MWANAMKE, NINI CHAKUFANYA BAADA YA KUJIFUNGUA! - Bongo Loves

MWANAMKE, NINI CHAKUFANYA BAADA YA KUJIFUNGUA!

Image result for love on bed
Kuna namna nyingi ningeweza kuiandika hii makala kutokana na kichwa hiki cha habari. Ningeweza kuzungumzia kuhusu mazoezi na chakula ili kubadilisha muonekano wako na labda kurudi kama mwanzo, kipindi bado hujabeba ujauzito. Najua hiki ni kitu ambacho wanawake wengi kinawaumiza vichwa, lakini kwangu pamoja na umuhimu wa mazoezi, umuhimu wa kufunga mkanda, umuhimu a kutaka kupungua.

Pamoja na umuhimu wa kujaribu kuondoa michirizi lakini kitu cha muhimu zaidi ni namna wewe Mama uliyetoka kujifungua unavyowaza. Hilo ndiyo la muhimu kwangu kwani namna unavyojisikia leo sio kwakua unaonekana hivyo ulivyo bali nikwakua unawaza hivyo. Nianze kwa kusema kuwa kujifungua na kuwa Mama si ugonjwa bali ni baraka, hivyo kama mwanamke unapaswa kufurahia mabadiliko ambayo yanatokana na baraka hizi hata kama hayatawapendeza watu wengine.

(1) Kila Kitu Kipo Kichwani Kwako Zaidi; Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa una matatizo ya kimuonekano lakini ukweli nikuwa hayo mambo yapo kichwnai kwako. Wewe ni Mama ndiyo umetoka kujifungua hivyo kila mtu anatagemea kuwa nilazima utaongezeka, ni hali ya kawaida na zaidi ya wewe hakuna hata mtu anayekushangaa.

Hapa nikimaanisha kuwa, hakuna mtu anajali wewe kunenepa, mume wako hajali hiyo michirizi, anajua kuna mtoto, anajua ni mabadiliko hivyo hajali. Yaani ni sawa na mtu ashangae mwanaume mtu mzima kuota ndevu, hawashangai na hawajali kwani ni kitu cha kawaida.

(2) Mume Wako Hajali; Unaweza kuamini lakini asilimia 90 ya wanaume hawajali mabadiliko ambayo hutokea katika miili ya wake zao baada ya kujifungua. Wengine hata hawajui kama kuna mabadiliko, sanasana atasema mimba imekunenepesha lakini huanza kugundua pale unapowambia. Unapoanza kulalamika nimekua mnene, kulalamika diety haifanyi kazi, kuanzakuchagua nguo za kuvaa, kuanza kuchagua sehemuza kwenda hapo ndipo huanza kuwaza hivi kumbe kweli mke wangu kabadilika.

Wanaume wengi hawapo makini na hayo mambo ila kwakua kila siku wewe unalalamika nimekua mnene, unalalamika nimekua mbaya, unalalamikia nguo hazikutoshi basi ni kama unamstua na kumuambia “Niangalie mume wangu kwamakini uone ubaya wangu!” Lakini nikuhakikishie mumeo alitegemea utanenepa hivyo akili yake hata haijui kama ukijipenda na kuacha hayo malalamiko labda kama mumeo alikua kichomi kabla hatajua kilichobadilika.

(3) Vaa Nguo Zinazokufanya Uwe Huru, Unazozifurahia Wewe; Inawezekana kuna msukumo na presha kubwa ya kutaka kupendeza, unataka miezi kadhaa uanze kufiti katika nguo zako za zamani. Unataka kutoka na unataka kwenda na wakati hivyo unajiangalia hakuna nguo inakutosha. Hembu nunu au vaa nguo ambazo zitakuweka huru na zinakupendeza wewe zaidi na si zile ambazo unadhani watu watazipenda.

Unapovaa nguo, ikakufanya uwe huru, utulie basi nirahisi watu wengine kukuona una mvuto. Lakini ukijilazimishia katika nguo, viatu na vitu vingine, hutakua huru na hata huyo mumeo naye atakuona hauko huru na utamboa. Tuchukulie hujapungua lakini ushaanza kuvaa nguo za kubana, hutaki sijui Braa za aina gani, unakaa kaa tu ili kuonekana unavutia, hapo watu watakushangaa na mumeo ndiyo atashtuka mbona huyu kabadilika, ila kama umevaa nguo imekukaa uko huru wala hakuna wakuona mabadiliko.

(4) Muangalie Mwanao; Najua wakati mwingine ni vigumu kuacha kusahau kuhusu tumbo, kuhusu miachirizi na mabadiliko ya mwili wako, unajiangalia na kujichukia, unachukia muonekano wako na ukiangalia picha zako za zamani au kuona marafiki zako ambao mlikua saizi sawa basi unachanganyikiwa zaidi. Lakini kila unapokua na mawazo ya namna hiyo, hembu kabla ya kuanza kulia na kujilaumu.

Hembu kabla ya kuanza kumlaumu Mungu kwanini hataki kukufanya uwe kama zamani muangalie mwanao. Jinsi alivyolala hapo vizuri, jinsi anavyokuangalia na vimacho vyake, namna ambavyo anakuhitaji na anavyocheka bila hata sababu. Halafu shika tumbo lako, angalia michirizi na kujiuliza hivi ukiambiwa uchague kati yake na hayo mabadiliko ungechaga nini!

Ndiyo najua haitabdilisha muonekano lakini iyabadilisha namna unavyojiona na kuona kuwa kumbe ulichokifanya ni cha thamani kubwa zaidi ya mabadiliko uliyoyapata, utajikuta unajipenda zadi. Hata kama mumeo ni kichomi ni wale wa kukuambia maneno ya kashfa na kukuambia umekua mbaya, wewe bado muangalie mwanao na jiulize kipi bora zaidi, kama akizidi kukusimanga tabasamu na jisemee kichwani “Hata kama ingekua ni michirizi ya uso bado ningemchagua mwanangu!”

(5) Fanya Mazozi Kwaajili Yako; Mazoezi ni muhimu, si kwasababu wewe ni mbaya hapana ni kwasababu tu za kiafya, unapojifungua kuna wakati ukifika na unapokua tayari basi fanya mazoezi, najua unaweza kujiuliza kwanini mazoezi tena baada ya maelezo yote hapo juu? Hii ni kwasababu mazoezi hufanya kazi pale tu akili yako nayo inapokua huru kama una mawazo, stress na unafanya kwa uoga wa kuachwa basi ni ngumu kupungua!

Ndiyo afya ya mwili huendana na afya ya akili, kuna watu hawali, wanafanya mazoezi lakini hawapungui kwakua tu wana mawazo mengi na hufanya mazoezi kwakua wanajiona wabaya na si kwakua wanataka kuwa na afya bora. Nataka uondoe hizo stress kwanza na ukifanya mazoezi fanya kwasababu ya afya na si kwakua unadhani umbaya, unadhani mume atakuacha au kwakua nguo hazikutoshi, fanya kwa raha zako wewe ni Mama umefanya kitu pekee ambacho mwanaume hawezi kukifanya asikutie mawazo bure kama rahisi si angefanya yeye!

0 Response to " MWANAMKE, NINI CHAKUFANYA BAADA YA KUJIFUNGUA!"

Post a Comment