Kila mwanaume anapenda kujua jinsi ya kumchangamsha mwanamke ili
ampende. Lakini wengi hushindwa njiani pale wanapojaribu kufanya hivyo
kwa sababu hawajui vitu vitano vya kumchangamsha mwanamke.
Yafahamu hayo mambo matano, na namna kuyatumia.
Nadhani utakuwa ushashuhudia baadhi ya wanaume wakichati na
wanawake(zao),wakati mwingi unakuta mwanamke anacheka na kumsifia kuwa
anamfurahisha(“hahahaha!…. unanifurahisha”).
Kuambiwa na msichana kuwa unamfurahisha ni mojawapo ya kitu kikubwa sana
ambacho wanaume wengi hawakisikii kutoka kwa mwanamke. Haihusiani na
muonekano wako, ila namna unavyopangilia hoja zako na mada zako kwake na
jinsi unavyoziwasilisha kwa kuangalia mazingira.
Jinsi ya kumfurahisha na kumchangamsha mwanamke
Ni kitu gani hasa kinamfurahisha mwanamke? Hauwezi kumfurahisha mwanamke
kwa kumkejeli au kumshika baadhi ya maeneo ya mwili wake(utaishia
kumchukiza na kujiondolea point).
Utajua unamfurahisha mwanamke pale tu unapomfanya ajisikie furaha, na wakati mwingine hushindwa kujizuia na hujikuta anakukiss!.
Ntakupa mambo matano ya kufanya ambayo yakuufurahisha moyo wa msichana unayemtaka(kumpenda).
Unaweza kubadilisha muonekano wako kimavazi, wakati mwingine unaweza kumkazia macho lakini hiyo haitamfurahisha bali itamtisha.
Kumchangamsha/kumfurahisha mwanamke kunahitaji kutengeneza mvuto(impression) zaidi ya muonekano na swaga.
Kama unataka kujua jinsi ya kumfurahisha mwanamke , mwanzo wa yote, huanza na maongezi. Na mwisho wa yote ni hapo pia.
Mawasiliano mazuri kimaongezi ndiyo njia pekee ya kumfurahisha na kumchangamsha msichana.
Yatumie haya mambo matano, na utafanikiwa hata kabla ya kufikia mwihso:
1. Mshawishi kupitia kitu anachokipenda
Unaweza kudahani hii haina umuhimu. Wanaume wengi hufikiri hivyo na
hushangaa kwanini tu niongee kuhusu kitu ambacho msichana anakipenda.
Kwanini wasichana nao wasiongee kuhusu vitu wanavyovipenda wanaume?
Wanawake huweza kufanya hivyo, japo hatujui. Wanawake wengi hujitahidi
sana kujua wavulana hupenda kuongelea nini. Lakini, wakati unataka
kumvutia msichana, ni muhimu ukajua ni kitu gani kinachoendelea kwenye
mawazo yake. Sasa tambua kwamba, kujua kitu msichana anachokipenda
haimaanishi, dhahabu, mitindo au vipodozi. Tofauti kati ya msichana na
mvulana kwa namna ya kuishi imepungua sana kwa sasa(wanawake hufanya
vingi ambavyo wanaume hufanya). Kwa maana hiyo ni rahisi kuwa na
maongezi yenye kuvutia bila kuboa. Achana na mambo ya mahesabu, michezo,
teknolojia, amini yatakua poa tu maongezi yenu.
2. Mtanie
Unapoongea na msichana, ni rahisi sana kumfanya na yeye aongee na wewe
hatakama hakupenda mwanzo. Lakini hiyo haitoshi. Kama unataka kujua ni
jisi gani ya kuongea na msichana/mwanamke, utapaswa kumfanya yeye
ajisikie huru na mwenye kujiamini(confortable), lakini pia mfanye ajue
kuwa unampenda hatakama haujamwambia.
Kumbuka, kama utaongea nae kama rafiki, lazima awaze na ajue kuwa wewe
ni mwanaume noma sana(great guy), lakini hatahisi kwamba wewe ni
mwanaume unaeweza kumchangamsha au kumfurahisha. Ili kuonekana kama
mwanaume anayefurahisha kwa mwanamke yeyote, inatakiwa akuone kama mtu
muhimu wa kukutana nae, na ili kufanya hivyo, msukume sukume hata bega
katikati ya maongezi. Lakini usizidishe sana utaishia kumboa, fanya
hivyo pale tu anapoongea jambo linalochekesha au lenye utani ndani yake.
Ila usiende na kumwambia maneno ya kawaida kama “unamuonekano mzuri”,
“wewe ni mzuri sana”, au maneno yenye kufanana na hayo. Inawakera sana
na haioneshi utofauti na watu wengine wa mtaani. Badala yake, jaribu
kuwa specific wakati unamuambia jambo fulani mnapokutana. Mwambie maneno
kama “umependeza sana leo. Huo ni mtindo mpya wa nywele?”, Hayo ni
maneno mazuri sana kwa mwanamke kwa sababu ni wanaume wachache sana
huyatumia kwao. Kwa hiyo unavyosema “leo umekua mrembo zaidi” inamfanya
ajue ni jinsi gani unamaanisha mpaka umevunja ukimya.
Kwa kumtania huko – unaweza kufanya mambo matatu. Unaweza kumshtua na
kumfanya atabasamu. Unaweza kumfanya ajue kwamba wewe unamuona mtu wa
tofauti sana. Au tatu, unaweza kumfanya atambue kwamba umemwona wa
kuvutia sana. Kumbuka hayo yote unamfanya yeye aone ni mtu mzuri ambaye
anaweza kudate na wewe.
3. Kuwa mcheshi(be funny).
Baada ya kumfanya atabasamu na kuyafurahia maongezi yako na yeye, ni
muda wa kumuingia ndani zaidi kidogo. Kila mmoja wetu anamambo yake ya
siri ambayo hatupendi watu wote wajue labda mtu ambaye tunamwamini sana.
Ili kumfanya ajiamini kwako, unatakiwa kumfanya awe na good time sana
na wewe. Sasa hatuwezi kukuambia kabisa jinsi ya kumfanya mwanamke
acheke. Lakini tunaweza kukupa mambo mawili ya kutumia. Usimwambie utani
wowote wakati unaongea nae. Kuwa mwenye furaha muda wote unaoongea nae.
Hii inaweza kukutatiza kidogo. Kwanza kuongea utani wa moja kwa moja
kama mtu aliyekariri ni ujinga. Badala yake, ongea nae maongezi
yatakayomfanya aone unamtania, na hapo naye ataanza utani.
Jitahidi kuonesha unafurahia maongezi wakati unaongea nae kama unataka
kumchangamsha. Ukiwa na furaha, dunia nzima inatabasamu pamoja nawe!.
Kama unatabasamu na kujisikia furaha, naye atatabasamu pia na kuwa na
furaha. Lakini kama unauoga, utamfanya naye awe
mwoga(unconfortable).
4. Unaweza kumsukuma kidogo kati kati ya maongezi
Najua unaelewa ninaposema kusukumana, hii utokea mara nyingi pale
mvulana na msichana wanapukua wamezoeana, kwa hiyo kuifanya na mwanamke
kwa mara ya kwanza inatakiwa uwe mwangalifu na makini ili usije
kuharibu. Unapofanikiwa kufanya hivyo, jitahidi isiwe kila saa maana
utamkera kama nilivyosema hapo awali.
Ili uweze kufanya hivyo inatakiwa uwe wa kawaida – chukulia kama ni mtu
wa kawaida japo wewe unajua ni special. Muulize alifanya nini weekend au
baada ya kutoka kazini, muulize anapenda kwenda wapi akitoka out au ni
mgahawa gani anaupenda au anatamani kwenda au kitu kingine chochote
ambacho ni binafsi(very personal). Lazima atajua wewe unamtania mana
hakuna mtu ambaye anaweza kuulizwa maswali yote hayo na hajazoea
kuulizwa, hivyo lazima afunguke.
Na bila kusitaa, usisahau kuuliza hili swali.
“Hey, samahani hii ni very personal – hivi una boyfriend? Kama unaye
basi jua moyo wangu utavunjika vipisivipisi zaidi ya millioni hamsini
sasa hivi!”, umeona ilivyo ya kichokozi eeh?. Lakini hii hufanya
maajabu!.
Lazima acheke, lakini hiyo sentensi itaweka lengo lako kwake moja kwa
moja, na lazima atajua kuwa unamtaka–hahahah!. Lakini angalia usiharibu
kwa kuwa kituko baada ya kukupa jibu – maana unaweza kuta anaye, na kama
atakwambia anaye tabasamu. Na ongelea mada nyingine tofauti kama vile
swali lililopita halikumaanisha kitu kwako. Lengo lake lazima atakuwa
ashalijua, na pia utafanikiwa kumfanya awe confortable kwako.
5. Mshike.
Huu ni uwanja hatari sana, lakini ni kitu unachopaswa kujifunza kwa
sababu unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, si ndiyo? Hivyo
kumshika katika muda muafaka inakamilisha point ya 5 ya mambo ambayo
unapaswa kuyajua wakati unataka kumfurahisha mwanamke. Kama utafanikiwa
kulifanya hili kwa usahihi, utakua umejichukulia point kubwa sana.
Sasa kumshika msichana ni kama kucheza na moto. Ukiushika fasta hauwezi
kusikia joto, lakini ukiushika muda mrefu utaungua! Unaona ilivyo
hatari?
Unaweza kumshika bega au mikono kama tayari ushamfurahisha vya kutosha.
Lakini kumbuka hili, mshike tu pale unapokua na sababu ya kumshika,
mfano mshike masikio kama unayasifia masikio yake au nywele kama
unazisifia nywele zake, au mfute koti lake kama kuna kauchafu hatakama
hana hako kauchafu, au mshike begani kama unatembea nae barabarani/
mtaani. Kumbuka kumshika mtu ni very personal, hivyo inabidi uwe makini
sana na uangalie anamuitikio gani wakati unamshika kabla haujamshika
tena.
Kama unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, yatumie haya mambo
matano wakati utakapokutana na mwanamke next time. Na baada ya hapo
utaona ni jinsi gani unavyoweza kumfurahisha mwanamke na kumfanya
ayapende maongezi yako kwa mara ya kwanza!.
Share this post
0 Response to "Jinsi ya Kumchangamsha na Kumfurahisha Mwanamke "
0 Response to "Jinsi ya Kumchangamsha na Kumfurahisha Mwanamke "
Post a Comment