MUME WANGU, SIWEZI KUSHINDANA NA MABINTI WADOGO WA MJINI - Bongo Loves

MUME WANGU, SIWEZI KUSHINDANA NA MABINTI WADOGO WA MJINI





Alikuwa akisoma article fulani kwenye mtandao huku amekaa kwenye kiti kilichopo chumbani mwao..

"Darling...." Akamuita mumewe..

"Yes.." Mume akaitika...

"Unanipenda?" Akamuuliza mumewe ambae alikua busy akifunga tai tayari kwa kuivaa shingoni.

"Of course nakupenda my love. Nakupenda sana tu." Mume akamjibu.

Mke akamtazama na kumwambia.."Kuna makala naisoma hapa inasema kwamba asilimia 52 ya wanaume wanasaliti ndoa zao na mabinti. Hasa kama wake zao wameshazaa. Huu ni unyama huu".

"Kwa hiyo....?" Mume akauliza.

"Kwahiyo me naogopa sana. Naogopa labda umeanza au ukaanza kufanya mapenzi na hao mabinti wabichi. Mimi nimezaa sipo kama nilivyokua binti mbichi. Angalia maziwa yangu yamelala, tumbo linakovu la operation. Me siwezi kushindana na hao mabinti wa mjini naogopa watakuteka kabisa na ukaisahau familia yako.." Mke akaongea huku akionesha wasiwasi.

Mume akaacha kufunga tai na akamtazama mkewe usoni. Akatabasamu. Then akaanza kuongea

"Naanza na namba Moja, hua nashangaa hizi takwimu zinatoka wapi. Asilimia 52? Sijawahi kuwaza hilo. Hiyo asilimia 52 isikubabaishe mpenzi wangu ..cha msingi ni kuamini maneno yangu".

Akaanza kumfuata mkewe alipo.

"Namba mbili, mimi sio mnyama. Mimi ni mume wako. Uliolewa na mimi sio kwa sababu mimi ni mnyama lakini ni kwa sababu uliniona ni KING na nastahili himaya yako. Sijaumbiwa roho ya unyama bali ni kwa nguvu ya roho mtakatifu. Ninaishi kwa principles.."

Akasogea zaidi kwa mkewe na kumbusu kwenye paji la uso..kisha akaendelea...

"Namba Tatu, ni kweli kabisa hauwezi kushindana na mabinti wa mjini; Usijaribu wala usithubutu kushindana nao maana hawapo kwenye ligi yako na hawataifikia. Hawawezi hata kujifananisha na wewe, hawawezi kuvaa viatu vyako, busara na hazina ya maarifa yako hawawezi kufikia. Haujaishi maisha yako basi, bali umeishi maisha yako na mimi. Hawana kumbukumbu na expirience ambazo mimi na wewe tumezipitia kwa pamoja. Hawataweza kuni-handle tabia zangu kama wewe unavyoni-handle. Sanasana watataka pesa zangu na watakuwa tayari kufanya lolote kwa minajili ya kunila pesa zangu..kimsingi hawana hata thamani ya kujifananisha na wewe malikia wangu.

Akachukua simu kutoka mkononi mwa mkewe na kuiweka kwenye meza...

"Kuhusu maziwa yako. Kila siku ya Mungu inapokwenda maziwa yako yanakua mazuri. Maziwa ni maziwa lakini yako ni mali ya mwanamke naempenda" Mume akaongea huku akiyashika taratibu taratibu. Mke akatetemeka kwa mshtuko

"Maziwa haya umenyonyesha wanangu kwa upendo wa mama usio na kifani....kwanini nisiyapende?

"Tumbo lako, unasema lina kovu, me naliona liko sexy...limekua nyumba ya wanangu. Uliwabeba kwa upendo mkubwa..nilifurahi kuligusa pale ulipokua mjamzito..hata hivi sasa nafurahi kulishika.

Kovu la operation. Hili linanikumbusha madhila uliyopitia, hii inanifanya nikupende zaidi.."

"Miguu yako..imetembea na mimi kwa kila hatua hata pale tulipokua hatuna usafiri tulitembea kwa miguu pamoja. Uliniamimi pale nilipokua sina kitu, miguu yako ikasimama na mimi na ukanitia moyo. Mpaka kufikia hatua hii tukiwa na mali za kutosha ni mchango wako mkubwa sana...

"My love, wewe bado ni namba moja. Hakuna mwanamke alie mkubwa kuliko wewe au mdogo kuliko wewe ambae yupo kama wewe na atakaeifikia ligi yako. Hawana viwango vya kukufikia. Mimi ni mfalme kwa malikia mmoja tu. Malikia huyo ni wewe"

Mke akavua night dress yake..akamkumbatia mmewe na kumbusu kwa hisia kali, alimhitaji mumewe..alimhitaji ampe raha kusindikizia maneno mazuri aliyoyasikia kutoka kwenye kinywa cha mumewe mpenzi.

Mume hakufanya makosa..akajisogeza na kuangukia kitandani and they made passionate love ile asubuhi.. the kind of love that foreigners cannot intrude.

Aliye mfalme huilinda himaya yake isiingiliwe na wevi...

Mwenyezi Mungu aiponye ndoa yako na kuiimarisha kwa pale penye kila dalili ya kuleta mtafuruku #AMEN

0 Response to "MUME WANGU, SIWEZI KUSHINDANA NA MABINTI WADOGO WA MJINI"

Post a Comment