Nimesalitiwa na Mpenzi Wangu Nimeona Live, Naumia Sana. Nimeachana nae
Natumai wote ni wazima
Juzi nilipanga kuonana na mpenzi wangu tutoke out weekend tukale bata ndogondogo za hapa mjini baada ya mihangaiko ya wiki nzima. Sijui ananipenda kiasi gani ila mimi nampenda sana.
Mchana wa juzi tulikutana nae na tukapanga kutoka usiku ila kilichotokea ni kwamba ilipofika saa 2 nikampigia simu akawa hapokei, baada ya muda nikasema maybe yupo busy sana ngoja niende kwake (sio mbali less than 1km) sina mazoea hayo ila siku hiyo moyo ulinisukuma kufanya hivyo. Nilipokaribia nikaona kuna gari (harrier) imepaki nje na yeye akaingia. Gari ilipoondoka ilikuja uelekeo nilipo na nikaona kuna mdingi ndani wao hawakuniona.
Baada ya mda akanitumia txt "bby nilikuwa naoga ntakuxtua". Nikajifanya boya nikamwambia poa. After that akaja kunijibu mda umeenda sana tutatoka next time.
Very easy nikamwambia asinitafute tena, japo nimeumia sana.
USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en
0 Response to "Nimesalitiwa na Mpenzi Wangu Nimeona Live, Naumia Sana. Nimeachana nae "
Post a Comment