MAHABA - Bongo Loves

MAHABA

 Image result for Mahusiano
Kama madege yanavyotua na kuondoka ndivyo mawazo kuhusu sex huja yenyewe
kwa mwanaume! Binadamu hawezi kuwa amekamilika akiwa kimwili na kiroho peke yake bila hisia (emotions).
Pia kuna tofauti kubwa sana namna mwanamke na mwanaume wanavyoweza
kufanyia kazi emotions kwenye ubongo.

Bila kufahamu tofauti hizi kati ya mwanaume na mwanamke wakati mwingine
hupelekea suala la mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume kuwa na
matatizo hasa kutokana na upande mwingine kushindwa kuelewa mwenzake
anahitaji nini au kitu gani na wakati gani.

Linapokuja suala la emotions mwanamke ana uwanja mkubwa sawa na barabara
yenye uwezo wa kupitisha magari 8 kwa wakati mmoja (eight lanes super
highway) wakati mwanaume ni sawa na barabara moja ya kwenda kijijini
kiasi kwamba magari hata mawili kupishana ni kasheshe.

Hii ina maana kwamba kumkumbatia mwanamke huweza kumpa raha na msisimko
wa ajabu kihisia na kumsikiliza akiongea humpa raha na kumpa ahuaeni
kuliko kawaida. Wakati mwanaume kuongea sana bila kutoa point kwa maneno machache anaona
unampotezea muda wake.

Pia mwanamke huweza kukumbuka kutukanwa, au kupigwa na anaweza kukumbuka
rangi ya chumba mlichokuwa wakati wa hilo vagi, shati mwanaume ulivaa,
sura yako wakati mnapigana au kutukanana na siku, mwezi na mwaka kwa
kuwa inahusishwa moja kwa moja na hisia zake kwenye hiyo super highway,
wakati mwanaume anaweza akawa baadhi ya vitu hakumbuki.

Wanawake hupenda kuongea kuhusu hisia zao wakati wote!

Linapokuja suala la kuwaza kuhusu sex (mapenzi) basi mwanaume huweza kuwaza kuhusu
sex kila baada ya dakika mbili na mwanamke huweza kuwaza sex wengine ni siku kadhaa katika mwezi.
Je, ndo kusema mwanaume muda wote yupo kwenye foreplay na ndiyo maana
huwa na dakika chake akikutana na mwanamke na kutaka kwenda south pole
moja kwa moja kuchimba gold hata kabla mgodi haujawa tayari!

Kuingia na kutoka kwa mawazo kuhusu sex kwa mwanaume ni sawa na ndege
zinavyoingia na kutoka katika International Airport kama vile Amsterdam, Atlanta
au London Heathrow na mwanamke ni kama kiwanja cha ndege kule Nduli -
Iringa kiasi kwamba wakati mwingine ndege hata zikifika zinaweza zisitue
hadi hali ya hewa iwe nzuri (hadi mwanamke akaribie kuwa fertile)

Hii ina maana kwa mwanaume mawazo kuhusu sex hutua kwa wingi kama madege
makubwa kila baada ya dakika mbili (kutua na kuondoka) na mwanamke ni
sawa na kiwanja kidogo ambapo ndege ndogo za mawazo ya sex (tena private dedicated jet)
hutua kwa mwezi angalau siku chache tu au kwa siku mara moja.
Kwa mwanamke foreplay ni saa 24 kabla ya sex, wakati mwanaume foreplay
ni dakika 3 kabla ya sex. Hapa bila mwanaume kufahamu tofauti iliyopo na mwanamke
mahusiano ya mapenzi huweza kuwa ya kuumiza au kutimiza wajibu tu.

Ndiyo maana linapokuja suala la kutaka sex mwanaume ndiye mara nyingi
hulianzisha, ingawa hii haina maana kwamba mwanamke kama anataka sex kwa
mumewe asubiri mume aanze.

Wanaume hupenda kutafakari kuhusu mapenzi WAKATI WOTE!

ZINGATIA!
Data zinaonesha kwamba wanawake wengi huvutiwa na wanaume ambao
wamewazidi umri zaidi ya miaka miwili na kuendelea iia wanaume ambao ni
warefu kidogo kuliko wanamke wenyewe ingawa wanawake wakiulizwa huwa
wanaruka kimanga.

SWALI LA KIZUSHI…
Ni kweli wanawake wengi huvutiwa na mwanaume kwa sababu ya ukubwa wa wallet
yake na reputation au status aliyonayo katika jamii na si sura, size, rangi au
kitu chochote kwenye mwili wake?

0 Response to "MAHABA"

Post a Comment