Njia 15 Za Haraka Za Kumsahau Ex - Boyfriend Wako - Bongo Loves

Njia 15 Za Haraka Za Kumsahau Ex - Boyfriend Wako


Kama umekua na wakati mgumu sana wa kumsahau mpenzi wako wa zamani, unaweza hitaji msaada kutoka nje. Hizi ndizo namna za kumsahau Ex- boyfriend wako.

Kuwa na uhusiano unaodumu haitokei sana kwa watu wengi - hasa katika ulimwengu wa sasa. Na inauma sana pale unapoachana na mtu ambaye awali haukuwa hata na wazo la kuwa naye lakini baadae mkawa wote na akaja kukuacha. Ni ngumu sana kumsahau - Lakini, kuna baadhi ya mambo unaweza kuyafanya na yakakufanya umsahau kabisa x-boyfriend wako - na kuachana na masononeko ya kila siku ambayo hayakusaidii.

Kwanini kuachana ni kitu kigumu sana?


Nadhani wote tunajua kuwa
kuachana na mpenzi wako ni jambo gumu sana kwa sababu ni jambo linalogusa na kuvunja mioyo yetu. Kusema kweli, inauma sana kuona mtu unamjali lakini yeye hakujali kwa lolote, lakini kwanini iume sana mtu asipokujali?

[Soma: Kwanini mapenzi yanaumiza sana pale yanapokwenda kombo!]

Ukweli ni kwamba maumivu huja kwa sababu ya miunganiko ya mambo mengi ndani yake. Kwanza, haukutegemea jambo kama hilo lingetokea kwa hiyo imekua mshtuko wa kuumiza. Lakini pili, Una deal na kukataliwa jambo si lakawaida kama mambo mengine.

Na sababu kubwa kabisa ya kwanini unaumia ni kwa sababu maisha yako yameshakuwa tegemezi kwa mtu mwingine. Siku zote ushamzoea kiasi kwamba akikosekana tu katika maisha yako unajiona mtupu - huwezi fanya jambo lolote bila yeye. Na kuwa mtupu - mpweke inakua ni ngumu sana kuyazoea hayo mazingira - hivyo kuumia moyo.

[Soma: Namna ya kumsahau mwanaume ambaye unazani huwezi kumsahau!]

Namna ya kumsahau X wako


Muwe na amani wanawake wenzangu. Hii haikutaki ufanye sana kazi au uhangaike sana ili umsahau x wako. Ukweli ni kwamba kuna mambo lukuki unayoweza kufanya yakakusaidia kumsahau huyo jamaa yako wa zamani. Makuu ni haya yafutayo:-

#1 Usiliweke sana moyoni hilo jambo. Nnachomanisha ni kwamba, kama unataka kuwa na huzuni na kulia siku nzima - LIWEKE MOYONI!. Usizishike wala kuzikumbuka hisia mbaya za nyuma maana zitakufanya ushindwe kufanya mambo mengine - na hii maumivu yatakuwa makali zaidi. Hivo sahau tu kama unavyotoa pumzi - usijaribu wala kukumbuka mambo mliyoyafanya nyuma hata yawe mazuri kiasi gani - hiyo ilikua historia - tazama mbele kwa mapya - Jipe moyo wewe ni mwanamke wa Nguvu na Siyo tu Msichana.

#2 Futa namba zake na usimfate katika mtandao wowote ule wa kijamii. Kila kitu kifute. Mara nyingine unaweza kuwaza, "Vipi kama nitahitaji ____", HAPANA!, Tambua mmeshaachana na nyie ni watu wawili tofauti kila mtu ana mambo yake - hamtegemeani - so Futa mana hautamuhitaji kwa jambo lolote lile. Na niamini, unapokua umelewa unaweza ukahitaji kumtext, lakini hautaweza kwa sababu hauna tena namba yake. [soma: Namna ya kuachana na mwanaume ambaye bado unampenda - lakini unaona hana muelekeo!]

#3 Tupa kila kitu chake ulichonancho kinachomuhusu yeye. Mrudishie au kama anajishaua tupilia mbali, au fanya vyovyoyte vile ili usiwe na kitu chochote kinachoweza kukufanya umkumbuke yeye. Usijali hatakama ni kwa kiasi gani unapenda kulala na ile T-shrt aliyokunulia. Usipepese macho - Zichome kabisa. Itakufanya ujisikie wa amani kabisa.

#4 Epuka kuangalia Movie za kimapenzi. Mnapokua mmeachana naye - jitahidi sana usiwe unaangalia hizo movie mpaka utakapompata mwingine. Maana hii inaweza kukuliza na kusema huwezi pata mwanaume mwingine anayeweza kukupa mapenzi kama yale. Lakini niamini - -hizo movie hazinaga uhalisia ndo mana yakaitwa maigizo, ukiziangalia zitakufanya uwe unalia na utamtafuta mwishowe. Usifanye hayo mambo kama unataka kusahau X boy wako.

#5 Waambie mashoga zako. Najua kuna mambo mengi sana unahitaji kuyasema kwa mashoga zako - lakini hili ni lamuhimu zaidi, jihimu na waambie. Wapigie simu na uwaambie kilichotokea, na kama vipi andaa hata ka party kidogo kako na mashoga zako mana inawezekana ni kitambo hamjaonana mana huyo X wako alikua hata hakuachi ukapumua uwaone mashoga zako. Yachome mambo yote yake, itakufanya ujisikie wa furaha.[Soma: Namna ya kufanya mambo yako baada ya kuachana na X wako!]

#6 Kuwa busy. Huu sasa ndo muda muafaka wa kumuomba bosi wako kazi za ziada(Extra works) na hakikisha kichwa chako unakielekeza katika hobies zako. Ukiwa hauna cha kufanya unakuwa unajijengea muda mwingi wa kumkumbuka X wako na utammisi.

Kama kweli unataka kumsahau kiurahisi - piga kazi kama kichaa kwa ajili ya maendeleo yako binafsi. Jiunge katika vikundi, nenda mazoezini, ka meditate, fanya kazi za kujitolea katika jamii na mambo mengine yanayofanana na hayo. Hilini jambo muhimu sana usije ukalisahau hata siku moja.

#7 Jitahidi sana muda mwingi usiwe peke yako. Hili ni jambo lingine linaloweza kukufanya ummisi. Pangilia muda wako wa siku kiasi kwamba utakuwa na muda mchache sana katika siku ambao utakuwa mwenyewe. Ukiwa mpweke muda mwingi - itakufanya uimisi kampani yake, na hiyo siyo kitu nzuri kama kweli unataka kumsahau. [Soma: Hatua 10 za kuachana na mpenzi wako na jinsi ya kuzipita zote!]

#8 Fanya mambo ambayo alikua hayapendi. Napendaga sana kutoka Out na kufanya mambo ambayo X wangu alikuwa hayapendi. Nilikua na X ambaye alikua hapendi hata tuukaribie mgahawa. Kwa hiyo baada ya kuachana, nilikua naenda mgahawani angalao mara moja kwa week kujifunza mapishi mapya ya wanawake wenzangu.

#9 Panga Upya nyumba yako. Kama nyie wawili mliishi kwa pamoja kwa muda mrefu ni wazi kwamba ile sehemu itakuwa ishammisi kama haukupanga na kuweka muonekani mpya ndani ya nyumba yako. Muonekano mpya wa nyumba/ chumba chako utaashiria kuwa mambo yamebadilika. Hii itakusaidia na hautamkumbuka wala kummisi.

#10 Kanyoe nywele zako. Hili ni jambo la kiwango sana wanawake wengi wanaojielewa hulifanya pale wnapoachana na wale waliokua wakiwapenda. Kwanini? Kuwa na muonekano mpya utakusaidia wewe kujua namna ya kumsahau na kwamba umemvua kabisa akilini kwako. Ukishapata kitu cha kukupa kampani hautakuwa na muda wa kumkumbuka mshkaji tena. Najua unazipenda sana nywele zako - lakini hii itakupa hasira na itakufanya ujioe una maisha mapya na utamsahau kwa kasi ya ajabu.

#11 Jitafutie kampani mpya. Sio kila mtu anaweza akatoka na kuafuta kampani nyingine ya kula bata, kama unaweza hii itakuondolea upweke. Kama utakuwa na kitu au mtu wa kukupa kampani wakati upo kipweke ni jambo linaloweza kukusaidia na hautakuwa na muda wa kumfikiria X wako tena!.

#12 Nenda Gym. Usiwe tu kila siku unapoteza muda mwingi katika kufata hobb zako kama kuangalia movie, mara moja au mbili katika wiki - nenda gym. Hii itakuweka busy, na itakufanya uwe na upumuaji mzuri utakaokufanya umtoe out yule jamaa kama hewa chafu unayoitoa ukiwa mazoezi, itakufanya ufurahi, na itakufanya ujiamini zaidi kwa sababu utaonekana ni mtu amaizing baada ya kutoka mazoezini!.

#13 Jifurahishe mwenyewe. Nenda katengeneze T-Shirt yako, kanunue mask, weka mziki mzuri ndani- air freshner tofauti na ambayo ulikua ukitumia, pamba bafu lako kaunue wyne au tengeneza juice yako itakayokufanya uwe na usiku mtulivu - jambo hili litakufanya haukuwahi kuhitaji mwanaume akufanyie hayo yote. Fanya haya mara chache katika wiki. [Soma: Jinsi ya kujifurahisha mwenyewe baada ya kuachana na mpenzi wako!]

#14 Tafuta hobby mpya ambayo haukuwahi hata kuifikiria au kuizoea. Usijiweke bize na hobby ambazo zitakuwa rahisi na kukufanya wewe kumkumbuka tena X wako. Badala yake, Chagua hobby ambayo itakupa changamoto na kukufanya uifikirie na usimfikirie yule jamaa.
Mfano, unaweza ukaanza kujifunza lugha mpya na itakufanya uanze kujitafutia patners wa faida. Ndivyo tunavyofanyaga ili kuwasahau Shosti.

#15 Kajirushe. Najua hili haliwezi kuwaingia akilini wanawake wengi, lakini kutoka out na kukutana na wanaume wengine itakufanya umsahau kwa haraka. Simaanishi uwe na uhusiano nao - hapana, tembea nao tu, au piga nao story.[Soma:Hatua 14 za haraka za kumfuta Akilini!]

[Soma: Maswali 13 ya kujiuliza kuhusu mapenzi kabla haujayafanya!]

Watu wengi sana hupenda kufahamu namna ya kuwasahau X's wao wa zamani, hivyo kama kweli unahitaji kumsahau kwa haraka, hii ndiyo namna. Share na wenzako tafadhali na wengine wajue.

0 Response to "Njia 15 Za Haraka Za Kumsahau Ex - Boyfriend Wako"

Post a Comment