Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne hii Gracia, Sarri, Leeds, Maddison, Maignan, Gomes, Pogba
Kocha wa Watford Javi Gracia huenda akachukua nafasi ya Maurizio Sarri ya kuwa kocha wa Chelsea ikiwa muitaliano huyo ataondoka Stamford Bridge kuelekea Juventus (ESPN) .
Juve inajiandaa kumpa mkataba wa miaka mitatu na kitita cha pauni milioni 6.22 kwa kila msimu. (Corriere della Sera – in Italian)
Wakati huohuo, matumaini ya Eden Hazard ya kuelekea Real Madrid yamewekewa kikwazo na mipango ya kuondoka kwa kocha Sarri. (Evening Standard)
Real iko njiani kumalizia hatua za mwisho kupata saini ya Hazard kwa kitita cha euro milioni 120.Klabu hiyo inawapeleka wawakilishi jijini London kukutana na Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia. (Goal)
Juventus wanataka kumsajili tena kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba.Mchezaji huyo, 26 alichezea ligi ya Serie A kwenye klvbu hiyo kwa miaka minn kati ya 2012-2016.(Sky Italy)
Nasser al-Khelaifi, Mmiliki wa Paris St-Germain anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa Leeds United mjini Doha, Qatar
Mmiliki wa Paris St-Germain Nasser al-Khelaifi, hayuko tayari kumuachia mshambuliaji wa Brazil Neymar, kuondoka msimu huu.(Marca)
Manchester United wana mpango kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison, 22.(Independent)
Beki wa kushoto wa Leicester Ben Chilwell, 22 amesema Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemwambia msimu huu amekuwa mchezaji aliyemvutia zaidi msimu huu.(Mirror)
Klabu za nchini China Guangzhou Evergrande na Shanghai SIPG wanatamani kumchukua mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang wakiahidi kumlipa karibu pauni laki tatu kila wiki.
Manchester United itatoa kitita cha pauni milioni 31 kumpata mlinda mlango wa Lille Mike Maignan,23.(Daily Record)
West ham imetangaza kumuwania kiungo wa kati wa Barcelona Andre kwa kitita cha pauni milioni 20.Gomes alikuwa akiichezea Everton kwa mkopo msimu uliopita.(Guardian)
Cardiff City imekataa dau la pauni milioni 8 kutoka Aston Villa kumuachia mlinda mlango wake Neil Etheridge. (Wales Online)
Bournemouth na Burnley zina mpango wa kumnasa mshambuliaji wa West Brom Jay Rodriguez, 29. (Express na Star)
Mchezaji wa zamani wa Liverpool John Barnes anamini kuwa Virgil van Dijk huenda akashinda tuzo za Ballon d’Or mwaka huu.(Talksport)
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en
0 Response to "Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne hii Gracia, Sarri, Leeds, Maddison, Maignan, Gomes, Pogba"
Post a Comment