DALILI ZA MWANAMKE ASIYEKUPENDA KWA DHATI
Unapokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwanamke ambaye hakupendi kwa dhati basi utamgundua kwa dalili zifuatazo;
1. Hataki kuambata na wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali.
2. Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.
3. Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa.
4. Anaahilisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu.
5. Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna!
6. Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkimya na mshiwishi mkubwa wa kuachana kutoka kwenye matembezi yenu ya jioni. “Aaah, mi nimechoka narudi nyumbani”
7. Anajaribu kukuunganisha na wanawake wengine na haoni vibaya anaposikia unamfukuzia mwingine badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.
8. Hajuti anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.
9. Msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.
10. Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake pia. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi ya kwako kuliko wewe kujua yake.
0 Response to "DALILI ZA MWANAMKE ASIYEKUPENDA KWA DHATI"
Post a Comment