MVUTIE MPENZI WAKO - Bongo Loves

MVUTIE MPENZI WAKO


Kuna hali ya kumpenda mtu unapomuona tu kwa mara ya kwanza, huenda ukawa umevutiwa na sehemu Fulani ya mwili wake na hili ndilo watu husema mapenzi ya kushindwa kujizuia unakuwa kama umepagawa na mapenzi.Ni mbaya sana kuoa au kuolewa kwa msingi kama huu kwasababu itaishia pabaya. Kwahiyo kama utaamua kuoa ama kuolewa na mtu Fulani kwa msukumo  wa hisia ulionao, kwahiyo hiyo ndoa yako itazimika pale pale kwakuwa hisia zilizokupeleka mwanzoni  zitatoweka baada ya kupata kile ulichokuwa umetarajia kukipata. Na tunajua kwamba ndoa nyingi sana zinajengwa juu ya hisia za mwili. Sasa basi kama hisia zako ziko juu kwa ajili ya kupata mwenza, utakimbilia swala la kuoa au kuolewa na pindi tu fikira zako au hisia zako zikiisha, ndoa itageuka kuwa kama gereza la mfungwa na inapofikia hapo unaelewa maana yake ni nini. Kuna wanandoa ambao wakiisha kuoana tu wanaishia kuchukiana kwenye mwaka wa kwanza tu hawana hamu tena. Naweza kuuita huo ni mlipuko wa hisia za mapenzi hapo mwanzoni na  hauwezi kudumu hata kidogo.
Kwahiyo tunaweza kuona upendo halisi ni pale mnapoelewana na kufahamiana na kuwa na maamuzi ya kuishi pamoja ambapo kuna kujali,kusaidiana,kushirikiana kwa kila jambo. Ni kuwa na moyo wakati wa shida na wa raha na unapenda na kuahakikisha hakuna kitu kitakachowatenganisha zaidi ya kifo.
Kila mtu huwa ana mtazamo wake, je wewe mtazamo wako ni upi katika hili?

0 Response to "MVUTIE MPENZI WAKO"

Post a Comment