Jitahidi kumuonyesha kuwa unampenda mfanyie hivi - Bongo Loves

Jitahidi kumuonyesha kuwa unampenda mfanyie hivi

 Image result for love couple black
Yawezekana hii ndiyo sababu mapenzi ya sasa yamekuwa na changamoto, mateso na maumivu sana kwa sababu mtu anamuaminisha mwenzake kwamba anampenda kwa kutamka ‘nakupenda’ nyingi wakati ndani ya moyo wake, hana mapenzi hata kidogo bali anasukumwa na tamaa za kimwili.
Swali la msingi ni je, utajuaje sasa kwamba anayekwambia ‘nakupenda’ anamaanisha kutoka ndani ya moyo wake na utamjuaje ‘anayekuzuga’ kwamba anakupenda? Swali hili pia lina upande wake wa pili, kwamba ukimfanyia nini mpenzi wako ataamini kwamba unampenda kwa dhati na si kwamba unaongozwa na tamaa zako za mwili?
Je, utamfanyia nini mpenzi uliyeishi naye miaka mingi aamini kwamba bado upendo wako kwake haujachuja na kwamba unampenda leo kuliko jana? Majibu ya maswali haya ni mepesi sana, twende pamoja kuchambua mbinu moja baada ya nyingine kama ifuatavyo:
  1. MSAIDIE BILA MASHARTI YOYOTE
Kihulka, mtu yeyote huwa anafarijika sana anapomuona mtu mwingine akimsaidia kufanya jambo fulani, hata kama ni dogo kiasi gani. Siyo lazima umsaidie kitu kikubwa, hapana! Kumsaidia tu unayempenda kubeba mkoba wake kuna maana kubwa sana katika mapenzi.
Hii inawahusu wote, wale ambao wapo kwenye hatua za mwanzo za safari yao ya mapenzi au walioishi miaka mingi pamoja! Ukiwauliza wanawake wengi, watakwambia hakuna kitu kinachowafurahisha kama kusaidiwa kazi ndogondogo na wanaume wanaowapenda. Kama ni mkeo hebu siku mfanyie sapraizi kwa kumuoshea vyombo au kuwaogesha watoto (kama mnao) au mfulie nguo zake.
  1. MPE KIPAUMBELE MNAPOKUWA PAMOJA
Ukimpenda mtu kwa dhati, hata mnapokuwa kwenye mkusanyiko wa watu wengi, akili yako yote itakuwa kwake, utataka kila anachokiongea ukisikie na umjibu kwa haraka, utapenda akicheka na wewe ucheke, akiumizwa na kitu uwepo karibu yake na hisia nyingine za aina hiyo.
Mkiwa wawili utapenda muda wote umtazame, mfurahi pamoja na ukaribu wenu usiingiliwe na chochote, huo ndiyo upendo wa dhati unavyopaswa kuwa. Cha ajabu siku hizi mambo ya teknolojia yanawafanya wengi wawe washamba wa mapenzi.
Umetoka out na mpenzi wako lakini cha ajabu, muda wote upo bize na simu, mara WhatsApp, mara Instagram au Facebook! Inawezekana vipi ukawa makini kumsikiliza anachokizungumza na muda huohuo ukawa unaendelea kuchati.
Unapochati mbele yake ni kwamba umeona simu ni ya muhimu kuliko yeye, sasa ataamini vipi kama unampenda wakati unashindwa kumpa kipaumbele hata katika kitu kidogo kama hicho?
Wanandoa wengine unakuta muda pekee ambao wanakutana pamoja, ni jioni baada ya shughuli za kutwa nzima kuisha lakini cha ajabu sasa, jioni ikifika wakikutana, baba yupo bize na simu mama yupo bize na tamthiliya, au baba yupo bize kutazama mpira kwenye runinga mama yupo bize na simu!
Kwa namna hiyo unafikiri hata ukimtamkia ‘nakupenda’ elfu kumi kwa siku atakuamini? Hakuna mapenzi hapo na hata ukisema nakupenda, ni maneno tu ya kawaida ambayo yanatoka mdomoni na siyo moyoni.
  1. WAONESHE WATU WENGINE KWAMBA UNAMPENDA
Watu wengi huwa wagumu sana kuonesha hadharani kwamba wanampenda mtu fulani. Yaani kama ni mwanaume, akiwa na mpenzi wake mbele za wenzake, hakuna chochote anachoweza kukifanya mpaka kila mtu akajua kwamba huyo aliyenaye, siyo dada yake wala ndugu yake, bali mpenzi wake.

0 Response to "Jitahidi kumuonyesha kuwa unampenda mfanyie hivi"

Post a Comment