Unapoufurahia Ujuzi wa Mpenzi Wako, Hujiulizi Kautoa Wapi? - Bongo Loves

Unapoufurahia Ujuzi wa Mpenzi Wako, Hujiulizi Kautoa Wapi?

Kwetu tunaamini mchawi aliyekubuhu, ni yule aliyeuwa watu wengi zaidi. Au hata ukimuona dereva anakimbiza gari barabarani unaamini ana uzoefu wa udereva wa mda mrefu na atakuwa ameshawahi kuendesha magari mbali mbali. Sasa linapokuja swala la mahusiano, ninaona watu wanalalamika kuhusu ujuzi wa wenzi wao. Ingekuwa mimi, endapo mwenzi wangu angekuwa na kiwango kidogo cha ujuzi kwenye maswala ya chumbani, lingekuwa jambo la furaha na kheri. Pale unapotaka mpenzi wako awe na ujuzi wa PhD katika maswala ya chumbani, wewe unataka awe amejifunzia wapi? Kama unataka mjuzi, nenda kachukue Changu doa ambaye anajua michezo yote... Dada zetu waliofunzwa wakatulia, na kaka zetu au wadogo zetu waliofunzwa wakatulia technically watakuwa na ujuzi mdogo na over the time katika maisha yao ya mahusiano (ndoa) wataweza kujifunza na kuimprove. Ukimpata yule anayekupeleka puta, inabidi ukae chini na ujiulize atakuwa amewapitia au amepitiwa na wangapi mpaka akapata utaaalam huo? NB: Sio wote wenye utaalam wa chumbani wanahistoria ndeefu (mbaya) ya kwenye mahusiano...USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍

0 Response to "Unapoufurahia Ujuzi wa Mpenzi Wako, Hujiulizi Kautoa Wapi? "

Post a Comment