MA EX GIRLFRIENDS WA MUME WANGU WAMEUNGANA KUNISHAMBULIA - Bongo Loves

MA EX GIRLFRIENDS WA MUME WANGU WAMEUNGANA KUNISHAMBULIA

Mimi ni mama wa watoto wawili mapacha. Niliolewa 2010 na kijana m handsome sana. Sikufanya effort yeyote kumpata. Sikumwendea kwa waganga wala sikulala makaburini ili anioe. Nilikutanae kwenye ndege na tulikaa pamoja, huo ulikuwa ndio mwanzo wa mapenzi yetu. Miaka mitatu ya uchumba ilikuwa mitamu sana na haikuwa na makuu. Baada ya kuolewa ndipo makasheshe yalipoanza. Siku moja nikiwa dukani kwangu walikuja wadada wawili wakajitambulisha mmoja ni Jack na mwingine ni Irene, wakaniambia mume wangu alikuwa ni boyfriend wao kwa nyakati tofauti na hawawezi kuishi bila yeye. Kwakweli nikaona ni kama sinema, wakaniomba niwape ruhusa wawe wanakuja nyumbani kulala na mume wangu. Kwakweli walinikera, nikaondoka dukani na kurudi nyumbani huku nikilia kwa hasira. Mzee alipokuja nikampa kisanga kizima. Tangu hapo wanawake hao wamekuwa wakinisakama kwa msg za matusi. Wanamtukana pia mume wangu kuwa eti nimemroga. Kwa kweli wamekuwa ni kero kwa familia yetu. Jamani sijui wadada wengine wameumbwaje? Mume wangu kasema atawapeleka polisi iwapo watanifuata tena dukani. Dukani sasa hawaji ila tunakomaje na mitusi ya kwenye sms?USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍

0 Response to "MA EX GIRLFRIENDS WA MUME WANGU WAMEUNGANA KUNISHAMBULIA"

Post a Comment