Mambo Matatu ya Muhimu Unayoweza Kufanya ili Kumdatisha Mpenzi Wako Bila Kutumia Pesa - Bongo Loves

Mambo Matatu ya Muhimu Unayoweza Kufanya ili Kumdatisha Mpenzi Wako Bila Kutumia Pesa



Na Martha Magawa

Nikikuuliza unapenda kipi kutoka kwa mpenzi wako najua wengi watatoa majibu tofauti tofauti wapo watakao sema, mcheshi, anamvuto napenda anavyotabasamu na vitu vingine kama hivyo, LAKINI leo kupitia Udaku Special Mapenzi karibu uyatambue mambo matatu muhimu ili kumdatisha mwenza wako.

1.UZUNGUMZAJI WAKO
Unavyozungumza na mpenzi wako ni tofauti kabisa na navyozungumza na watu wengine. Ni hatari sana kutumia lugha ya ukali ama isiyo ya kiungwana kwa mpenzi wako. Unatakiwa kufahamu kwamba, mpenzi wako ni mtu muhimu sana katika maisha yako hivyo unatakiwa kuwa makini pindi unapozungumza naye.

Kuonesha kwamba wapo wasiojua mapenzi ni nini, unamkuta mtu anamwita mpenzi wake majina kama vile mshamba, demu, shembe na mengine mengine kama hayo. Mpenzi wako kweli umuite demu? Na wale wengine kule mtaani utawaita nani?

Huo si ustaarabu na kamwe mapenzi yenu hayawezi kushamiri kwa mtindo huo. Kuna wengine matusi hayawaishi midomoni mwao. Kwa kufanya hivyo jua tu kwamba unamboa laazizi wako. Aidha mapozi katika uzungumzaji wako ni miongoni mwa vitu vinavyoweza kumdatisha

2.TABIA ZAKO
Huu ndio msingi imara wa uhusiano wa kimapenzi. Wapo wanawake ambao ni wazuri na wenye kila sifa ya kuwa na wapenzi bora, lakini kutokanana tabia zao chafu wamekuwa wakiachwa kila wanapoingia katika uhusiano.

Nani atakupenda na kudiriki kuendelea kuwa katika uhusiano na wewe kama tabia zako si nzuri? Wengi wetu tunapenda kupata sifa ya kuwapata wapenzi ama wachumba wenye tabia nzuri ili tuweze kusifiwa na marafiki zetu pamoja na wazazi.

Kwa maana hiyo basi, kuwa makini sana na tabia ambazo unajua haziwezi kumvutia mpenzi wako ama jamii inayowazunguka kama vile WIVU uliopitiliza kiasi cha kuwa kero, kutaka makuu pamoja na tamaa zisizo na msingi.

Nimeweka wivu juu kutokana na ukweli kwamba, kuna wanawake hata wakiwakuta wapenzi wamesimama ama kupigiwa simu na mtu wa jinsia tofauti bila kujua ukweli wa mambo wanaanzisha vurumai, huu ni ulimbukeni.

3. JINSI UNAVYOMRIDHISHA
Yote hayo hapo juu ni tisa, lakini kumi ni jinsi unavyoweza kumridhisha mpenzi wako hasa mnapokuwa faragha mkipeana raha za dunia.

Hata kama una tabia nzuri na umbile la kumvutia kiasi gani, kama huna utaalam na ujuzi wa kutosha katika kumpa raha mpenzi wako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa, lazima penzi ama ndoa yako itakuwa na walakini.

Lakini kitu ambacho kimekuwa kikiwavutia walio wengi waume kwa wanawake ni utundu na ubunifu wakati mnapokuwa faragha. Kinachotakiwa ni kupeana kile roho inataka ili suala la kusalitiana lisiwepoUSISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en

0 Response to "Mambo Matatu ya Muhimu Unayoweza Kufanya ili Kumdatisha Mpenzi Wako Bila Kutumia Pesa "

Post a Comment