MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUTENDWA
Mambo ya kufanya baada ya `kutendwa’ na mpenzi wako’
Leo nitazungumzia mambo gani ya msingi ambayo mpenzi unapaswa kufanya baada yakutengana au kutendwa jambo lisilomfurahisha na mpenzi wake.
Kupishana lugha na kusababisha malumbano kati ya wapenzi ni jambo la kawaida kama wanadamu, kwani huombana msamaha na kusameheana.
Wapenzi wengi wamekuwa wakilumbana na wakati mwingine wamekuwa wakitoleana siri zao za ndani kutokana na mhemko wa asira kati yao na kufanya penzi lao kuwa shubiri au kutodumu.
Mbaya zaidi ni pale wapenzi hawa wanapotengana, wahajitathimini kujua wapi walijikwaa ili kutorudia makosa ili kujiepusha na kasumba ya kuachwa au kuacha mara kwa mara. Kutokana na kutojitathimini huko, utashangaa katika kipindi kifupi mmoja wao ana mpenzi mwingine!
Hii yote ni kutokana na wengi wa wapenzi kutojua mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wanapokwazana au kutengana.
Leo katika kona yetu, nitazungumzia mambo matatu ya msingi ambayo mpenzi unapaswa kutafakari baada ya kuachana na mpenzi wako.
Jambo la kwanza, mpenzi unachopaswa kufanya baada ya kuachana na mpenzi wako ni kujiuliza kwanini ulimpenda?
Unapaswa kujiuliza hivyo kwa sababu hadi kufikia kuwa wapenzi mmechunguzana mambo mengi ambayo kwa hayo yaliwafanya kuaminina na kufikia hatima ya kuwa wapenzi, wachumba au kufunga pingu za maisha (yaani kuishi kama mke na mume).
Wakati unapojiuliza kwanini ulipendana hadi kuwa wapenzi, lazima urudishe mawazo yako nyuma kwa kukumbuka mazuri ambayo mmefanyiana, lakini usiruhusu kukumbuka mabaya yaliyojiri katika penzi lenu.
Kukumbuka mazuri kunakufanya kisaikolojia kutafakari zaidi na kwa mwanadamu anayetambua umuhimu wa kusamehe lazima huruma inayoambatana na chozi kujitokeza hapo.
Kama hiyo haitoshi, kujiuliza kwanini ulimpenda na kukumbuka mazuri ya nyuma ni ishara kwamba huyo alikuwa mpenzi wako mliyependana, na hivyo lazima `mtima wako’ udunde kidogo pindi litakapokuja swali `automatikale’ kwamba je ninapoachana na huyu, nitampata mwingine atakayenifanyia mazuri, makubwa vile? Na hapo lazima mtima wa kurudisha mahusiana unapoanzia kwa wapenzi waliofundwa!
Kwa kubali kuanzisha mahusiano ni kiashiria kuwa mlikuwa mnapendana na katika hali ya ubinadamu kuhitilafiana ni jambo la kawaida, lazima msameheane na daima kukumbuka mema yaliyojiri katika penzi lenu.
Kwa hiyo katika mazingira mengine unapoupa mtima wako nafasi ya kiburi cha kutosamehe hujenga saikolojia ya kiburi na kawaida ya kiburi hujijenga kama tabia na mwishowe tabia ya mpenzi wa aina hiyo ni kuwa na wapenzi wasiodumu sawa na maji ndani ya pakacha!
Kwa hiyo wewe unakuwa ni mtu wa hivyo, hata mtoto anayeanza kutambua jua na mwezi atafahamu tabia zako, vivyo hivyo thamani yako husinyaa kama ua jangwani.
Baada ya kufahamu kwanini ulimpenda hatua ya pili unayopaswa kuchukwa sasa ni kujiliza kwanini mmetengana wakati mlipendana?
Epuka kukubaliana na msemo wa kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho; kwani kwa kuamini hivyo hata ukiingia ndani ya ndoa msemo huo utakutesa sana na hautadumu katika ndoa kwani utakosa uvumilivu.
Hakuna wapenzi wanaotengana pasipo sababu ya msingi, kaa chini ukiwa peke yako ukiwa umejipumzisha kitandani au kaa kwenye kijistuli chako, kochi, mkeka, au sofa lako pale sebuleni, ila saikolojia ya tafakari nzuri ni kitandani chumbani mwako, hakikisha hakuna kelele halafu jiulize maswali manne ya msingi: Kwanini mmeachana? Kulikuwa na mapungufu gani? Nani anapaswa kulaumiwa? Nani alikuwa mkorofi?
Ndani hayo unapaswa ujiulize tena ,je nimemtendea haki mpenzi wangu? Kama ni ndiyo kwanini kaniacha na kama sio unachopaswa kuangalia uwezekano wa kumfuata na kumuomba msamaha kama ni muelewa atakusamahe na kama sivyo basi unapaswa kuwa makini kwa mpenzi wako mpya.
Lakini inashauriwa kutumia njia washauri mahiri, wanasaikolojia wa mapenzi, wazee na hata ikiwezekana kutumia watu mahiri katika imani kabla ya uamuzi wa kuwa na mpenzi mwingine.
Kwa kujiuliza kwanini mmetenganga itakusaidi kujua sababu za kutengana na baada ya hapo kama ukiamua kuingia kwenye uhusiano mpya itaweza kuepuka kufanya makosa kama uliyoyafanya mwanzo na hivyo itapelekea furaha kwenye penzi lako jipya.
Kabla ya kuchukwa hatua ya kuanzisha uhusiano mapya unashauriwa kutojihusisha katika swala zima la mapenzi si chini ya miezi mitatu na hii itaipa akili yako kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya katika swala zima la mapenzi.
Baada ya kukaa kipindi cha miezi mitatu sasa unashauriwa kuanza kutafuta mpenzi mpya ambaye unaamini hata kutenda kama wa mwanzo, ina unashauriwa kuhakikisha hurudii makosa uliyoyafanya mwanzo.
Jambo la tatu ni kuhakikisha unakamilisha tathimini ya mapenzi. Hii ina maana ya kujitathimini upya kama una kasoro ambazo ni kikwazo katika mapenzi. Mathalani, ukali uliopitiliza, uchoyo, ukosefu wa huruma kwa mpenzi wako, kiburi na roho ya wivu usiokuwa na tija!
Waswahili husema, mke hapigwi kwa kofi au gondo/fimbo, bali mke hupigwa kwa khanga, vivyo hivyo kwa mpenzi. Hakikisha unakuwa mpenzi ambayo unavutia wakati wote, usiyechokwa kwa namna yoyote.
Unatakiwa kuwa na saikolojia ya hali ya juu ya kutambua tabia za mpenzi wako, nini anachotaka, wakati gani na kwa kutambua hayo ni rahisi kuishi katika mapenzi yenye raha wakati wote.
Vijizawadi havitakiwi kukoma kwa mpenzi wako, lakini hakikisha ni zawadi ambayo mpenzi wako anaipenda baada ya kuwa umefanya saikolojia ya kile anachopenda.
Kumekuwa na fikra miongoni mwa watu kuwa mpenzi wa kike hawezi kumnunulia zawadi mpenzi wake, lahasha; ukweli ni kwamba hata mpenzi wa kike huweza kumnunulia zawadi mpenzi wake, na hayo ndiyo mapenzi ya kweli.
Kwa leo naweka nanga kwa hayo machache, wasaa mwingine nitazungumzia mpenzi
mwema ni yupi? Na njia za kumpata mpenzi mwema na sifa za mpenzi huyu.
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en

0 Response to "MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUTENDWA"
Post a Comment