Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’,
‘Magnesium’ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina
virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex
libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile
Dysfunction).
Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta
mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za
kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya
damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari
yoyote mbaya.
Tikitimaji lina kirutubisho aina ya ‘arginine’, ambacho huchochea
uzalishaji wa ‘nitric oxide’ kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza
nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.
Kazi nyingine zinazofanywa na tikiti maji katika mwili wa mwanadamu;
Huimarisha mishipa ya damu.
Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile
Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo.
Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali,
huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
Husaidia kupunguza uzito wa mwili.
Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji.
Huimarisha kinga za mwili.
Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji mbali ya baadhi
ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa
uimarishaji wa kinga ya mwili.
Huondoa sumu mwilini.
Kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo
la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya
magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti,
kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.
0 Response to "Nguvu iliyopo kwenye tikiti maji katika kutibu tatizo la nguvu za kiume"
Post a Comment