Madhara Ya Kuchaguliwa Mwenzi Wa Kuishi Naye Katika Mahusiano Ndoa
Madhara Ya Kuchaguliwa Mwenzi Wa Kuishi Naye Katika Mahusiano Ndoa
KAMGISHA BLOG / 28 minutes ago
KAMGISHA BLOG / 28 minutes ago
Mtanzania? Ni imani yangu kuwa uko salama rafiki na
unaendelea vizuri katika harakati zako za kila siku kuhakikisha unapata
kile unachokitaka kwenye maisha yako. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya
siku hii ya leo ameweza kutustahilisha tena kuiona siku hii ya leo. Kwa
hiyo rafiki, tutumie muda huu wa leo vizuri kwani leo ni siku bora
ambayo haitokuja tena kutokea katika maisha yetu hapa duniani.
Mpendwa rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu
ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja yale ambayo nimeweza kukuandalia siku
hii ya leo. Hivyo basi, nakusihi ungana nami mwanzo hadi mwisho wa
makala hii ili tuweze kusafiri wote kwa pamoja. Leo tutakwenda kujifunza
juu ya madhara ya kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye kwenye maisha ya
mahusiano. Je ni madhara gani rafiki? Karibu rafiki tuweze kujifunza
wote kwa pamoja.
Katika moja ya matatizo yanayowasumbua watu duniani basi
moja wapo ni mambo ya mahusiano. Mahusiano haya yanaweza kuwa mahusiano
ya uchumba, mahusiano ya ndoa na nk. Sasa katika mahusiano ya ndoa wapo
watu wengi sana wanaruka hatua muhimu sana ambazo baadaye zinakuja
kuwaumiza vibaya. Hatua hizo muhimu ni urafiki na uchumba kwa hiyo,
ikitokea watu wamekutana ndani ya miezi miwili, mmoja na kukimbilia
kufunga ndoa ndio hawa wale wanaokuja kujuta kwa nini walifanya maamuzi
hayo.
Mpendwa msomaji, malengo mahususi ya somo letu la leo ni
madhara ya kuchaguliwa mwenza katika maisha ya mahusiano. Ziko jamii
tofauti duniani zenye utaratibu au utamaduni wa kuwachanguliwa watoto
wao wenza pale wanapokua wamekaribia ule umri wa kuishi ya maisha ya
ndoa kama mke au mume. Wazazi wa jamii za kuwatafutia watoto wao wenza
bado wapo mpaka leo katika zama hizi za taarifa na pengine unafahamu
watu ambao wanafanya jambo hili kwenye jamii iliyokuzunguka.
Kwa mfano, mtoto tokea akiwa mdogo anawekewa ‘’ oda’’
mapema kuwa wewe utaolewa na mtu fulani au utamuoa mtu bila kujali
unataka au la. Kwa hiyo, tabia hii inawanyima watoto wengi kuwa na mtu
Yule anayempenda badala yake wanakuwa na watu ambao siyo chaguo lao la
kutoka moyoni. Utamaduni huu unakuwa ni kama kumnyima mtu kuishi maisha
anayotaka hapa duniani.
Unaporuhusu wazazi wakuchagulie mwenza wa kuishi naye katika maisha ya ndoa kwanza inakuwa ni utumwa wa hali ya juu. Kwanini?
Unaporuhusu wazazi wakuchagulie mwenza wa kuishi naye katika maisha ya ndoa kwanza inakuwa ni utumwa wa hali ya juu. Kwanini?
Kwa sababu kuchaguliwa kufanya kitu ambacho hukipendi
katika maisha yako ni utumwa. Vivyo hivyo, kuchaguliwa mwenza wa kuishi
naye ni utumwa pia. Unapokuwa unachaguliwa mwenza wa kuishi naye unakuwa
unavunja hatua muhimu sana katika kuelekea maisha ya ndoa ambayo ni
urafiki na uchumba. Kupitia hatua hizi unaweza kumchunguza mwenzako ni
mtu wa namna gani, falsafa yake ya maisha ikoje, ni mtu chanya au hasi,
ni mtu wa kuigiza maisha au ni mtu halisi anayeishi bila kuigiza maisha
na mambo mengine mengi unayotaka kuyajua kutoka kwa mwenzako.
Rafiki, watu wanaoishi na wenza wao kwenye maisha ya ndoa
kwa kuchanguliwa na kwenda kuanza kuishi maisha ya urafiki, uchumba na
ndoa kwa wakati mmoja huwa wanashinda sana. unakuta mwenzako anaishi
falsafa tofauti kabisa na wewe ulivyotarajia. kwa mfano, wewe falsafa
yako ni kuishi chini ya kipato chako na unakuta mwenzako anataka kuishi
juu ya kipato kwa kufanya mambo ambayo hayana ulazima kwenye maisha.
Lakini kama ulikuwa umemgundua mwenzako na kumsoma vizuri katika hatua
za uchumba ungeweza kufanya maamuzi mapema kwa kumpima kama mtu huyo
anakufaa au la kulingana na vigezo vyako.
Kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye katika zama hizi ni aibu
kwa kweli kwani ni kuchaguliwa kufanya chochote ambacho hukipendi ni
utumwa katika maisha yako. Kumbuka rafiki, hata mzazi akikuchagulia
mpenzi ambaye wewe humpendi na ukakubali utakua umejichagulia wewe
mwenyewe kuingia shimoni. Kwa hiyo, hata wazazi wakikuchagulia kuishi na
mwenza ambaye wanampenda wao ni kama kuchaguliwa maisha ya kuishi hapa
duniani. Licha ya kuchaguliwa maisha wewe ndiye utakayeenda kuishi hayo
maisha na wala siyo wazazi watakaopata raha au shida, ukiingia shimoni
wao hawatakuwepo bali wewe ndio utawajibika.
Hatua ya kuchukua leo; usikubali kuchaguliwa mwenza wa
kuishi naye katika maisha yako. Ishi na mtu unayempenda kutoka moyoni,
ishi na mtu ambaye mliweza kupitia hatua za urafiki, uchumba ukamjua
vizuri tabia zake ni mtu wa namna gani. Fanya kitu ambacho unakipenda
ndio furaha ya kweli katika maisha ambapo utapata mafanikio makubwa
yenye furaha na ubora wa hali ya juu.
Kwa kuhitimisha, tunaishi karni ya ishirini na moja na
hatuko tena katika zama za mawe bali tupo katika zama za taarifa. Kuwa
chachu ya mabadiliko kwa kuvunja utumwa huo katika jamii uliyopo siyo
unasoma na kupata elimu ya juu bado ukirudi nyumbani wazazi
wanakushurutisha kuoa au kuolewa na mtu Fulani bila ya ridhaa yako
mwenyewe. Wewe ndio mwenye maamuzi ya maisha yako kwa sababu hakuna mtu
mwingine atakaye ishi maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe.
0 Response to "Madhara Ya Kuchaguliwa Mwenzi Wa Kuishi Naye Katika Mahusiano Ndoa "
Post a Comment