SABABU KUU ZA WANAWAKE KUCHITI KWENYE MAHUSIANO - Bongo Loves

SABABU KUU ZA WANAWAKE KUCHITI KWENYE MAHUSIANO



Asilimia kubwa sana katika mahusiano kumekuwa na jambo la kutoaminiana.
Tunapoongelea why Girls cheat? Wewe unafikiri ni kwanini msichana anafikia kuwa na tabia hiyo?   Je ni tamaa? pesa? na vipi kama nikisema maranyingine mwanaume anaweza kusababisha msichana kuanza tabia hiyo hata kama hakuwanayo??  Kama vile

Ø  kupungua kwa urafiki wa kimapenzi , msichana anaweza kuwa na kila kitu  kama nyumba nzuri, magari na vitu vya thamani,kwa ufupi nje kuko sawa lakini ndani  akawa anapungukiwa kitu kimoja tu na muhimu sana katika mahusiano yake urafiki wa kimapenzi.
Kama unavyojua sio tu tendo la ndoa linalofanya wanawake kujisikia wameunganishwa katika mahusiano; kuna kama kushikana sehemu maalum ambazo zitampa msisimko, mabusu motomoto, na kuwa na mahusiano mazuri kati ya mtu na mpenzi wake. Women crave it, na akikosa huduma hiyo nyumbani anaweza kuitafuta  inapopatikana.Na hili kuboresha urafiki tenga mda maalumu na mpenzi wako, na kuwa na tabia ya kumpa nafasi ya kutoa mawazo yake na hakuna kitu kibaya kama kutojua mpenzi wako anapenda nini na hataki nini; na kama kunahitajika kufanya maamuzi sehemu Fulani basi si vibaya kama utamshirikisha na kutimiza mambo yote hayo kunaleta ukaribu zaidi kwa wapendanao.

Ø  Kutokuwa na imani kwa mpenzi wako ,Kukosa kumuamini  kunaleta kuchoka na kukata tamaa, Mke wako ni mzuri yes na inawezekana kila unapopita unasifiwa lakini inaonekana moyoni mwako kuna wasiwasi uliojengeka unaibiwa, pamoja  na wasiwasi na simu zinazoingia na kutoka, na kuzuia safari za hapa na pale ukifikiri kwamba atakapotoka ataharibu. Hakuna kitu anachopenda mwanamke kama kumwamini na kumthamini kuwa yeye ni mtu mzima na anaweza kuwa na maamuzi ambayo yatajenga na kuimarisha mahusiano yenu. Inawezekana kabisa hukawa na tatizo la kutomwamini mtu anayeitwa mwanamke lakini kumbuka sio wote wako hivyo unavyofikiria wewe au ulichowahi kufanyiwa. Trust your woman.

Ø  Kupungua kwa tendo la ndoa ,Kumbuka awali ulimuona kama lulu na kutotaka kubanduka  machoni pake wakati mkiwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa mara kwa mara na michezo ya kitoto. Alafu punde tu majukumu yalipoanza na watoto pia ambao ni Baraka kwa wazazi. Na kabla hamjatambua hilo kwenu kulala ikawa ni muhimu sana kuliko tendo la ndoa. Mara nyingi sana mwanamke anapenda sana kuhisi anatamaniwa. Na kama hutamfanya ajisikie hivyo basi ni fursa pekee ya kutoka nje. Hivyo basi kuongeza chachu kwenye mapenzi, mfanyie mitoko ya kimapenzi,mtumie msgs za kusisimua mida ya lunch na utani hapa na pale,

Ø  HEARTBREAK. inavunja uaminifu aliokuwanao msichana  hapo awali na kujisikia kujeruhiwa na kulaghaiwa ndipo hapo sasa inapoleta mawazo mabaya ya kulipiza kisasi au kutolipa umuhimu swala zima la uhaminifu katika mapenzi na mahusiano.
But why do you cheat??

0 Response to "SABABU KUU ZA WANAWAKE KUCHITI KWENYE MAHUSIANO"

Post a Comment