Mama Sele, washa!
Leo asubuhi wakati nikiwa kwenye gari naelekea kazini huku nikisikiliza redio Clouds FM nilisikia tangazo la kipindi maarufu cha Leo Tena. Si tangazo jipya, binafsi nimelisikia mara nyingi sana.
Lakini leo nililielewa tofauti.
Nitarejea tangazo hilo kwa nukuu ambazo si rasmi bila kupotosha maana/ujumbe. Nafanya hivi kwa sababu, mosi, sikumbuki neno hadi neno kwenye tangazo husika (lakini nakumbuka ujumbe), pili, nina jambo nataka kulieleza.
Ningeweza kusubiri hadi tangazo hilo lirushwe tena ili ninukuu kiufasaha lakini nina dukuduku ambalo siwezi kusubiri kulisema. Hivyo mniwie radhi pale ambapo sijanukuu kwa ufasaha.
Kwenye tangazo hili inasikika sauti ya mwanaume mwenye lafudhi ya Kichaga. Anaitwa Baba Sele.
Baba Sele anamtaka mkewe, Mama Sele, awashe redio ili asikilize kipindi cha Leo Tena. “Mama Sele, washa!” anasikika mwanaume huyo kwa takribani mara tatu, akirudia rudia wito wake huo.
Wakati wote huo Mama Sele anaonekana kutoelewa mumewe anataka nini. “Niwashe nini?” anahoji. Kisha analalamika, “Niwashe nini jamani? Si unaona nafua nguo, na kule mtoto analia? Au kwa sababu bado sijapika chakula?”
Baba Sele yeye hana habari, anaendelea tu, “Mama Sele, washa!” Mwisho, Mama Sele anagundua mumewe anamtaka awashe redio ili tu asikilize kipindi cha Leo Tena! Mama Sele anawasha redio na mumewe anafurahi!
Tangazo hili linaweza kuonekana ni la kawaida tu. Na wengi hubaki kucheka lafudhi ya Kichaga ya Baba Sele – na inawezekana kabisa aliyetengeneza tangazo alilenga hilo tu. Hata Baba Sele haongei kwa ukali kwa maana ya kuamrisha.
Lakini kuna kitu cha ziada, na kinahusu taswira inayojengwa na tangazo husika. Ni taswira ya mfumo-dume.
0 Response to "Mama Sele, washa! "
Post a Comment