JIFUNZE KITU KWENYE KISA HIKI
Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.
Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.
Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.
Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: “Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”
Akajibu: “Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”
.
.
.
FUNZO:
Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.
Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.
1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.
2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.
3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.
Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.
Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.
*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.
Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!
0 Response to "JIFUNZE KITU KWENYE KISA HIKI"
Post a Comment