JINSI YA KUJUA KAMA MWANAMKE ANAKUPENDA KWELI!
JINSI YA KUJUA KAMA MWANAMKE ANAKUPENDA KWELI!
7:57 AM
Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupena kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na kuzifanyia kazi;
1. Mwanamke anayekupenda atakuwa tayari kujitoa muhanga kwa ajili yako yaan kujitoa kafara, vipo vitu ambavyo watu hawawezi kuvifanya ila isipokuwa kwa wale wanaowapenda kwa moyo wote. Je wewe ni sehemu mojawapo ya vitu vichache anavyovipa kipaumbele? Je, wewe unakuwa wa kwanza mbele ya marafiki zake? Je, anakufanyia vitu ambavyo hawezi kuwafanyia wanaume wengne? Je, ameacha mambo mengine ili aweze kuwa na wewe? Ni kwa vitu kama hivi unaweza kutambua wewe ni wa muhimu kwake.
2. Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, mtu anayekupenda atahangaika juu ya usalama wako, raha yako, heshima yako na maendeleo yako. Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke uliyemlenga anakupenda kweli.
3. Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa, ingawaje wivu mara nyingine unaweza kuvuruga penzi endapo utazidi. Wivu ni ishara kuwa anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza, anaogopa usije ukatoka katika maisha yake, au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.
4. Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia wewe macho (namaanisha uso wake haraka sana). Kufanya hivi ni kuonesha kuwa anakuhesabia wewe kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake. Zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.
5. Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine. Mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa ” ANAKUHITAJI”.
6. Mwanamke anayekupenda atajitahidi apendekeze kwa kuvaa vizuri pale anapojua kuwa atakutana na wewe, atajali sana juu ya nywele zake, nguo zake na hata anavyonukia, yaani atajipulizia pafyumu.
7. Mwanamke anayekupenda ataonesha dalili za kupenda kuwa karibu yako katika mazungumzo au maeneo mengine, atapenda mara nyingi kuwepo katika maeneo unayopendelea na pia sauti yake itabadilika kuashiria hali ya kukupenda na kutaka kukuvuta kwa sauti yake
0 Response to "JINSI YA KUJUA KAMA MWANAMKE ANAKUPENDA KWELI!"
Post a Comment