DALILI ZA MPENZI ALIEBOREKA NA WEWE
Read More
Mahusiano
mengi sana yapo katika hali ya kusikitisha, na wengi hawajui wamefikaje fikaje
katika hali hiyo jambo ambalo linatisha. Unapokutana na hali ambayo hujui jinsi
ya kuiondoa, inatisha sana na ni sawa sawa na mtu ambae ameanguka kwenye dimbwi
refu la kuogelea wakati huo na yeye hajui kabisa kuogelea. Jambo la ajabu
katika mahusiano mengi ya kimapenzi ni kwamba mtu anaweza kuwa ameboreka na
mpenzi wake lakini hajui afanye nini kubadili hali hiyo mbaya, na mbaya zaidi
akashindwa hata kutafuta njia za kuibadili hali hiyo. Ukijua kuwa mpenzi wako
ameboreka unaweza kuanza kutafuta njia za kumsaidia achangamke lakini usipojua
hilo na ukaendelea kama vile hakuna tatizo unakaribisha majanga katika uhusiano
wenu.Matokeo hayo nayaona pale mteja anaponiambia kuwa mpenzi wake
kabadilika na sababu haijui na anaumia
kwa kuwa anampenda sana.
Unapohisi kuwa
mpenzi wako ameboreka upo uwezekano mkubwa kuwa ni kweli ameboreka na haijalishi
kama kosa ni lako au la kwake au mchanganyiko wa yote ya kwako au yak wake hiyo
ni hali ambayo inahitaji ufumbuzi haraka.
Zifuatazo
ni dalili kuwa mpenzi wako ameboreka na wewe au na uhusiano wenu kwa ujumla:
1)
Pamoja
na bidii yako kubwa bado mpenzi wako anaonekana kama akili yake ipo sehemu nyingine
ofauti kabisa. Katika mazingira kama
haya ndio unasikia mtu unasema “Mpenzi wangu simuelewi” unampigia simu
hapokei kwa wakati na anachelewa sana kukupigia. Unamtumia SMS nzuri za
kimahaba lakini yeye anajibu kikavukavu tu, ukiuliza kitu basi anatoa majibu
mafupi mafupi au mkato mkato.
2)
Mara
nyingi anakuwa mzito kukujulisha nyendo zake au mizunguko yake na pindi ukihoji
juu ya mwenendo wake anakuwa mkali.
3)
Ameanza
kukulinganisha na wanawake au wanaume wengine bila kujali hisia zako.
4)
Hapendelei
kukuita kwa majina ya kimahaba kama baby, honey, mpenzi n.k. Pia hapendelei
muongelee juu ya kiwango cha penzi na ubora wake.
5)
Unapokuwa
na jambo linalo kuhuzunisha au kukukosesha raha haangaiki kukufariji. Huzuni
yako au maumivu yako hayasumbui nafsi yake.
6)
Uso
wake hauonyeshi uchangamfu kama pale mwanzoni. Uonapo mpenzi wako anapokuwa na
wewe uso wake upo kama vile amesikia mtu alietoa hewa mbaya, tambua kuwa
ameboreka na wewe kwa kiasi kikubwa.
7)
Uonapo
anakasirika sana kwa mambo madogo madogo na hali hiyo ikawa inajirudia rudia
hiyo ni ishara kuwa amekuchoka. Na iwapo mara kadhaa katika mazingira kama hayo
anasema mambo yanayoonyesha kuachana na wewe hiyo ni haja ya moyo wake basi tambua kuwa
yasipotokea mabadiliko kifo cha uhusiano wenu hakiko mbali. Mara nyingi hali
hiyo huambatana na maneno yanayokatisha tamaa.
8) Anakwepa
mada zinazohusu madhaifu au mapungufu yake. Uonapo kuwa mpenzi wako hapendi
mzungumzie kwa kina mambo yanayoharibu ubora wa uhusiano wenu maana yake haoni
sababu yoyote ya kupoteza muda wake katika kujenga uhusiano wenu, yaani
ameishiwa nguvu za kujenga na kupamba uhusiano wenu.
9) Mpenzi
wako anapendelea zaidi kuchati na marafiki zake kuliko kuongea na wewe muwapo
pamoja. Lingine linalofanana na hilo unakuta mpenzi wako anapendelea zaidi
kuangalia TV kuliko kuongea na wewe muwapo pamoja. Hali hii ikiendelea
mtajikuta mnaishi kama vile ni kaka na dada yake.
10) Ameanza kutumia maneno
makalimakali pale unaposema bila kujali hisia zako au amekuwa mtu wa kufoka
foka na kuguna guna.
11) Uvaaji wake unakuwa wa hovyo
hovyo na hajali sana kupendeza katika uvaaji wake. Ukiwa na mpenzi kama huyo na
ghafla ukaona ameanza kuvaa vizuri maana yake amepata mchepuko.
12) Ni mara chache sana mmetoka
pamoja kwa chakula au vinywaji au hapendi muonekane pamoja.
13) Husikilizwi kikamilifu; Ni
kweli hakuna mtu anaependelea hali ya kubishana bishana lakini kuna wakati hali
hiyo inajitokeza na jinsi mpenzi wako anavyo kabiliana na hali hiyo itakupa
picha ya mtu alieboreka na wewe na hategemei faida yoyote ya majadiliano ya
aina yoyote. Pale mpenzi wako anapoanza kukatisha mazungumzo yenu kwa kusema “Yaishe” au “Kila siku jambo lile lile tu” au “Sitaki kelele zako” tambua kuwa umekuwa kero kwake japo hoja yako
ni halali kabisa. Kama vile hakuna mtu ambae anapendelea kula chakula
kilichopikwa lakini hakikuiva hakuna mtu anaefurahia kuona haja yake ya kutoa
yote yaliomo moyoni imekatishwa kwa sababu zisizo halali. Mpenzi anaekupenda
atakusikiliza kilio chako bila kujali ni marudio kwa kuwa anaheshimu hisia
zako.
14) Kaacha mambo yanayokusisimua;
Mtu alie boreka na wewe utamuona ameacha kukupa surprise za hapa na pale na
amekuwa mwepesi wa kuahirisha mambo mliokubaliana.
15)UCHEZAJI wa ngoma ya wakubwa umeanza kupungua; Chakula ambacho
kimeanza kuchacha kinagundulika kutokana na kubadilika kwa ladha yake jambo
ambalo linakuondolea hamu ya kula chakula hicho. Uonapo mpenzi wako amepunguza
bidii yake katika kuhakikisha unaridhika na tendo la ndoa tambua ngoma hiyo
imechcha na ameanza kuboreka katika eneo hilo na pia uonapo analeta visingizio
vyenye ulemavu ili kuepuka kucheza na wewe ngoma ya wakubwa ni dalili ya hatari
sana..
Ndugu
yangu,usijidanganye kwa kusema mapenzi ndivyo yalivyo wakati huna raha na uhusiano uliomo. UPO uwezekano wa kuleta mabadiliko mazuri kama
vile wahenga walivyosema penye nia pana
njia.Tafuta njia ya kumsaidia mpenzi wako aelewe umuhimu wa kufurahiana katika
uhusiano uliomo kinyume na hapo utaishi kama mtumwa kwani hisia zako
haziheshemiwi.
0 Response to "DALILI ZA MPENZI ALIEBOREKA NA WEWE "
Post a Comment