NAMNA YA KUACHA KUJICHUA AU KUPIGA PUNYETO - Bongo Loves

NAMNA YA KUACHA KUJICHUA AU KUPIGA PUNYETO



Karibuni tena wapendwa wasomaji wa blog hii ya MAHUSIANO kama kawaida leo tena unapata shule nyingine ambayo namatumaini inaendelea kukujenga kiakili na Kimahusiano 

Makala iliyopita niliongelea maana na madhara yanayosababishwa na kupiga punyeto nilipokea simu nyingi ambazo zilitaka pia niongelee suluhisho au jinsi gani mtu anaweza kuacha punyeto kabisa

Punyeto kama tulivyoongea ni tatizo la tabia na linaweza kudhibitika kabisa kama matatizo mengine yeyote. 

FANYA YAFUATAYO.... 

Acha kuangalia video za ponograph: video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

Epuka kukaa nyumbani peke yako; mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine.
Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata hasa madogo madogo kama uchovu mkubwa, kuumwa kichwa na kusahau sana hii itakupa moyo wa kuendelea kutopiga punyeto.
acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema ivoivo, kama unaacha acha mara moja.

Tafuta mpenzi kama huna kabisa: ukiwa na mpenzi madhara ya punyeto kama kupungukiwa nguvu za kiume yatakufanya uache kabisa kwani ukiendelea utaaibika siku moja pale uume utakaposhindwa kusimama kabisa mkiwa faragha chumbani na pia utapata nafasi ya kushiriki tendo la ndoa hivyo kuacha kabisa punyeto. pia unaweza kumshirkisha mwenzi wako tatizo lako ili akusaidie kuacha.

Anza mazoezi na jishughulishe na mambo mengine:hii itakufanya ue bize na mambo mengine na utumie mda wako mwingi huko, pia mazoezi ya jioni yatakufanya uchoke na kushindwa kufikiria kupiga punyeto wakati wa kwenda kulala

Uzoefu unaonyesha, mtu anayepiga punyeto, hata kama ameathiriwa na tatizo la punyeto kwa kiwango gani, endapo atafanikiwa kutopiga punyeto kwa muda wa siku arobaini mfululizo, mtu huyo hatopiga tena punyeto katika siku zote za maisha yake kwani tayari mtu huyo atakuwa amerudia katika hali yake ya kuto kuwa addicted tena na upigaji punyeto, na atalichukia kabisa hata jina la tendo hilo achilia mbali tendo lenyewe.

MAELEZO ZAIDI........

Pia ileleweke kuwa Sio rahisi kwa mtu aliyekuwa addicted na punyeto kustahimili kujizuia kupiga punyeto kwa muda wa siku arobaini mfululizo. Anaweza kujizuia kupiga punyeto kwa siku mbili lakini baada ya hapo ataendelea tena na mchezo wako.



JARIBU PIA DAWA HII....



PILIPILI

Pilipili inayo hitajika hapa ni yoyote ile ili mradi iwe kali sana, ( Ila inayo pendekezwa ni pilipili mbuzi ama pilipili kichaa, pilipili hoho haihusiki hapa ).


MATUMIZI


Kwanza kabla ya kujua matumizi ni vyema ukatambua muda ambao huwa unapiga punyeto ( Mara nyingi huwa ni asubuhi baada ya kuamka,wakati wa kuoga ama usiku kabla ya kulala ).

Chukua pilipili zako, zipasulie kwenye viganja vya vidole vyako na kujipakaza katika viganja vya vidole vyako. Unaweza kutumia pili moja kwa kila kiganja, na kwa kila muda ambao huwa unapiga punyeto lakini unaruhusiwa kujipakaza zaidi ya pilipili moja.

Ukishajipaka pilipili kwenye viganja vya vidole vyako, moja kwa moja unakuwa umekwisha jilazimisha kutokufanya punyeto, kwa sababu ukipiga punyeto kwa viganja ambavyo vina pilipili utawashwa sana wala hautaweza kufurahia tendo hilo.


JAMBO LA KUZINGATIA : Hakikisha unakuwa na walau pilipili mbili mpaka nne kila unapokuwa katika maeneo ambayo yanaweza kukuchochea kufanya punyeto.


UFANISI WA DAWA HII : Dawa hii inawafaa wale tu ambao wamedhamiria kutoka mioyoni mwao kuacha kufanya punyeto. Kwa wale ambao hawajadhamiria haitaweza kuwasaidia. 



MWISHO,TUNAWATAKIA KILA LA HERI WATU WOTE WATAKAO AMUA KUJARIBU KUTUMIA NJIA HIZI ILI KUACHANA NA SUALA LA UPIGAJI PUNYETO. NITAFURAHI SANA ENDAPO MTATUPA FEEDBACK/MREJESHO BAADA YA HIZO SIKU AROBAINI TANGU MUANZE KUFANYA ZOEZI HILI. MUNGU AKUBARIKI

0 Response to "NAMNA YA KUACHA KUJICHUA AU KUPIGA PUNYETO"

Post a Comment