Soma hii! Mchagua nazi……
Hakuna mtu aliye mkamilifu kwa asilimia 100. (mfano)
Duka la kuuza waume (husbunds) limefunguliwa, ambapo mwanamke anaweza kwenda na kuchagua mume anayemtaka.
Moja ya maelekezo yaliyopo getini, ni maelezo kuhusu ni jinsi gani duka hilo linaendeshwa. Na masharti makubwa ni kwamba unaruhusiwa kutembelea hilo duka MARA MOJA TU!
Kuna ghorofa (floors) sita ambamo waume wapo, na kila unavozidi kupanda ghorofa ya juu sifa za mwanaume zinaongezeka. Unaruhusiwa kuchagua mume kutoka ghorofa yoyote ile iwe ya chini au juu.
Lakini unavyopanda juu zaidi kuchagua mume kwenye ghorofa za juu basi kamwe huruhusiwi kurudi tena kuchagua mume katika ghorofa za chini ambazo tayari umeshazipitia.
Mwanamke mmoja aliamua kwenda kutafuta mume na alivyofika tu dukani katika ghorofa ya kwanza, alikuta bango limeandikwa hivi:
GHOROFA YA 1 - Wanaume hawa wana kazi nzuri, na wanayo hofu ya Mungu. Akapanda juu zaidi
GHOROFA YA 2 - Wanaume hawa wanakazi nzuri, wanahofu ya Mungu na wanapenda watoto. Akaendelea juu tena
GHOROFA YA 3 - Wanaume hawa wana kazi nzuri, wanayo hofu ya Mungu, wanapenda watoto, na wanamuonekano mzuri.
"Wacha wee," akavutiwa kupanda juu zaidi ghorofa ya nne na kukuta bango limeandikwa:
GHOROFA YA NNE - Wanaume hawa wana kazi nzuri, wanahofu ya Mungu, wanapenda watoto, wanamuonekano mzuri na wanasaidia wake zao kazi za nyumbani.
"oh oh nimchague huyu huyu" alisikika akisema lakini bado akaona ajaribu kwenda ghorofa ya tano na akakuta bango linasomeka hivi:
GHOROFA YA 5 - Wanaume hawa wana kazi nzuri, wana hofu ya Mungu, wanapenda watoto, wana muonekano mzuri, wanasaidia kazi za nyumbani na wako romantic sana.
Yule mwanamke akavutiwa kubaki ghorofa ya tano amchukue mume, lakini ajabu akavutiwa kupanda juu zaidi ghorofa ya sita, huko akakuta bango lomeandikwa hivi:
GHOROFA YA SITA - Wewe ni mgeni wetu namba 4,457,238 katika ghorofa hii ya sita. Ghorofa hii ni kwa ajili ya wanawake ambao wameweka viwango vikali kwa wanaume wanaowataka, ambao kimsingi ni vigumu mno kuwapata hapa dukani kwetu na kwingineko.
Asante sana kwa kutembelea dukani kwetu, angalia ngazi vizuri, usije ukaanguka unaposhuka kuondoka dukani kwetu na uwe na siku njema.
Mwanamke aliondoka mikono mitupu pasina kupata mume.
Ndugu zangu huu ni mfano tu kwa jinsi gani Wanawake wengi wanavyoweka vigezo na masharti magumu kwa wanaume wanaowahitaji kwa ajili ya kujenga maisha pamoja.
Hakuna mume au mke aliye mkamilifu kwa asilimia 100 popote pale duniani. Wengi wetu tumeweka viwango vikali sana kwa aina ya mke au mume tunaowahitahi.
Tumejisahau kuwa na sisi vile vile tunayo madhaifu fulani na Kwa bahati mbaya watu kama hao ni vigumu mno kupatikana na kimsingi hawapo.
Tumeumbwa kuchukuliana madhaifu yetu. Sisemi kwamba mtu yeyote anayekuja mbele yako umuoe au uolewe nae, hapana!
Najaribu kuelezea kuwa kuna tofauti nyingine zafaa kuchukuliwa kama ni challenge tu na zinaweza kuzoeleka au kurekebishika huko mbeleni.
Wanandoa au waliopo kwenye mahusiano, ambao wamechagua kuzisheherekea tofauti zao, na sio tofauti zao ziwafarakanishe, mahusiano yao hukua na kudumu kila uchweo.
Mchagua nazi huangukia koroma, na siku zote kumbuka muda haukusubiri wewe.
0 Response to "Soma hii! Mchagua nazi……"
Post a Comment