Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1
WANAUME
wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza
kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa
hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya
mahitaji ya mwanamke, lakini si
sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha.
Fikra
hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika
mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao
wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke
mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
Upweke,
kwa hakika, huzaa migogoro isiyokwisha inayowafanya wanaume [ambao
kimsingi ndio wasababishi wa upweke huo] washindwe kuwaelewa wanawake.
Kwa mtazamo wao, ni vigumu kumridhisha mwanamke.
Wengine wanaenda mbali na kufikiri , 'mwanamke ni kiumbe mgumu
kueleweka' kwa
sababu, ‘hata ufanye nini...hata umpe nini hawezi kuridhika’.
Lakini
wanachosahau wanaume wenye mawazo haya ni kuwa mwanamke kwa asili yake
anayo mahitaji ya msingi ambayo yanapopuuzwa,
chochote kinachofanyika kama mbadala wa mahitaji hayo hakiwezi kuwa na
maana yoyote. Usipoweza kujua mahitaji yake halisi, unaweza kumpa
chochote kile unachodhani anakihitaji na bado mambo yasiende kama
unavyotamani iwe.
Kusema hivyo, haimaanishi sielewi kuwa wapo wanawake wengi wanaopenda kujipatia fedha kwa wanaume. Hawa ni wanawake wanaofanya biashara ya mahusiano. Kwao, hakuna sababu yoyote ya kuwa na uhusiano imara na wenzi wao isipokuwa mpangilio wa kujipatia vitu na fedha.

Hatuzungumzii
uhusiano huo wa kibiashara kati ya mwanamume na mwanamke bali uhusiano wa dhati
unaojengwa katika misingi ya upendo, uaminifu, kuelewana na ahadi ya kuwa
pamoja katika dhiki na raha.
Hebu
na tutazame mahitaji makubwa ya kihisia aliyonayo mwanamke mwenye upendo wa dhati
kwa mwenzi wake.
Kupendwa kwa vitendo
Tulishaona kuwa hadhi ya mwanaume inategemea kwa kiasi kikubwa namna anavyoheshimiwa. Kwa mwanamke hali ni tofauti. Hadhi yake inategemea namna anavyopendwa na mwenzi wake.
Upendo kwa mwanamke unaeleweka anapoambiwa bila kuchoka na kuthibitishiwa kwa kutendewa vitendo kuwa anapendwa. Katika lugha ya kiingereza, hapa tungetumia neno affection, yaani matendo yanayoonesha mapenzi kwake.

Hata hivyo, lugha
ya mapenzi hutegemea mambo mengi. Kuna athari za utamaduni, desturi na imani zilizopo
katika jamii aliyokulia mwanamke. Hata hivyo, yapo matendo yaliyothibitika
kuvuka mipaka ya kiutamaduni.
Mfano,
kumwambia mwanamke unampenda mara nyingi iwezekanavyo, ni hitaji la
msingi. Kwa
mwanamume, kuambiwa anapendwa inaweza isiwe jambo la maana, lakini si
kwa mwanamke. Mwanamke anatamani kusikia mara nyingi kadri
inavyowezekana kuwa anapendwa.
Pia kuna vitu kama kupewa zawadi asizotarajia, kutumia muda wa mapumziko pamoja nae, kutoka naye kwenda mbali na nyumbani na mambo kama hayo yanayoonesha kuwa kweli unampenda.

Ndio
kusema, ikiwa unataka kuugusa moyo wa mwanamke, akupe heshima
unayoihitaji kama
mwanaume, unawajibika kujua vitu gani mahususi ukimfanyia vinatuma
ujumbe wa
wazi kuwa unampenda. Usipoweza kumfanya mwanamke ajisikie kupendwa,
anapoteza hamu ya uhusiano. Huchoka kihisia na anaweza kufanya mambo
yasiyotarajiwa ili tu kuhujumu mahusiano.
Anataka kuwa kipaumbele chako
Mwanamke hapendi kujikuta katika mazingira ya kushindania nafasi ya kwanza na kitu kingine chochote iwe ni kazi, mtu au chochote kile unachokipenda wewe mwanamume.
Tulishaona kuwa kwa mwanaume, hadhi yake hutegemea zaidi namna uwezo wake unavyotambuliwa. Hali hiyo humfanya mwanamume atumie muda mwingi kufanya mambo yanaweza kumpa heshima katika jamii. Inaweza kuwa kazi, biashara, mamlaka na namna zozote zile zinazomwongezea uwezo.
Lakini wakati anapotumia muda mwingi katika mambo hayo, ni rahisi kuonekana ameyafanya mambo mengine kuwa ya muhimu kuliko uhusiano wake na mwenzi wake. Wanawake wengi hawapendi kujikuta katika hali hii. Hapa ndiko iliko tofauti.
Mwanamke hatamani kuwa kwenye nafasi ya ‘mengineyo’, ‘ziada’, ‘baadae’ ‘nikipata muda’. Unapomweka 'akiba' mwanamke hawezi kufurahia kwa sababu anatamani awe kipaumbele chako.
Mambo mengi huthibitisha kuwa umempa nafasi ya kwanza. Mfano kuwa na muda wa kuwa naye mara nyingi kadri inavyowezekana, kuahirisha mambo mengine ya muhimu kwa ajili yake, kuwahi miadi unapoahidi kukutana nae, kuwasiliana naye kwa karibu na mambo kama hayo. Unaposhindwa kufanya hivyo, mwanamke hupata ujumbe kuwa yeye ni mtu wa ziada baada ya mambo ya muhimu.

Kadhalika, ili kumwambia yeye ni kipaumbele, mwanamke anatamani kila unapoongea nae akili yako yote iko
pamoja naye. Kuwa pamoja naye maana yake ni kuachana na vyote vinavyokuondolea uzingativu na kumsikiliza kwa makini.
Mwanamke anatamani unapozungumza naye ufuatilie anachokisema, umpe mrejesho kuwa unamwelewa na uonesha kuwa mwili, akili, hisia ziko pamoja naye kumsikiliza. Vinginevyo, mwanamke anakuoana kama hujaweza kumpa nafasi yake anayoistahili.

0 Response to " Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1"
Post a Comment