MAMBO HUBADILIKA MKISHAOANA NA KUANZA KUISHI PAMOJA. - Bongo Loves

MAMBO HUBADILIKA MKISHAOANA NA KUANZA KUISHI PAMOJA.


Watu wawili wanaopendana na kuishi kila mmoja kivyake ni tofauti sana na watu wanaopendana na kuishi nyumba moja.
Wapo ambao hujiuliza inakuwaje wapenzi wawili waliokuwa wanapendana na kuwa na moto wa mapenzi wa kiwango cha juu sana wakianza kuishi pamoja mambo huanza kubadilika? Pia wapo ambao hukubaliana kwamba baada ya kuoana na kuishi pamoja watajitahidi sana kuhakikisha wanapendana kama mwanzo hata hivyo baada ya kuanza kuishi pamoja hujikuta wamekuwa dada na kaka na hakuna moto wa mapenzi tena.

Jambo la msingi unatakiwa uwe makini kwani kuishi kila mpenzi kwake ni tofauti na kuishi na mpenzi nyumba moja na kitanda kimoja.
Pia wapo wanaume au wanawake baada ya kuoa au kuolewa hufikiria na kuamini kwamba wale wameoana nao si wazuri kama wale walioko nje hata hivyo ukweli ni kwamba kwa kuwa huishi naye masaa 24 kwa siku Ndiyo maana unaona ni mzuri, ukiishi naye kwa saa 24 siku 365 kwa mwaka ndo utajua ni tofauti kabisa.

Inawezekana wakati mnaishi tofauti na mpenzi wako ilikuwa ni kulala saa sita au nane usiku kwani mlikuwa mnapigiana simu na kutumiana sms kiasi ambacho hamkulala hata hivyo baada ya kuoana sasa kila mmoja anakuwa sehemu ya maisha ya mwenzake kila siku inayopita duniani.

Sasa unalala naye, unaamka naye na kula chakula naye. Mnamiliki sebule moja, chumba cha kulala kimoja na kitanda kimoja, frji moja nk. Unajifunza tabia zake kwa undani, unajifunza nini anapenda na nini anachukia, unajifunza udhaifu wake na uimara wake unajua nini anapenda kwenye TV na zaidi rafiki zake watakuja kwenu upende usipende na kufanya au kuongea mambo yao.
Simu za rafiki zake zitapigwa kwenu, utakuwa domesticated man au domesticated woman.

Unapoishi na mtu mwingine taratibu hubadilika, masuala ya sex yatabadilika kwani utalazimika kufahamu hisia zake kimapenzi mahitaji na kile anapenda siku zote na wewe kuwa mbunifu maana unaye kila siku.

Pia unatakiwa kuripoti kila siku kama utachelewa kurudi nyumbani utalazimika kumwambia mapema. Lazima utambue kwamba sasa utakuwa na mtu ambaye ana hofu na wewe kuchelewa au kutokupata habari zako ndani ya saa 6 mchana na huruhusiwi kwenda kimya hadi sita usiku bila yeye kujua upo wapi na kama ni salama.

Pia kuishi pamoja ni kujifunza kuwa kitu kimoja na usipokuwa makini unaweza kujikuta excitement zote za nyuma zinaisha na maisha yanakuwa tofauti na yale kabla ya kuishi pamoja.
Unahitaji kuwa mbunifu wa namna ya kufanya kila siku inayokuja duniani ili mambo mazuri yanayofanya kila mmoja kuwa excited na mwenzake la sivyo badala ya kuishi kama wapenzi mtaishi kama dada na kaka wanaolala pamoja na ambao moto wa mapenzi umezima.

0 Response to "MAMBO HUBADILIKA MKISHAOANA NA KUANZA KUISHI PAMOJA. "

Post a Comment