KANUNI ZA KUISHI NA MWANAMKE
Naomba nizungumze na wewe kidume mwenzangu, ambaye huelewi namna ya kuishi na mwanamke kwa akili. Nimesema kuishi na mwanake kwa akili, naam, ndiyo ewe mwanaume unayesoma makala haya ni kwamba katika maisha yako utakayoishi hapa dunia hakuna kiumbe unachotakiwa kuishi nacho kwa akili kwa mwanamke.
Ni kweli usiyohitaji mwanga wa jua juu ya hilo. Mwanamke usipoishi naye kwa akili ni kwamba mahusiano yenu hayatadumu hata iweje labda ukatambike. Pamoja na maudhi waliyoumbwa nao viumbe hawa unatakiwa kuyaelewa na kwenda nayo sawa kwani pindi utakapofanya kinyume chake ni kwamba hautadumu na kiumbe huyo.
Labda twende tukaone kanuni za kuishi na Mwanamke kama ifutavyo;
Kwanza usimpige mwanamke, Naam nazungumza na wewe hakuna mwanamke ambaye anapenda kupigwa na mumewe, labda uende mkoa wa Mara, kwani huko ndiko wanakosema ukipigwa ndiyo upendo, sina ushahidi na hilo kwani hayo ni maneno ya kuambiwa tu.
Kuna baadhi ya wanaume hudhani kumpiga mwanamke kunasaidia, hapana kitendo hicho hakisaidii hata iwaje kwani hata kisheria ni tabia isiyofaa hata chembe. Upendo wa kweli hujengwa na misingi imara ya upendo wenyewe na si kupigana.
Usimtukane na kumshushia heshima, Kila wakati hakikisha ya kwamba unapambana ili kuukuza upendo baina yako na mpenzi wako. Hautakiwa kuonesha unamjali mpenzi wako mkiwa wawili wakati mwingine ukiwa na marafiki zako unamshushia heshima mpenzi wako kwa kusema maneno yasiyo na heshimam kumuhusu yeye mbele ya marafiki zako. Mambo yenu wawili basi yabaki kuwa ni ya kwenu pekee, usiwalishe marafiki chakula ambacho mlipaswa kula wewe na mpenzi wako. Kila wakati unatakiwa kuhakikisha heshima inafuata mto msimbazi, hapa nimetia chumvi ila huo ndiyo ukweli halisi.
Usimfanye ajihisi hapendwi na anamkosi, kila mwanamke anapendwa kupendwa, hivyo kila wakati unatakiwa kuonesha kwamba unampenda mwanamke uliyenaye katika mahusiano yenu, usioneshe kwamba humpendi kwani kufanya hivyo kutamfanya ajihisi ya kwamba dunia hii haina usawa kwani atajihisi hakuna anayempenda na kila wakati ana mkosi katika sayari hii.
Usimsaliti na kujionyesha kabisa kwamba una saliti, usaliti ni mbaya na maumivu yake hayana dawa, kama unalitambua hilo basi kila wakati tulia na huyo mwanamke uliyenaye kwani kufanya hivi kutamfanya mwanamke huyo naye atulie na wewe. Usaliti huleta magonjwa na pia huleta mitafaruko mikubwa katika mahusiano ya kimapenzi hivyo ili uweze kuishi vyema na mwanamke hatimaye mfikie malengo yenu mnatakiwa kuhakikisha ya kwamba hamsalitiani hata iwaje.
Mpe zawadi, hata kama ni ndogo kiasi gani kwake ni alama tosha. Zawadi ni zawadi hili ndilo unapaswa kulielewa. Zawadi ni surprise kwa huyo unayempenda. Hakuna kitu ambacho huongeza alama kubwa kwa mwanamke kama ukimpa zawadi. Pindi unapompa zawadi mwanamke uliyenaye ni kwamba mwanamke huyo ataona uthamani wako kweke na pia ataongeza mahaba na wewe.
Mpaka kufikia hapo Muungwana blog hatuna la ziada tunachotaka tu kukusihi ni kwamba kila wakati hakikisha unayazingatia hayo vyema kama kweli unataka kuwa mtu mwenye maisha bora na yenye furaha katika mahusiano yenu ya kimapenzi. Tukutakie siku njema na mafanikio mema.
Na; Benson Chonya.
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en
0 Response to "KANUNI ZA KUISHI NA MWANAMKE"
Post a Comment