Dalili 9 Kwamba Mpenzi Wako Amepata Mchepuko
Mtaalamu wa ushauri wa maswala ya ndoa, Sheri Meyers aliandika kitabu kilichotoka mwaka 2012 akiwa na lengo la kuelimisha zaidi kuhusu uzoefu wake alioupata kutokana na kujaribu kutatua migogoro mingi ya wanandoa waliokuwa wanakwenda kupata huduma za ushauri kutoka kwake.
Anasema kwamba “hisia za mapenzi ” ni ngumu kuzielezea kama zilivyo hisia nyingine — na mara nyingine ni ngumu kujijua kama una hisia hizo, na ugumu zaidi ni kujua endapo mtu uliyenaye kwenye uhusiano ana hisia za namna hiyo kwako.
Sababu hiyo ndiyo ilimfanya aandike kitabu cha “Chatting or Cheating” ili kuwasaidia watu kugundua baadhi ya ishara zinazoweza kumaanisha kuwa mpenzi wako ameanzisha uhusiano na mchepuko, hata kama bado hujathibitisha.
Zifuatazo ni dalili tisa ambazo ukiziona kwa mpenzi wako, basi yawezekana akawa ameanzisha uhusiano na mchepuko:
Mpenzi wako anatumia muda mrefu zaidi kwenye simu/kompyuta
Mabadiliko ya ghafla kwenye matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivi vya mawasiliano ya kidigitali, hasa kwa wizi (akiwa anakuvizia usipokuwepo naye) ni ishara mbaya.
Meyers ameandika: “Unaweza kumwona mpenzi wako anashtuka unapoingia chumbani baada ya kumuacha peke yake au akaiweka simu pembeni ghafla. Wanaweza kuwa na mawasiliano mazuri kwa siku nzima lakini ukashindwa kuyabaini au kuyafatilia kwakuwa hampo pamoja.”
Mnapogombana anasema kwamba amegundua unataka muachane
Anakuwa mwepesi kukutupia mpira ili kukwepa hatia aliyonayo, hasa mnapogombana. Utamsikia mpenzi wako akitoa kauli kama, “Utafanya nini kama tukiachana?” au jambo la kushtua zaidi kama, “Endapo uhusiano wetu utafikia mwisho, bado nitaendelea kukupenda kama rafiki.”
“Kwa ujumla, wanakuwa na mawazo hasi tu kila mnapogombana badala ya kufanya jitihada za kutatua matatizo yaliyopo kama ufanyavyo wewe,” ameandika Meyers.
Unapomuuliza mpenzi wako kuhusu rafiki zake, anajitetea au anakwepa kujibu
Inaweza kufika wakati ukaanza kumdadisi ili kujua kinachoendelea kati ya mpenzi wako na mtu unayehisi ana uhusiano naye. Angalia iwapo mpenzi wako atajificha kwa kutoa majibu ya mkato sana au majibu yenye maelezo mengi sana.
Kwenye hili, Meyers amesema: “Atatoa jibu fupi sana na la mkato unapomuuliza swali jepesi kabisa kuhusu mtu aliyesema ni ‘rafiki’ au mfanyakazi mwenzake, au atajidai anatoa maelezo mengi sana bila sababu yoyote – na unakuta maelezo yenyewe yanazidi kuongeza shaka.”
Mpenzi wako ameanza kubadilisha sana aina ya mavazi yake anapotoka
Kwa mwanaume, unaweza ukaanza kupata wasiwasi mpenzi wako anapoongeza kasi ya kununua nguo mpya ambazo zinaacha wazi maungo yake, kana kwamba anamvutia mwanaume mwingine tofauti na wewe.
Au, kama Meyers anavyosema, unaweza kuona mpenzi wako ameanza ghafla “kutaka kupunguza uzito wa mwili, kuanza mazoezi, kununua nguo mpya zenye muonekano tofauti na uliouzoea, kubadili mitindo ya nywele, [na] kuzidisha vipodozi mara kwa mara.”
Mpenzi wako akianza ghafla kuhitaji aachwe peke yake zaidi
Kama mpenzi wako ana mchepuko hasa, jambo kubwa atalojaribu kufanya ni kujiweka mbali na wewe kila anapoona inawezekana ili apunguze uwezekano wa wewe kugundua nyendo zake za nje.
“Utamuona anataka kufanya vitu vyake mwenyewe na kubadilika kwa kutotaka kufanya vitu kwa kushirikiana akitoa visingizio mnapokuwa mnapanga ratiba ya pamoja ya kifamilia kama safari, likizo au kutembelea familia,” ameandika Meyers.
Mpenzi wako anapokukosea sana kuhusu muonekano au tabia yako
Unaweza kugundua kwamba sasa mpenzi wako hakuangalii kwa umuhimu mkubwa kama ilivyokuwa awali. Meyers anasema kuwa unaweza kuona mpenzi wako anaanza “kukosoa mambo mengi kuhusu wewe ambayo mwanzoni wote mlikuwa mnayaona ni yenye mvuto mkubwa na yanawapendeza – lakini ghafla yanakuwa hayana mvuto kwake tena na hayapendezi tena.
Mabadiliko ya mambo anayoyataka mnapojamiiana
Mahitaji na tabia ya mpenzi wako mnapojamiiana yanaweza kwenda kwenye upande mmojawapo:
Kwa upande wa kwanza, Meyers anasema kuwa, “inaweza kuonekana kama mpenzi wako ana msongo wa mawazo au akili yake kutokuwepo kabisa kwako – kiakili au hisia za mapenzi.”
Kwa upande wa pili, mpenzi wako anaweza kubadilika ghafla na kuanza kutaka kujamiiana zaidi au kukutaka mjaribu mambo mapya mnapojamiiana. Hali zote mbili zinaweza kuwa na ishara mbaya kwamba ameanzisha uhusiano na mchepuko.
Mpenzi wako kuzidisha kumtaja mwanaume/mwanamke mwingine
Meyers amegundua kwamba, iwapo mpenzi wako atakuwa ameanzisha uhusiano wa nje wa kimapenzi, basi “utakuta anaanzisha mazungumzo kwa kukuuliza vitu kama … ‘Hivi, unadhani inawezekana kumpenda mwanaume/mwanamke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja?’ na hili yawezekana lisiwe swali la mzaha kama watu wengi wanavyopenda kudhani.
Unapohisi kwamba inawezekana kuna uhusiano kati ya mpenzi wako na ‘rafiki yake’
Hapa pia, tabia ya mpenzi wako yawezekana ikaelekea upande mmoja katika pande hizi mbili, anasema Meyers.
Kwanza unaweza kumuona “anavyobadilika kila huyo ‘rafiki yake’ anapokuwa karibu” au utaona “anavyoanza kumkandia sana kukufanya udhani kwamba mtu wa aina hiyo hawezi kuvutiwa naye kimapenzi au kuwa naye kwenye uhusiano wowote.”
Unapokuwa na hisia za aina hii kuhusu mpenzi wako, usizidharau haraka, hasa kunapoonekana mabadiliko ya tabia. Si lazima hisia zako ziwe za kweli, lakini ni vyema ukathibitishe kabla ya kuziacha.
Hata hivyo, tahadhari inabidi izingatiwe kwamba si tu kwa sababu umeona baadhi ya ishara hizi kwa mwenza wako – basi ikamaanisha moja kwa moja kwamba ana mchepuko – yawezekana ikawa ni mambo mengine kama matatizo makubwa kazini. Unapoona wasiwasi unakuzidi, siku zote ni bora zaidi kuzungumza hisia zako kwa mpenzi wako ili naye apate nafasi ya kueleza upande wake na ujue sababu za mabadiliko hayo. Kumlaumu moja kwa moja kwamba ameanzisha uhusiano na mchepuko wakati sababu yawezekana kuwa amefukuzwa kazi inaweza kuweka ndoa au uhusiano wenu pabaya zaidi, kwahiyo, mara zote ni bora zaidi kuzungumza.
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en
0 Response to "Dalili 9 Kwamba Mpenzi Wako Amepata Mchepuko "
Post a Comment