Nesi Afungwa Maisha kwa Kuuwa Wagonjwa 85 - Bongo Loves

Nesi Afungwa Maisha kwa Kuuwa Wagonjwa 85


Nesi mmoja nchini Ujerumani amekutwa na hatia ya kuua wagonjwa 85 katika hospitali mbili kaskazin mwa Ujerumani na kupatiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Jaji Sebastian Buehrmann ametaja vitendo vya mauaji vya nesi huyo Niels Högel "haviingii akilini."

Högel, ambaye anatumikia vifungo vingine viwili vya maisha jela kwa mauaji ya wagonjwa, alikuwa akidunga dozi kali za dawa za moyo kwa watu aliokuwa akiwahudumia baina ya mwaka 1999 na 2005.


Inaaminika kuwa yeye ni mtu ambaye kauwa watu wengi zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Ujerumani.

Wapelelezi wanadai kuwa lengo lake lilikuwa ni kuwastaajabisha wafanyakazi wenzake kwa kuwarejeshea fahamu wagonjwa (ambao hata hivyo aliwalaza kwa kificho kwa kutumia dozi kali).

Moja ya wafanyakazi wenza wa zamani wa nesi huyo ameliambia gazeti la Bild la nchini humo kuwa Högel alipewa jina la utai la "Rambo wa ufufuo" kutokana na namna "alivyokuwa akiwapiga vikumbo watu wote wampishe" pindi mgonjwa alipokuwa akihitaji kurejeshewa fahamu.

Katika siku ya mwisho ya kesi yake, Högel, 42, aliziomba familia za wagonjwa aliowaua wamsamehe "matendo yake mabaya".

"Ningependa kuwaomba radhi kwa kila kitu kibaya nilichowafanyia katika miaka yote ile," alisema.

Haki miliki ya pichaAFP
Högel alikuwa akishtakiwa kwa kuuwa watu 100 katika miji ya kaskazini ya Delmenhorst na Oldenburg. Polisi wanaamini kuwa nesi huyo aliua watu wengi zaidi ila ushahidi unakosekana kutokana na baadhi ya miili ya watu hao kuchomwa moto.

Högel alikiri kuua watu 55 na mahakama ya Oldenburg ilimkuta na hatia ya kutekeleza mauaji ya watu 85, vyombo vya habari vya ujerumani vimeripoti.

Akitoahukumu yake, Jaji Buehrmann ameelezea kusikitishwa kwake kuwa mahakama hiyo imeshindwa kuondoa wingu lililotanda ndugu wengi ambao bado wanaomboleza kuuawa kwa wapendwa wao.

Nesi akiri kuua wagonjwa 100 Ujerumani
Mwandishi wa BBC wa Berlin, Jenny Hill amesema kesi hiyo imewashangaza wengi nchini Ujerumani - huku uongozi wa juu wa hospitali mbili zilizokubwa na kadhia hiyo wakilaumiwa kutochunguza mapema ongezeko lisilo la kawaida la idadi ya vifo kwenye vituo vyao.

Högel alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 akimdunga mgonjwa sindano ambayo hakuandikiwa katika mji wa Delmenhorst.
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en

0 Response to "Nesi Afungwa Maisha kwa Kuuwa Wagonjwa 85 "

Post a Comment