JINSI YA KUONGEZA MAPENZI YALIO JUU KWA MPENZI WAKO
Hakika unahitaji akiwa mbali awe anatamani aone sura yako au asikilize sauti yako au hata asome SMS tamu iliyoandikwa kitaalamu na vidole vyako.
Hii ni hatua kubwa zaidi katika mapenzi. Ukiona mwenzi wako amefika kwenye kiwango hicho cha upendo, maana yake unamkonga kwelikweli. Amekushiba na umejaa ndani ya kuta za moyo wake.Hayo hayaji kama zawadi.
Mapenzi huzaliwa, hustawishwa kabla ya kukua. Kuna mambo ambayo unatakiwa uyafanye kuhakikisha mwenzi wako anakuza upendo wako kwako. Ni kama msemo wa ukiona vyaelea vimeundwa.Jinsi ya kumchombeza mtu, hutegemea pia jinsia.
Yapo mambo ambayo mwanamke anapenda aambiwe na mwenzi wake pia yapo matarajio ya wanaume kwa wapenzi wao.Kupitia yote hayo, tutayatazama katika muktadha mpana.
YAMPENDEZAYO MWANAMKE
Hapa chini kuna maneno 10 ambayo huwapendeza wanawake wengi. Yazingatie:
WEWE NI MREMBO (You’re beautiful)
Kiswanglish kinachukua nafasi pana hapa kwetu, kwa hiyo unaweza kumwambia kwa Kiswahili au Kiingereza, muhimu ni kuangalia jinsi anavyoweza kufurahia. Inawezekana akawa si mrembo kama Irene Uwoya au Jokate Mwegelo lakini unayo nafasi ya kumfanya ajione yupo sawa nao. Mwambie kuwa akivaa, hutoka bomba kuliko hao. Mtamkie maneno hayo asubuhi kabla hamjaachana kwenda kazini. Neno lako litamfanya ajiamini siku nzima.
UNAYAWEZA (You’re a great lover)
Kama wewe una bahati ya kupata mwenzi ambaye amepita unyagoni na kufuzwa kimitindo, ni heri yako.
Ikiwa uliyenaye hajiwezi, basi usisite kumwambia kwamba ukiwa naye faragha, anakutosheleza kwa asilimia 100. Unaweza kumchombeza kwa kumwambia afanye ziada ili kukufurahisha lakini tangulia kumsifia.
Wanawake wengi, hupenda kujua kama wanaume wao wanatosheka pindi wanapowapa huduma ya faragha.
Ukimsifia, unampa amani ya moyo na kumfanya ajiamini.
UNA AKILI SANA (You’re so smart)
Mwanamke hupenda kuonekana ana akili. Kama kuna kitu ambacho unaweza kumkwaza mwenzi wako ni pale utakapomtamkia kwamba yeye ni mjinga. Mfanye ajione ni bora kwa kumwambia kuwa ana akili sana. Mueleze kuwa kutokana na akili alizonazo, unaamini familia yenu itapata maendeleo makubwa kwa sababu ubongo wake ni hazina.
WEWE NI RAFIKI MKUBWA
(You’re my best friend)
Mwanamke wako anakupenda sana. Siyo tu kwamba anataka kuwa mpenzi wako bali pia anahitaji awe rafiki yako mkubwa. Mwambie kuwa huna rafiki mkubwa kama yeye chini ya jua.
Mchombeze kwamba huna mtu mwingine wa kuchangia naye siri zako zaidi yake. Hii inamaanisha kuwa mwanamke hapendi kuwa kimbilio lako la pili, daima hutaka kuwa wa kwanza ndani yako.
WEWE NI MUHIMU KWANGU
(You’re the most important thing to me)
Inawezekana ukawa ‘bize’ mno na kazi. Unatumia muda wa wikiendi kuponda maisha na marafiki. Angalizo ni kuwa, usithubutu kumfanya mwanamke wako akahisi humuoni ni muhimu.
Pamoja na ‘ubize’ wako, tumia muda mchache unaoutumia na yeye kumuonesha jinsi alivyo muhimu. Isiishie hapo, mtamkie kwa herufi kubwa: “Wewe ni muhimu kwangu kuliko kitu kingine chochote duniani.”
SIKUDANGANYI
(I would never lie to you)
Mwanamke hujiamini pale anapobaini kuwa mwenzi wake ni mkweli. Anapokosea, hukiri na kuomba msamaha. Humchukia yule ambaye hujifanya kauzu, macho makavu anadanganya. Mwambie humdanganyi na umaanishe unachosema. Hayo yakijaa kwenye ubongo wake, utakuwa umempatia kwa kiwango kikubwa.
SIJAWAHI KUKUSALITI
(I have never cheated on you)
Jaribu kuanzisha mazungumzo kuhusu namna ambavyo unachukia usaliti. Mbele ya mazungumzo yako, mueleze kuwa unaridhika kuwa naye, kwa hiyo hujawahi kumsaliti hata mara moja. Ni kawaida ya wivu kukua muda baada ya muda lakini wewe unayo nafasi ya kumfanya asiwe na chembe yoyote ya kukuhisi unamsaliti.
NINGEPOTEA BILA WEWE
(I’d be lost without you)
Ni katika kumfanya ajione yeye ni taa ya maisha yako. Mueleze kuwa kama si yeye, ungeshapoteza muelekeo wa kimaisha. Kwa kawaida, mwanamke hataki tu kujua kuwa unampenda na kumtaka, ila unamhitaji kwa dhati, kwa hiyo ukimwambia ni yeye ndiye amekuweka kwenye mstari, atajiamini kuwa unamhitaji sana.
WEWE NI MCHESHI (You’re funny)
Daima tembea na kanuni hii. Wawili wanaopendana na kucheka pamoja ndiyo hudumu. Mpe uhuru akuchekeshe halafu uruhusu mbavu zako zivunjike kwa kicheko. Mwisho wa kicheko, gonganisha naye viganja halafu mwambie “wewe ni mcheshi sana mpenzi wangu.”
NAKUPENDA (I love you)
Ni neno la kawaida lakini kwa mwanamke huwa lina maana kubwa endapo litatamkwa na mtu anayempenda.
0 Response to "JINSI YA KUONGEZA MAPENZI YALIO JUU KWA MPENZI WAKO "
Post a Comment