Zifahamu Sababu za Matairi ya Gari Kuwa na Rangi Nyeusi - Bongo Loves

Zifahamu Sababu za Matairi ya Gari Kuwa na Rangi Nyeusi



Ulishawahi kujiuliza kwanini viwanda havitengeneza matairi ya kijani au njano ili yakiwekwa kwenye matrekta ya John Deere yaendane vizuri kwa rangi.  Au ya rangu nyingine ili kuendanana na rangi ya gari? Au kwanini hawauachi mpira unaotengenezea matairi katika rangi yake ya asili ya nyeupe?

Kuna sababu kwanini matairi ya magari duniani huwa na rangi nyeusi na si rangi nyingini. Sababu kubwa ni kuweza kuwa na ubora zaidi wa kutumika.

Kwa makusudi kabisa matairi ya magari ni ya rangi nyeusi ili yaweze kufanyakazi vizuri na kuyafanya yaweze kutumika kwa muda mrefu zaidi kwa kuongeza kemikali kwenye mpira inayojulikana kitaalamu kwama ‘Carbon Black’ ambayo ndiyo hubadilisha rangi ya matairi.

Kwanini Carbon Black? Kemikali ya Carbon Black hufanya kazi kubwa ya kuongeza uwezo wa mpira wa tairi kufanya kazi kwa ubora wa hali ya ju kiasi kwamba duniani kote wakawa wanaitumia kemikali hiyo. Asilimia 70 ya kemikali hiyo inayozalishwa dunia, hutumika kutengenezea matairi mbalimbali.

Carbon black huongeza uwezo wa raba kuweza kutumika muda mrefu zaidi pamoja na kuipa uimara ili kuzuia kutoisha kirahisi ikiwa juu la lami.

Aidha Carbon black husaidia kuipa tairi muda mrefu wa matumizi kwa kuondoa joto na hivyo tairi haiwezi kuathiriwa na joto kirahisi. Kabla ya vita ya kwanza ya dunia, Zinc Oxide (iliyofanya matairi kuwa meupe) ilitumika kwenye matairi badala ya carbon black ili kuzuia tairi kupata joto na kuwa ngumu. Lakini baada ya matumizi ya carbon black kushika kasi, ilianza kutumika sehemu ya juu ya tairi (tire tread) na zinc oxide kutumika kwenye kuta za tairi (tire sidewalls)

Carbon black pia huisaidia tairi kujikinga dhidi ya madhara ya gesi ya ozone (corrosive effects of ozone). Gesi ya ozone ni moja ya vitu ambavyo huchangia kuharibika sana kwa tairi, hivyo kemikali hiyo ni ya muhimu sana kwa watengenezaji na watumiaji, bila hiyo tairi zingekuwa zinaharibika haraka sana. Madhara ya gesi ya ozone ndiyo sababu haushauriwi kuhifadhi tairi zako karibu na mota za kielektroni ambazo huto gesi hiyo.

Kwa kuhitimisha unaweza kusema kuwa, sababu kubwa ya tairi za magari na vifaa vingine kuwa nyeusi ni kwa sababu ya matumizi ya kemikali ya carbon black ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uimara wa mpira unaotumika kutengenezea tairi.


USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍 https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.konayamahaba.app&hl=en

0 Response to "Zifahamu Sababu za Matairi ya Gari Kuwa na Rangi Nyeusi "

Post a Comment