VACATION NA MAPENZI
heylow pipo!
nadhani nikiongelea 'vacation' watu wengi mnanipata. kwa niliowaacha kidogo na haka ka umombo maana ake ni vijisafari vya hapa na pale kwa ajili ya kubadilisha mazingira ya kinyumbani uliyoyazoea na kwenda kufanya recreation of mind sehemu nyingine ya mbali kidogo.
sasa basi hizi vacation zinahusika vipi na kujenga mahusiano wa kimapenzi na huyo umpendae?
kwa upande wangu mimi nina imani kabisa mara mnapokuwa sehemu ileile kila siku bila ya kubadilisha mazingira ni rahisi sana kuchokana, simaanishi kuchukiana hapana! ila mnazoeana kupita kiasi hadi mnaona ni hali ya kawaida tu na mwisho wa siku mtaonekana kama ni marafiki tu wa karibu na si wapenzi, kwa sababu mapenzi yana nakshi yake jamaani, mpenzio sharti umpetipeti ili ajihisi nae anapendwa au sio jamani?mnnh!
hizi vacation si lazima mchukue vacation za kwenda visiwa vya comoro ndio muonekane mnafanya veekeeesheenii! hapana jamani zinategemea na kipato chenu nyie wenyewe wawili, mnaweza hata mkatoka mjini mkaenda kulala mbezi beach kwa siku mbili sio mbaya, au hata kigamboni basi au maeneo mengine ambayo unaweza kuaford, ukifanya hivyo hata mara mbili au mara moja kwa mwezi c mbaya sana jamani, lakini kama mfuko unaruhusu, basi usifanye hiana, mchukue mpenzio mpeleke hata miami akale raha za dunia, mara moja kwa mwaka c mbaya wandugu!
mapenzi hayajengwi kwa ndumba wala ubabe ndani ya ndoa, ni hivi vijimambo vidogo vidogo na vijisapraiz ndio hudumisha mapenzi,. tudumishe mapenzi yetu jamani tufanye mapinduzi ya wale wanaosema wabongo hatujui mapenzi, tunayajua saana basi tu hatujaamua.. anhaa haa ha!
asanteni jamani, msiache kutembelea blog hii usije kupitwa na raha za ulimwengu wa wapendanao.
0 Response to "VACATION NA MAPENZI"
Post a Comment