JINSI YA KUFANYA ILI KUMVUTIA MWANAUME MNAPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA.
Ukweli kila mwanamke hutuma signal kwa mwanaume na wanaume wengi huweza
kufanya detection ya hizo signal kwa sekunde tu na signal za kwanza
ambazo mwanamke huzituma na kupokelewa na mwanaume ni mwonekano na lugha
ya mwili.
Ni rahisi mno kwa mwanamke kumvutia mwanaume kwani wanaume huvutiwa sana
kwa kile wanaona, hata hivyo jambo la msingi kwa mwanamke ni kufahamu
kwamba ni aina gani ya attention anahitaji kutoka kwa mwanaume kwani
wavuvi huamini kinachodhihirisha aina ya samaki utakayemkamata ni aina
ya chambo unayotumia.
Je, unahitaji mwanaume kuvutiwa na wewe kama mwanamke (person) au kama
chombo cha starehe (an object) hivyo basi ni muhimu kuzingatia mambo ya
msingi ili kupata kile unahitaji.
Mwanamke kujiamini ni jambo la kwanza na msingi kabisa kwa kumvutia
mwanaume, kujiamini wewe mwenyewe na mazingira yanayokuzunguka huweza
kumvutia mtu anayefanana na wewe, pia utajisikia na kuona watu
wanavutiwa na wewe pia.
Mwonekano wako (appearance) ni jambo la msingi sana, mwonekano wako na
jinsi unavyotumia mwili wako kuongea huvutia sana hata hivyo ili
uliyemvutia abaki na wewe unahitaji personality na uchangamfu.
Pia Kumbuka kwamba jinsi unavyoonekana na kufanya pale mnakutana kwa
mara ya kwanza ni muhimu sana kwani akikutana na wewe wakati upo ovyo
kuliko wakati wote hawezi nkupoteza muda kuwa na wewe tena (first
impression)
Pia hakikisha unampa mwanaume sababu ya msingi ya yeye kukufikiria wewe,
hapo inabidi uwe mbunifu kuhakikisha milango yake ya fahamu itafanya
akukumbuke, mwanamke hupendeza akivaa nguo soft, pia kuvaa smile usoni
kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa yeye kukuondoa kwenye mind yake.
Jitahidi kuhakikisha anajisikia yeye ni very important, elekeza akili
yako kumsikiliza na pia respond kwa kile anaongea na ku-respect mawazo
yake. Cheka wakati anatoa jokes zake hata kama jokes zake hazina kichwa
wala miguu hapa ni kuwa na interest kwenye interest zake.
Na mwisho usithubutu kuvaa kitu kingine na ukasababisha yeye ku-fall in
love na sanamu kwani siku akikugundua wewe halisi hapatatosha. Onyesha
originarity yako na kwamba ni wewe kamili na si mwingine katika haiba,
akili na tabia.
Share this post
0 Response to "JINSI YA KUFANYA ILI KUMVUTIA MWANAUME MNAPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA. "
0 Response to "JINSI YA KUFANYA ILI KUMVUTIA MWANAUME MNAPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA. "
Post a Comment