NIMETOA PENZI KWA SHEMEJI BILA KUTONGOZWA, IMENIUMA SANA
Ni rafiki yake na aliyekuwa mtu wangu kwani baada ya mtu wangu kufariki kwa ajali mwishoni mwa mwaka jana amekuwa karibu sana nami, ukaribu huu haukunitia mashaka kwani kipindi bado mtu wangu yupo tulikuwa tukiambatana naye sehemu mbalimbali zikiwemo za starehe na hata kwenye shida pia.
Sasa baada ya kumaliza msiba amekuwa akinitumia pesa kidogo kidogo kwani nasoma nje ya mkoa tunaoishi hasa siku za weekend na kuniambia "mwanafunzi nenda kapate mbili tatu maana najua ulikuwa umeshazoea", na kwa sababu tumekuwa kama family friend kwa muda mrefu sikutilia shaka hata kidogo. Toka mwezi wa kumi hadi juzi ndo alikuja kikaz huku ninakosoma na ndo haya yakanikuta.
Jana akataka kinitoa out kwa kwa kuwa kwa sasa tuko kwenye maandalizi ya mitihani inayoanza jumatatu nikamtaka iwe jioni kwani muda wa mchana na asubuhi nitakuwa najiandaa kwa kujisomea, akasema na ndio utakuwa muda mzuri kwani hata yeye atakuwa ameshatoka kwenye semina pia.
Ilipofika jioni tukakubaliana tukutane kwenye resort moja hivi ambayo pia huwa kunakuwa na performance ya live band, na kweli ikawa hivyo kwa hiyo tulikula na kunywa pia. Muda wa kuondoka ulipofika dala dala zikawa zimeisha barabarani na kwa boda boda ni mbali kiasi kwamba ingeweza leta shida kwani nilikuwa nimelewa pia, tax kwa umbali ule ingekuwa ni gharama sana hivyo akanitaka niambatane naye hadi hotelin alikofikia kwan haina tatizo.
Kwa kuwa hata siku za nyuma nilishawahi kumsikia akisema kuwa yeye kama hajaamua kufanya mapenzi hawez kufanya hata kama atalala na mwanamke kwa mwezi mzima nikaamua kumwamini na isitoshe yeye ni shemeji kwa upande mwingne sikuhofia lolote.
Tukaingia kulala japo sikuvua nguo nililala na nguo zangu, sijui ilikuwaje mpaka ikawa hivyo sielewi nieleze ilikuwaje na hivi nilikuwa na pombe kidogo kichwani sielewi jamani,
Inaniuma sana kwani angenitongoza nisingemkubalia hata kidogo lakini ndo imekuwa hivyo,
nimechanganyikiwa, mke wake ni rafiki yangu sana hata sijui nifanyeje maana nikisema nimwambie nahatarisha ndoa yao, nikipiga kimya akijaga kujua itanielewaje, mwanangu na wanaye ni marafiki kiasi kwamba hata shule wanaenda kwa gari moja, nishaurini mwenzenu hata sijui nifanyeje.
nimechanganyikiwa, mke wake ni rafiki yangu sana hata sijui nifanyeje maana nikisema nimwambie nahatarisha ndoa yao, nikipiga kimya akijaga kujua itanielewaje, mwanangu na wanaye ni marafiki kiasi kwamba hata shule wanaenda kwa gari moja, nishaurini mwenzenu hata sijui nifanyeje.
Na kuhusu huyu shemeji yangu nifanyeje kwani siku zote walishasema muonja asali haonji mara moja hapa nimechanganyikiwa kiasi kwamba hata kujiandaa na mitihani tena siwezi na ndo inaanza jumatatu.Naumia sana hapa nilipo nimekosa uelekeo kuninusuru na hili janga.
Naombeni ushauri.
0 Response to "NIMETOA PENZI KWA SHEMEJI BILA KUTONGOZWA, IMENIUMA SANA"
Post a Comment