Njia za kuondoa msongo wa mawazo (Stress)
Mara nyingi mtu anapokuwa na msongo wa mawazo anakuwa tofauti na vile alivyo na hata ufanyaji wake wa kazi unakuwa tofauti, kama ni kazini anakuwa mwenye unyonge na hata waliopo karibu yake umuona kuwa ni tofauti na vile alivyo.
vipo vitu vingi vinaweza kuleta msongo wa mawazo, ikiwa pamoja na:-
- kuachwa na mpenzi au matatizo katika mahusiano
- ugumu wa masomo,
- kubanwa sana na kazi au matatizo kazini ,
- marafiki,
- hata ugumu wa maisha.
- kulala sana bila mpangilio na isivyo kawaida
- kutokupata usingizi kabisa hasa wakati wa usiku
- kupoteza kumbukumbu ya vitu vingi
- mabadiliko katika tabia yako ya kula
- kuwa na hasira, kukataa tamaa na mara nyingi hata kujikuta unalia bila sababu.
- mara nyingi unakuwa na wasiwasi na hujiamini.
- Jua nini sababu ya msongo wa mawazo kwanza na kisha jitahidi kwa kiasi kikubwa kuepukana na tatizo ilo, mara unapojua tatizo lako linasabbaishwa na nini itakuwa rahisi sana kupata muafaka wa tatizo ilo na hii itakusaidia hata unapotafuta ushauri kwa watu inakuwa rahisi kujielezea.
- jifunze kusema hapana.-jitahidi sanakatika maisha kufanya kila kitu kwa kuangalia uwezo wako wa mwili na kila kitu pia, kama unaona kuwa kuna vitu viko nje ya uwezo wako kifedha, kiakili ,kimwili na hata maarifa ni bora kuachana nacho au kutafuta suluhisho na sio kulazimisha mambo.
- wakwepe watu wanaokusababishia tatizo-kaa mbali na wale wanaosababisa ujionekuwa uko tofauti nao au uwezi kitu, kama ni mahusiano yanakwenda kombo sio lazima kuwa namahusiano kwa wakati huo ni bora kujipa muda na kujitafakari kabla ya kujiingiza huko tena, kama ni marafiki wanakupa mawazo basi kaa nao mbali kwa muda huku ukitafuta njia ya kuishi nao.
- badilisha mazingira ya chanzo.-jitahidi kuyakwepa yale mazingira ambayo yanakupa mawazo muda wote, kama una pesa safiri na uwendembali kupumzisha akili yako, au jipe likizo hata ukatembelea sehemu tulivu peke yako ili akili iwezie kupumua.
- usijaribu kulikabili lile usiloliweza.-kama kuna kitu uweiz basi achana nacho sio lazima ukifanye wewe, fanya yale yanayowezekana kwa muda huo na kwa kiwango chako.
0 Response to "Njia za kuondoa msongo wa mawazo (Stress)"
Post a Comment