Mapenzi yanaweza kuangamiza Nafsi milele maishani
Wahenga hawakukosea waliposema mapenzi yanaua, mwanamke mmoja wa nchini Uturuki amenusurika kufariki baada ya kujaribu kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya nne baada ya mpenzi wake aliyetaka kufunga naye ndoa kuamua kumchukua mwanamke mwingine.
Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Pinar G. mwenye umri wa miaka 20, mkazi wa mji wa Bursa aliamua kujirusha toka ghorofa ya nne baada ya kugundua mpenzi wake ana mpenzi mwingine.
Taarifa zilisema kuwa Pinar na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Cemil C. walikuwa kwenye mipango ya kuoana hivi karibuni.
Lakini wakati siku ya harusi ikikaribia, Cemil alimtosa Pinar na kuamua kumvalisha pete ya uchumba mwanamke mwingine.
Kutokana na uchungu wa kumkosa mpenzi wake, Pinar aliamua kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya nne.
Pamoja na jitihada za zimamoto na polisi kumshawishi Pinar asijirushe toka ghorofani, Pinar aliamua kuhitimisha maisha yake duniani kwa kujirusha toka ghorofa ya nne.
Bahati nzuri kwake, zimamoto walikuwa wameishalitandaza boya kubwa chini ili kunusuru maisha yake. Pinar aliangukia kwenye boya hilo na maisha yake yakawa yamenusurika.
0 Response to "Mapenzi yanaweza kuangamiza Nafsi milele maishani"
Post a Comment