MAPENZI NI BAHATI AU JITIHADA
Ni kwanini baadhi ya wasichana wameonyesha kuwa na bahati kwenye mapenzi na wengine kuonekana kuweka jitihada zaidi?
Baadhi ya watu wameonekana kupata wenza wao wakiwa na umri mdogo ambapo imeondoa jitihada kwao na mapenzi ya kuachwa kwenye mahusiano kama wasichana wengine.
nimekuwa nikijaribu kuongea na wasichana mbalimbali ambao kwakweli wameonekana kupingana kabisa na dhana ya msichana kujilazimisha kwa mwanaume kwa njia yoyote ile, na kusisitiza kwamba ni mbaya sanaa to struggle for love, kama mtu hakupendi hakupendi tu na huwezi kulibadilisha hilo ni bora upate maumivu ya mwilini kuliko kuwa na maumivu ya moyoni wakati wengine wakinipa msemo usemao mtaka cha uvunguni sharti uiname na kusisitiza mwanamke kujishughulisha. lakini pamoja na hilo bado msimamo wangu uko palepale kwamba kwa kipindi cha sasa mapenzi yamepewa maana nyingine kabisaa kiasi kwamba kuna jitihada zaidi iliyofanywa na wasichana ambao tayari wamekwishaolewa. Asilimia kubwa ya wanaume kwa kipindi hiki wanaangalia pesa au connection kutoka kwa familia ya msichana na jitihada zaidi na sio tabia kama hapo mwanzo.
Kama sifa ya kumuoa msichana ni utajiri na familia inayojiweza hakukuhakikishii uhamisho wa utajiri na ndoa yenye furaha. Muoe msichana kwa jinsi alivyo nasio kwakile alichonacho au hadhi yake katika jamii. Ndoa si jukwaa kwa ajili ya ubinafsi na tamaa ya kufikia binafsi.
.Jambo la pili kama lengo la msichana la kufanya jitihada kuolewa ni kwasababu umechoka kuwa peke yako, kuolewa for the sake! Au kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara basi utakuwa umejenga ndoa yako kwenye msingi mbovu.Cha msingi ni mapenzi juu ya watu wawili, wote mkiendana kwa tabia na kusikilizana bila kuelemea upande mmoja.
Najua na wewe una mtazamo wako!!
0 Response to "MAPENZI NI BAHATI AU JITIHADA"
Post a Comment