Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo fulani hapa Dar lakini kutokana na maamuzi yetu tuliamua aishi mtaani badala ya Hostel. Huyu msichana nilianza nae mahusiano kwa kipindi kirefu sana na hata tumefikia kuvalishana pete na nyumbani kwao nafahamika pia. Kutokana na shughuli zangu nyingi kua mikoani hua tunakutana kwa baadhi ya wikiendi tu ninapokuja hapa Dar. Basi Ijumaa hii nikaona sio vibaya kum-surprise my wife to be. Nikatoka zangu mkoani na shauku ya kujiandaa kwenda kwa P-square na mamaa. Nilipofika pale Geto kwake hali sikuielewa. Nikaona sio mbaya kubisha hodi. Niligonga kidogo tu sauti yenye hasira na mikwaruzo ikatoka ndani. "Wewe Nani"??? Nikajibu kwa kujiamini nikijua wako discussion na wenzake.. "Mimi ni Edwin" Ndani nikasikia kama wanabishana kidogo. Ghafla jamaa akafungua mlango na kuniuliza huku amekasirika wewe nani? Nikajibu kwa kujiamini. "Kama Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?" Basi Grace alipoulizwa akakana kunifahamu. Hapo jamaa akaanza kunishushia kipigo. Kutokana na mwili mdogo nilionao jamaa alinipga kwa kweli huku akitishia kunipigia kelele za mwizi. Basi baada ya pale nikaenda hospital kupata matibabu. Nikaamua kumtaarifu mama yake Grace. Mama Grace alishangaa sana na kudai mbona Grace alimtaarifu tumeachana kwa Mwezi sasa? Nikachanganyikiwa zaidi. Nilipopeleleza zaidi kwa rafiki yake mmoja, nikagundua jamaa ndio anamgharamia Grace kila kitu na kias nilichotoa kwa Grace ilikua hela ya chumvi tu.. Hapa nilipo nina maplasta usoni na sehemu nyingine. Nisaidieni nichukue hatua Gani kisheria juu ya huyu jamaa? Je akisema nilitaka kuiba nitajitetea vipi? Ushauri wenu ni muhimu sana Note Nimetumia majina ya kweli ili kama Grace yupo humu ndani ujumbe umfikie na ajue ameniumiza sana moyoni kwa usaliti aliouonyesha mchana kweupe. Asanteni
Sio Kila EX wako anayeomba Mrudiane anamaanisha! Wengine huomba kurudi ili wakutesti tu jinsi ulivyo Mbulula,jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna Misimamo wala Future.
Jitu mmeachana miezi 6,leo linakutesti lirudishe majeshi,na wewe ulivyo kiazi,upo-upo tu,ina maana miezi yote hii ulikuwa umeganda unasubiria rehema zake ama??
Kurudia Matapishi ya EX ukitegemea Amebadilika ni Sawa na Kupika Sufuria la Makande kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi tu..
Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi??Nini Kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi??Akafie Mbele huko.
KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over umaanishe,sio unakuwa na hisia zinapepea tu kama Bendera ya Katibu Kata wa Kishumundu...Mtu kama Hajielewi achana nae,siku akijirudisha mwambie kwanza akapimwe Minyoo ya Kinyarwanda.
Umekazana kuwaambia marafiki zako 'Siku hizi hakuna Mapenzi ya dhati watu wote Majanga tu',nani amekwambia hayapo??Yapo sana ila wewe unatumia mbinu tofauti..Huwezi kusoma Degree ya Law halafu u-apply kazi ya Chief Accountant wa Bodi ya Tumbaku...Kila siku utasingizia Balance Sheet haina Jurisprudence..Lawyers mmenielewa!
Acha kudate watu wasiojielewa,Usidate kwa sababu uko lonely,Usiwe desperate kuingia Mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls..Ingia kwenye Mahusiano pale Moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na Veins,Auricles,na Aorta za Moyo wako kwamba He/She is really the One..
Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui,ukimuuliza anataka kuwa wapi ndani ya miaka 5 ijayo anakwambia Mungu anajua dont worry,halafu BBM na Instagram unajiita Baby Ake Mie Iam in Love..Utaishia kufua boxer hadi kucha zinukie gololi!
Mbwa kamwe hashughuliki na kesi za Paka kufungiwa kabatini.Date the Right Person,With Right reasons,in a Right Time uone kama Mapenzi hayapo...
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en
0 Response to " Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo fulani hapa Dar lakini kutokana na maamuzi yetu tuliamua aishi mtaani badala ya Hostel. Huyu msichana nilianza nae mahusiano kwa kipindi kirefu sana na hata tumefikia kuvalishana pete na nyumbani kwao nafahamika pia. Kutokana na shughuli zangu nyingi kua mikoani hua tunakutana kwa baadhi ya wikiendi tu ninapokuja hapa Dar. Basi Ijumaa hii nikaona sio vibaya kum-surprise my wife to be. Nikatoka zangu mkoani na shauku ya kujiandaa kwenda kwa P-square na mamaa. Nilipofika pale Geto kwake hali sikuielewa. Nikaona sio mbaya kubisha hodi. Niligonga kidogo tu sauti yenye hasira na mikwaruzo ikatoka ndani. "Wewe Nani"??? Nikajibu kwa kujiamini nikijua wako discussion na wenzake.. "Mimi ni Edwin" Ndani nikasikia kama wanabishana kidogo. Ghafla jamaa akafungua mlango na kuniuliza huku amekasirika wewe nani? Nikajibu kwa kujiamini. "Kama Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?" Basi Grace alipoulizwa akakana kunifahamu. Hapo jamaa akaanza kunishushia kipigo. Kutokana na mwili mdogo nilionao jamaa alinipga kwa kweli huku akitishia kunipigia kelele za mwizi. Basi baada ya pale nikaenda hospital kupata matibabu. Nikaamua kumtaarifu mama yake Grace. Mama Grace alishangaa sana na kudai mbona Grace alimtaarifu tumeachana kwa Mwezi sasa? Nikachanganyikiwa zaidi. Nilipopeleleza zaidi kwa rafiki yake mmoja, nikagundua jamaa ndio anamgharamia Grace kila kitu na kias nilichotoa kwa Grace ilikua hela ya chumvi tu.. Hapa nilipo nina maplasta usoni na sehemu nyingine. Nisaidieni nichukue hatua Gani kisheria juu ya huyu jamaa? Je akisema nilitaka kuiba nitajitetea vipi? Ushauri wenu ni muhimu sana Note Nimetumia majina ya kweli ili kama Grace yupo humu ndani ujumbe umfikie na ajue ameniumiza sana moyoni kwa usaliti aliouonyesha mchana kweupe. Asanteni"
Post a Comment