FANYA HAYA KUMNASA MWANAMKE ILI AKUPENDE DAIMA
Read More
Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au
msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia
mwanamke yeyote.
Hapa kuna njia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;
1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu
kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii
ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.
2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na
kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na
kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa
ukizungumzia.
3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu
yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa
bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni
wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko
sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa
nazo makini.
4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa
sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite
zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa
unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na
msisimko na starehe wakati ukonae.
5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke
huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa
ukaribu.
6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi
unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa
makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.
7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume
anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu
atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi.
Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.
8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au
msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya
kumuuliza maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza
mawazo yako kuhusu vitu flani.
9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe
umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii
itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.
10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako,
onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu
yeyote.
Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia
sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia,
isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua
ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda
kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa
maoni yako hapa.
MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji
mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako
na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana.
0 Response to "FANYA HAYA KUMNASA MWANAMKE ILI AKUPENDE DAIMA"
Post a Comment