hata wakiwa na wapenzi
wao. Lakini mwanaume anayemheshimu mpenzi wake atajitahidi sana kujizuia hali
hiyo isiendelee au kuonekana awapo na mpenzi.
(7) ANAKUPENDELEA
Mwanaume
anapompenda mwanamke atajikuta kuwa anaanza kumpa kipaumbele mwanamke
aliemchagua. Anaweza asiwe na pesa lakini akiona mpenzi wake anahitaji jambo
fulani atafanya juu chini amtimizie haja yake. Mara nyingine hali hii ikiwa
kubwa mwanaume huyu anaweza kusahau hata wazazi na ndugu zake. Mwanaume huyo
atajikuta anaacha mambo yaliyokuwa muhimu kwake kuwa na mwanamke aliemchagua.
Atakusaidia hata kabla hujaomba msaada kwake.
(8) ANATAFUTA MIZIZI YAKO
Mwanaume
anapompenda mwanamke na kutamani kuwa sehemu ya maisha yake ataonekana kupenda
kujua mengi juu ya familia na ndugu za mwanamke aliemchagua. Mwanamke aonapo
maswali ya aina hiyo yanarudiwa ajue kuwa mwanaume huyo anampenda na anatafuta
uhakika wa ubora wa familia ya mke wake mtarajiwa.
(9) ANAKUCHUNGA KWA FIMBO YA WIVU
Wivu
sio kitu kibaya pale ambapo lengo lake ni kulinda kitu unachokithamini sio hilo
tu bali pale uonapo wivu wake haukunyimi uhuru wako. Mwanamke aonapo mpenzi
wake ameanza tabia ya kuuliza “Uko wapi”? “Utarudi home saa ngapi”? “Mbona
nasikia kelele uko wapi na unafanya nini
huko”? Maswali yanayofanana na hayo yanaashiria kuwa moyoni mwake tayari
amekufanya sehemu ya thamani ya maisha yake.
(10) ANACHEKACHEKA OVYO
Uonapo
mwanaume anacheka mara kwa mara awapo nawe tambua kuwa ameanza kukolea penzi.
Mwanaume anapopenda anajikuta anafurahishwa na vitu vidogo vidogo asemavyo au
afanyavyo mwanamke aliemchagua. Hali hii inaoneysha ni jinsi gani anamwona
mwanamke huyo kuwa chanzo kizuri cha furaha maishani mwake.
(11) ANAANZA KUKUNADI
Mwanaume
aonapo kuwa sasa penzi lake kwa mwanamke aliempenda limekomaa ataanza
kumtambulisha kwa marafiki zake na mbwembwe hizo zinaweza kuwagusa hata wazazi
na ndugu zake wa karibu.
(12) ANAPENDA KUKUGUSAGUSA
Mwanaume
anapokuwa amependa atajikuta anataka kuimarisha mshikamano kati yake na
mwanamke aliemchagua. Kwa kumshika mkono, kumkumbatia au kumvuta karibu yake
wawapo kati ya watu wengi ni ishara ya kuonyesha kuwa sasa hataki mwanamke huyo
atoke maishani mwake.Hilo ni tangazo la siri kwa wanaume wengine kusema
vicheche chezeni mbali.
(13) ATAKUIMBIA WIMBO UUPENDAO
Wanawake
wengi wanapenda kusikia mwanaume akisema mara kwa mara kuwa anampenda. Kwa
mwanaume aliyempenda kweli kweli atakuwa na urahisi wa kusema “Nakupenda
mpenzi” mara kwa mara. Wimbo huu ni wa muhimu sana.N muhimu kuuchukulia kama
ishara muhimu kwani Biblia inasema “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi wake
na wao waupendao watakula matunda yake. Apataye mke apata kitu chema naye
ajipatia kibali kwa BWANA (MITHALI 18:21-22).
(14) ANAKUHANGAIKIA
Mwanaume
apendaye mwanamke atajitahidi kuhangaika juu ya mahitaji ya mwanamke
aliemchagua utaona anakuwa makini hata kwa mahitaji madogomadogo mnapokuwa
mmeachana.Utakuta anamuuliza mwanamke iwapo anahitaji hiki au kile.
(15) ANAJIRUDI KWA UPOLE
Katika
mapenzi hali ya kutoelewana haiepukiki kabisa na mwanaume ambaye anampenda
mwanamke aliemchagua atatambua umuhimu wa kuomba msamaha pale anapokosea. Hata
ikitokea mkagombana haichukui muda mrefu kwa yeye kuanza kubembeleza ili
kurudisha hali ya amani. Vile vile mwanaume huyo ataonyesha heshima kwa kuepuka
lugha ya matusi au dharau ya aina yoyote ile. Hii ni moja kati ya dalili kubwa
ya penzi lenye nguvu.
(16) ANAJINADI KWA NDUGU ZAKO
Mwanaume
mwenye nia ya kumfanya mwanamke awe sehemu ya maisha yake ataanza kufanya mambo
ambayo ndugu na marafiki wa mwanamke watamwona kuwa ni mtu wa maana na mwenye
thamani. Mwanaume huyo atafanya hayo kwani anajua kuwa furaha ya ndugu na
marafiki zake itakuwa ni furaha ya mwanamke ampendae.
(17) ANAFANYA BIDII KITANDANI
Asilimia
kubwa ya wanaume wana matatizo ya nguvu za kiume na kuwahi kumaliza lakini
pamoja na matatizo hayo mwanaume ambaye amempenda mwanamke aliemchagua
atahangaika kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha kuwa mwanamke alie nae
kitandani anaridhika kabisa. Hiki ni kipengele muhimu sana cha kuangalia kwani
sayansi ya mapenzi imethibitisha kuwa asilimia kati ya 80 na 85 ndoa huingia
katika migogoro kutokana na kukosekana utamu wa kutosha katika tendo la ndoa
katika Biblia kitabu cha KUMBUKUMBU LA TORATI inaonyeshwa kuwa ni wajibu wa
mwanaume kumfurahisha mwanamke. “ mtu atwaapo mke mpya asiende vitani pamoja na
jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yoyote akae faragha mwaka mmoja nyumbani
mwake apate mfurahisha mke aliyemtwaa (Kumbukumbu la Torati 24:5) kutokana na
agizo hilo toka kwenye Biblia utaona kuwa mwanaume ambaye anashindwa
kumfurahisha mwanamke katika eneo hilo anampa haki mke wake amdharau kama
Biblia kwa mara nyingine tena inavyoonyesha”.
“Maji
mengi hayawezi kuzimisha upendo wala mito haiwezi kuzimisha kama mwanaume
angetoa badala ya upendo mali zote za nyumbani mwake. Angedharauliwa kabisa”
(Wimbo uliobora 8:7).
ULAZIMA
WA KUFANYA MABADILIKO KATIKA MAPENZI
Ukweli
ni kwamba kila mtu angependa furaha ya mapenzi aliyoanza nayo iendelee kudumu lakini
kwa wengi hiyo ni historia ya mbali na kwa wengine wanaona kuwa jambo hilo la
kuendeleza furaha siku zote haliwezekani toka nianze kazi yangu ya ushauri na
vipindi redioni nimekuwa nikikutana na kesi nyingi sana za kusikitisha na
kuumiza moyo na sio hilo tu bali hata mimi mwenyewe nimekutana na changamoto
kubwa ambazo zimenifanya niendelee kufanya utafiti zaidi kutafuta siri ya
uhusiano wenye furaha ya kudumu.
Katika
sura hii nitaonyesha mwanga niliouona na katika sura ifuatayo nitaonyesha moja
kati ya njia kuu muhimu ya kudumisha furaha katika mahusiano ya kimapenzi.
Ugunduzi huu ni wa kisayansi na naona kuwa ni moja kati ya ufunguo muhimu sana
katika mahusiano ya kimapenzi mwanadamu ameumbwa aweze kuishi kwa furaha wakati
wote jambo ambalo linaimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi na kusababisha
akili kufanya kazi vizuri zaidi. Ili kudumisha
furaha na amani mwanadamu ameumbwa na uwezo wa kurudia katika kiwango
kile kile cha furaha alichokuwa nacho mwanzoni bila kujali kama mtu huyo
amekutana na mambo mazuri au mabaya. Hali hii hutokea kwani mwanadamu hujikuta
anayazoea mabadiliko yanayomkuta yawe mazuri au mabaya ili kudumisha kiwango
kile kile cha furaha au amani. Hali hii kitaalamu huitwa HEDONIC ADAPTION na
kuna mifano inayoweza kukuonyesha jinsi gani hata wewe mwenyewe umekumbana na
hali hiyo.
(1)
Unanunua saa mpya ya ukutani na unaiweka
nyumbani na mwanzoni unasikia mlio wa saa inapotembea lakini baada ya muda
fulani unapokuwa umezoea mlio huo unajikuta huusikii kabisa.
(2)
Mtu ambaye anahamia kwenye nyumba uliopo
kando ya barabara ambapo magari mengi hupita mwanzoni anasumbuliwa na kelele za
magari lakini baada ya muda fulani anaizoea hali hiyo na kuwa na amani tele na
wala hasumbuliwi na kelele za magari kama mwanzoni.
0 Response to " DALILI ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA"
Post a Comment