Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa kuolewa;
Visingisizio vingi visivyokuwa vya msingi.
Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana inaweza ikawa ni sababu ya
kufanya mabinti wengi wasiolewe. Binti unakuta anataka mwanaume awe
amesoma, mrefu, handsome, sijui awe na kazi nzur, awe na upendo wa
kweli, na mambo mengi kama hayo. Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni
wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa.
Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono
ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi. kuna msemo usemao, "ndege
mjanja hunasa kwenye tundu bovu" na mwingine ufananao na huo unaosema
"mchagua nazi hupata koloma".
Namna unavyojiweka.
Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa,
marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla. Mabinti wengi wanafeli
sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi
yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona
kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.
Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi
hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa
yapo wazi yananing'inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi mapaja yote
yapo wazi na tena ina mpasuo? Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani,
michirizi ya nguo ya ndani inaonekana.
Sidhani kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni
maonyesho ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na
mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka, Sidhani
kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya
usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma.
Niwasaidie dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa
kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha
usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.
Maneno Unayojitamkia ni sumu sana.
Vijana wengi wamekuwa na desturi ya kujisemea maneno ya laana bila kujua yana madhara gani katika maisha yao.
Utakuta Binti kwa sababu aliumizwa na kijana fulani basi, anasema
Wanaume wote ni wale wale, sijui siku hizi Hakuna waoji, mara Wanaume
wote ni waongo, baba mmoja na mama mmoja.
Sikia nikuambie, kinywa chako kina uwezo wa kuumba. Kila neno baya au zuri unalojitamkia ndivyo litakuwa kwako.
Binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu(Mwanzo 1 :26) , Mungu aliumba
dunia kwa kupitia Neno, kadhalika hata sisi tunao huo uwezo wa uumbaji
kupitia vinywa vyetu (Mithali 18 :18 - 20).
Kama Unasema Wanaume wote ni waongo basi usishangae Kila mwanaume
atakayekuja kwako akiwa muongo. Kama Unasema sina shida ya kuolewa basi
miaka 30 itakukuta ukiwa nyumbani kwa baba yako. Chunga kinywa Chako.
0 Response to "Hizi ndizo sababu kwanini mabinti wengi karne hizi hawaolewi "
Post a Comment