WASICHANA NA USHIRIKINA - Bongo Loves

WASICHANA NA USHIRIKINA


Wasichana walio wengi wamekuwa wateja wazuri sana kwa waganga wa kienyeji, wamekuwa wakishirikisha  mahusiano yao na ushirikina. Na hayo ni mazoea na kutojiamini katika mapenzi, ambayo inapelekea msichana kutafuta utaalamu kutoka kwa waganga wa kienyeji. naweza kusema mwanaume ndio chanzo cha haya yote i strongly say that. nilishawahi kuona mwanaume akiwa na wasichana wanne na wote alienda kutoa mahali, sasa hapo utaona wasichana watatu lazima waumizwe au wote wanne, hapo matokeo yake ni nini? au msichana alitolewa mahali na vitu vyote tayari ikiwa ni pamoja na gauni la harusi lakini chakushangaza siku ya mwisho akaolewa mwingine, ooh! kuna ya kushangaza mengi sana, kubwa ambalo limefanya wasichana wengi kujihusisha na ushirikina ni kutokujiamini, kuhachwa mara kwa mara, kukosa imani na mpenzi wake,na pia kujijengea uhakika katika mahusiano kwa kufanya ushirikina.

Mwanaume amekosa uhaminifu katika mahusiano na msichana amekuwa ni mtu wa kujituma ili kumridhisha mpenzi wake, lakini mwanaume doesn’t give a damn.Katika mapenzi utaona hata kama utakata viuno na utaning’inia mpaka juu ya feni lakini bado atatafutwa shalon kuendeleza, madai ni kubadilisha mboga. My dear utazunguka butcher zote nyama ni ileile. Na pia msichana atahakikisha anamtunza mpenzi wake kwa hali na mali na hata kuhakikisha mwanaume wake amependeza lakini cha ajabu utakuta amependezeshea wengine wanakula kiulaini. Mwanaume!! kama kuna mapungufu kwanini husikae na mpenzi wako muambie nataka hivi, napenda kile nahitaji hiki na msichana ni mtu wa kutii sikuzote. lakini kama suluhu ni kutoka nje basi naweza kusema nyie wanaume ndio mnaowatengenezea waganga soko.
Na ww msichana jiweke darasani, peleleza, kujua mpenzi wako anapenda nini na what drives him crazy,jiongezee ujuzi zaidi kwenye mapenzi kitandani, maneno mazuri na laini ya kumtoa nyoka pangoni, punguza mdomo,mbembeleze na kumlea mwanaume kama mtoto mdogo, yote hayo ukiyatekeleza mwanaume atakuheshimu na kukuthamini sikuzote.
Msichana jihepushe na mambo ya ushirikina kwasababu utakapoanza tu ni vigumu sana kuhacha na utabaki kuwa mtumwa wa mapenzi sikuzote, maana lazima u renew mara kwa mara sasa huo si utumwa? je  Unaamini Ushirikina?? ladies ni nini kifanyike ili kupunguza hili kama sio kuzuia kabisa?,USHIRIKINA ndio suluhisho la tatizo hili??

0 Response to "WASICHANA NA USHIRIKINA"

Post a Comment