NAMANA YA KUJIZUIA KUFANYA MAPENZI KWENYE PENZI JIPYA
Kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi huwa ni furaha na kuchanganya pia. Unaingiwa na hisia ambazo hujawahi kuwa nazo na pia kupenda kwa dhati. Mpenzi wako anakufurahisha na wewe pia unamfurahusha. Lakini inaweza kutokezea sitofahamu wakati ambapo wewe hutaki ama hujiskii kufanya mapenzi lakini yeye akawa na hamu ya kufanya tendo hilo. Sababu zozote zile uko nazo, una haki ya kujizuia kutofanya tendo la ngono mpaka ile siku ambayo utajiskia kuwa umefikia siku yako. Mwili ni wako na maamuzi ni yako.
So utafanyaje umzuie mpenzi wako kutofanya ngono na wewe?
Mambo ya kufanya kumzui mpenzi wako kutofanya mapenzi nawe
1. Usilale kwake
Iwapo hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako, basi ni vizuri usijiingize
katika hali ambazo zitachangia nyinyi wawili kuingiwa na hamu ya
mapenzi. Iwapo umetoka deti na mpenzi wako, usijaribu kumsindikiza hadi
kwake ama kuenda njia moja. Pia hutakiwi kuwa unazunguka sehemu ambazo
mpenzi wako anaishi wakati kama huo kwa sababu inaweza kuchangia pakubwa
kuingiwa na tamaa.
2. Usiwe mlevi
Kuna baadhi ya watu wanafikiria ya kuwa matumizi ya vinywaji ukiwa na
mpenzi wako inapunguza hisia za kufanya mapenzi. Well, labda inaweza
kuwa ni kweli lakini kulingana na utafiti ni kuwa mtu mlevi anapoteza
mwelekeo wa kufanya maamuzi yafaayo. Hivyo ukiwa umeathirika na ulevi
pamoja na mpenzi wako, kuna asilimia kubwa ya kufanya maamuzi ambayo si
sawa.
3. Toa visababu ambavyo havitomkwanza mpenzi wako
Unaweza kutoa visababu kama vile unaumwa na kichwa, hujiskii vizuri nk.
Ingawa kutumia uongo kwa mpenzi wako si jambo zuri, ni muhimu sana iwapo
itakuja kwa maswala ya kufanya mapenzi ama kama hujiskii kufanya mambo
mengine ambayo yanahusiana na wewe. Hivyo ni muhimu kupatia mambo
mengine kipao mbele.
4. Fungua roho yako
Hii ndio njia nzuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi. Kukaa na mpenzi
wako katika kikao na kumueleza ndani na nje kuhusiana na wewe kujizuia
kutofanya mapenzi ni jambo nzuri zaidi kwa nyote wawili. Kumueleza
ukweli mpenzi wako kutatoa ile nafasi ya kwako kuonekana kama unayapenda
mahusiano yenu na hauhitaji kuficha ama kudanganya katika mahusiano
yenu.
Iwapo atakubali basi itadhahirisha ya kuwa yeye anatilia maanani
mahusiano yenu. Kama atakataa basi bila shaka mahusiano yenu hayatokuwa
marefu.
0 Response to "NAMANA YA KUJIZUIA KUFANYA MAPENZI KWENYE PENZI JIPYA"
Post a Comment