MTUNZE MMEO
Anyway!!!!! |
" Here we go, mwanamke, msichana, call it any how, sijuhi ni kwanini msichana huwa anajiweka vizuri sana sana wakati wa kudate na baadaye kubadilika kabisa pale anapoona ameishampata mwandani wake aliyekuwa anamkusudia.
Kwanza kabisa mwanzoni, alizoea kuvaa kichokozi na kimatamanio ulipofika wakati wa kulala kuanzia kichwani mpaka chini, mpaka mwanaume hawezi kujizuia. alikuwa msafi, anajipenda kiasi kwamba ukimkuta nyumbani unaweza kudhani kwamba anatoka. Mmh!! midomo inaita, macho yanavuta na mwili unatamanisha, bila kusahau manukato na huku akishika nafasi yake kama mwanamke. Lakini sasa hivi akienda kulala utatamani ukimbie mana hajali tena anaonekana vipi usoni, kichwani na wakati mwingine utakuta anavaa litisheti na harufu aliyonayo hooo “lord have mercy” lakini wakati anadate viungo vyote viliongea kimahabamahaba, ubunifu wa kufanya mapenzi, lakini sasa ameishampata huyo mambo yote yamebadilika.
Yale macho ya wizi na tabasamu la aibu, sauti nyororo vyote vimemilikiwa na kununa kila wakati, midomo iliyokauka, maneno mabaya sasa anaamrisha kama mwanaume, nagging all the time. Hakuna tena nguo za kuvutia,kilasiku ni siku mbaya, nywele mbaya, na hata umbile la mwanzo limepotea, halieleweki.
Kwavyovyote mwanaume alikupenda ulivyokuwa mwanzo, na kuvutiwa na utaratibu uliojiwekea toka awali na kumzidishia hamu ya kukuona kila wakati sasa unapobadilika unamfanya mwanaume kutafuta pakutumia mda wake wa ziada, ndipo utaanza mwanaume wangu amebadilika kweli, sasa ni yeye au ni wewe wa kulaumu? Kwasababu anaona kama ametapeliwa hajui haamini kipi tena, na anahisi hawezi kumuamini tena. yule mwanamke aliyefikiri anamjua vizuri, na ikifikia hapo ndio hapo wale waliojiajiri kwaajili ya kusogeza vya watu upata ajira.
Swali ni ili je do you real want to keep your man??
0 Response to "MTUNZE MMEO"
Post a Comment