Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki - Bongo Loves

Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki


Misingi mingine ya ndoa zetu ni migumu sana.
Pata simulizi hii toka Marekani.
Smith na mkewe hawajawahi kuwa na mzozo ndani ya miaka 25 ya ndoa yao. Jambo hili likamfanya jirani yao mmoja kumuuliza Smith amewezaje kuishi na mkewe muda huo wote bila kuzozana! ??
Smith anaeleza:
👉 Tulienda fungate Australia miaka 25 iliyopita, Wakati mke wangu akiwa amempanda farasi, Farasi aliruka na mke wangu akaanguka,
Aliamka akampigapiga farasi kwa upole akasema, "hii ni mara yako ya kwanza"
Baada ya muda ikatokea tena, Alimpigapiga tena na kusema, "hii ni mara yako ya pili"
Farasi alifanya tena mara ya tatu, Mke wangu alitoa silaha na kumuua yule farasi!!!
Nilishitushwa sana na kitendo kile nikamgombeza mke wangu,
- umechanganyikiwa?,
- una matatizo gani?,
- kwa nini umemuua farasi?
Mke wangu aliniangalia, akatabasamu, kisha akasema, "hii ni mara yako ya kwanza"
Tangu siku hiyo nikaushona mdomo wangu,
Hii ndiyo siri ya kuishi miaka yote hii bila kuzozana! 👈
😂 😂 😂

0 Response to "Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki"

Post a Comment