Hivi Ndivyo Mwanamke Anavyoweza Kufanya Mpenzi Wake Atembee Na Mashosti Zake. - Bongo Loves

Hivi Ndivyo Mwanamke Anavyoweza Kufanya Mpenzi Wake Atembee Na Mashosti Zake.

Hivi Ndivyo Mwanamke Anavyoweza Kufanya Mpenzi Wake Atembee Na Mashosti Zake.



Maisha ya kimapenzi yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kwani kuna changamoto nyingi zinazoweza kujitokeza kiasi kwamba usipoangalia unaweza kuishia kusema hutakuja kumpenda mtu, heri uishi peke yako!

Tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida ni usaliti. Lakini naomba leo niseme kwamba, wapo watu wanajitakia kusalitiwa na hapa nawazungumzia wanawake.

Kuna wanawake ambao wana wapenzi au wako kwenye ndoa lakini wanafanya mambo ambayo yanawafanya wasalitiwe kirahisi.

Unamkuta mke anachekelea mumewe kuwa na ukaribu na shosti wake, anajipenda kweli huyu? Hili ni tatizo na ndiyo maana leo nimeona nizungumzie mambo manne ambayo ukiyafanya lazima mumeo ‘atoke’ na marafiki zako.

Moja; ukaribu wa mume na marafiki wa mke. Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kuwaweka waume zao karibu sana na marafiki zao. Unakuta mwanamke eti anamruhusu mumewe kwenda klabu au baa na shosti wake. Katika mazingira hayo unatarajia nini?

Sisemi uanze kumfikiria tofauti rafiki yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, sasa hivi kuna wasichana micharuko ambao ukiwapa nafasi kidogo tu kwa mumeo wamemchukua. Kwa maana hiyo kitendo cha kumuweka mumeo karibu na mashosti wako unatengeneza mazingira ya kusalitiwa kwa kujitakia.

Pili; mawasiliano ya mume na marafiki wa mke. Sisemi marafiki zako wasiwasiliane kabisa na mumeo lakini unatakiwa kuangalia wanawasiliana kwa mambo gani?

Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakubali mumeo apigiwe simu au achati na marafiki zako halafu hakuna cha maana wanachoongea, walahi utaula wa chuya!

Tatu; mke kuanika siri za mumewe. Kuna hii tabia ya baadhi ya wanawake kuwasimulia mashosti zao siri ambazo hawastahili kuzitoa nje. Kuna wanawake sijui nisema ni ulimbukeni au ushamba! Eti unamkuta mke anasimulia mashosti wake jinsi mumewe anavyompa furaha wanapokuwa faragha.

Unajiuliza ni kwa nini mtu anafikia hatua hiyo. Kimsingi hili ni kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanawake na kujikuta wakikaribisha usumbufu kwa waume zao kutoka kwa wanawake micharuko.Nne; mwanamke kutochukua nafasi yake. Kwa kifupi mwanamke kushindwa kumdatisha mumewe ni kumfanya aangalie wapi kwingine anakoweza kupatiwa kile anachokihitaji.

Hili liwe fundisho kwa wanawake waliobahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa. Kumridhisha mumeo ni kumfanya aepukane na vishawishi vinavyoweza kumfanya akusaliti.

Hata kama wapo wanaopatiwa kila kitu lakini wanachepuka, hao ni wale wasioridhika na ni wachache. Wewe chukua nafasi yako kama mwanamke halafu hakikisha unaziba mianya ya mumeo kushawishika kwa wengine.

0 Response to "Hivi Ndivyo Mwanamke Anavyoweza Kufanya Mpenzi Wake Atembee Na Mashosti Zake. "

Post a Comment