DAKTARI ASHTAKIWA KUWAPA WAGONJWA SUMU - Bongo Loves

DAKTARI ASHTAKIWA KUWAPA WAGONJWA SUMU

Uchunguzi wa uhalifu umeanzishwa dhidi ya daktari wa Ufaransa anayeshutumiwa kuwapasumu watu 17 nchini Ufaransa. Frédéric Péchier, ambaye ganzi ya nusu kaputi wakati wa upasuaji tayari amechunguzwa kwa visa vingine saba vya kuwapa sumu watu tisa ambao walikufa. Waendesha mashtaka katika kesi yake wanasema alimgonga kwa makusudi na daktari mwenzake mifuko ya dawa ya ganzi ili kusababisha dharura ili aonyeshe utaalamu wake. Bwana Péchier anayekanusha madai yote, anakabiliwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia. Wakili wake, Jean-Yves Le Borgne, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba uchunguzi haujathibitisha lolote. " Kuna uwezekano kwamba Dkt Pechier alilitoa sumu lakini hizi ni tathmini za nadharia tuu ," alisema Bwana Borgne. " Lazima suala la kutokuwa na hatia lisisitizwe." Jaji aliyemuhoji katika mshukiwa katika mji wa mashariki wa Besançon alimshinikiza kwa maswali Dkt Pechier , mwenye umri wa miaka 47, wakati wa uchunguzi mwezi Mei 2017 juu ya madai ya kuwapa sumu watu saba. Daktari huyo baadae aliachiliwa lakini akapigwa marufuku asifanya shughuli zozote za kitabibu. Wiki hii alihojiwa na polisi juu ya matukio 66 ya wagonjywa waliopatwa na mshituko wa moyo waliokuwa katika hali ya chini ya hatari.Shutuma za hivi karibuni zinatokana na mkesi hizi zinazowahusisha wagonjwa wenye umri wa miaka minne hadi 80. Dr Thomas Muyombo anayejulikana pia kama Tom Close Mwendeshamashtaka Etienne Manteaux aliviambia vyombo vya habari nchini Ufaransa kwamba Péchier amekuwa "mtu mwenye matamshi ya ukatili" kila mara na amekuwa na mzozo na wenzake kazini. " Mara nyingi amekuwa akipatikana karibu na chumba cha upasuaji wa wagonjwa" wakati matukio ya utoaji sumu yalipotokea, alisema Bwana Manteaux, na mara moja alitoa suluhu la hatua inayopaswa kuchukuliwa , "hata wakati hakuna sababu yoyote inayomwezesha mtu kushuku kuwa mgonjwa amepewa kiwango cha juu cha dozi ya dawa ya potassium au sindano ya ganzi". Bwana Péchier amekana madai, na wakili wake amewashutumu polisi kwa kupotosha taarifa aliyoitoa wakati alipohojiwa kwa mara ya kwanza. " Matokeo yoyote yatakayotolewa ya jambo hili taaluma yangu imeisha," aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi.USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍

0 Response to "DAKTARI ASHTAKIWA KUWAPA WAGONJWA SUMU"

Post a Comment