Wanawake Wengi Walioolewa ni Wepesi wa Kuchepuka..Yaani Simple Kama Kumsukuma Mlevi - Bongo Loves

Wanawake Wengi Walioolewa ni Wepesi wa Kuchepuka..Yaani Simple Kama Kumsukuma Mlevi

Wanawake wengi walioolewa wamekuwa wepesi (achilia mbali vidada ambavyo havijaolewa, ingawa navyo ni majanga lakini, afadhali mitego yao kidogo ni negotiable). Wengi wao huwatongozi ila watakutongoza wenyewe! Kundi risky zaidi ni la wamama wa nyumbani au wanawake ambao hawajasoma (I am sorry to say this)! Unaweza kukuta mme wake ana fedha na kila kitu, lakini kwa sababu jamaa hajaajiriwa serikalini au kwenye taasisi au kampuni (kumbuka tulio wengi tunatamani kujiajiri!), mke wake anamchukulia kama mtu fulani ambaye hana hadhi nzuri ya kuwa mme. Sumaku kali zaidi ambazo huwavuta wamama wa aina hiyo, ni wale vijana au watu wazima walioajiriwa, wanaotoka asubuhi, wamepiga tai, kiatu kiwi full time, wengine suti, halafu ni watu wa misheni town (wenye magari sijui inakuwaje, mtatuambia), (haata kama kazi zao ni kufagia au kuzunguka na mafile maofisini)! Wanawake wa aina hiyo huanza kwanza kwa kutafuta ukaribu na mazoea na watu wa aina hiyo kwa udi na uvumba katika harakati za kufanikisha azma zao. Licha ya uzoefu nilioushuhudia juu ya wamama hapo juu, hivi karibuni nimekumbana na majanga kadhaa yakihusisha wanawake walioolewa kwa ujumla, wengi wao wanaoonekana ni sex hungry moms au gold diggers. Nawapa tu mifano michache kuthibitisha haya ninayoyasema: 1. Mie nakaa mwenyewe mmama from no where akaanza kuniletea chakula (niliogopa sana), akaniambia naona unapata shida unakaa mwenyewe na wewe ni mwanaume huwezi kujipikia. Siku ya kwanza sikukila (nilikiweka kwenye chombo changu nikampa sahani, baadaye nilikimwaga), maana niliona kama labda kaweka kitu. Siku nyingine akaleta na kuniambia tule wote! Hooooooooo, nikamwambia tutakula wapi? Akasema kwako, usiogope mme wangu amesafiri! Sasa tukiwa tumekaa, alikuwa amejifunga kanga moja, anatawanya miguu na kuirudisha, nilijikaza sikufanya chochote, vituko anavyonifanyia mpaka sasa ni siri yangu. 2. Mwingine alipata namba yangu kupitia simu ya mmewe ambaye ni rafiki yangu, kila mara hasa usiku ana msgs kama hizi: "shem habari, nahisi wewe ni mcheshi, huna kiburi wala makuu, tena unachat na mimi bila shida, nina hamu siku moja nije Dar nikufahamu, au sio shem?" Mara nyingi sijibu, akiona hivyo "shem nijibu basi, usiogope maana mme wangu hayupo sasa hivi". Vituko vyake siku hizi havisimuliki! 3. Mwingine, kutwa kulalamika kuhusu maisha yake na ndoa "Yaani shem, we acha tu, maisha magumu, rafiki yako naye kipato hakieleweki na mie sikusoma wala kubahatika kuajiriwa, maisha yanaenda tu kwa nguvu za Mungu, ningekuwa sio mvumilivu sidhani kama hii ndoa ingekwepo, shem unakaa wapi nije kukusalimia au una mke?" Mie najiuliza hivi wakati wa kufunga ndoa hakuapa kuwa na mmewe kwa shida na raha? 4. Mwingine ni mama jirani yangu, tena ni mtu anayejiweza, siku moja akaniita anaomba nimsaidie kurudishia taa imeungua, nilivyopanda juu ya meza alinipa taa - tube light mbovu, kuiweka haiwaki, akaniambia naomba simu yako nimpigie kijana fulani wa mtaani aniletee taa nyingine, nilivyompa kumbe alijipigia, halafiu akaniambia hapatikani, acha. Tangu awe na namba yangu, utaona mida ya saa 4 usiku anatuma msgs kama vile "Mambo, Jumamosi hii twende tukatembee" au "Nina kitu nataka kukuambia ila tunahitaji faragha", Huwa namjibu, nina mambo mengi, labda siku nyingine. Ni majanga mengi sana nakutana nayo yanayohusisha akina mama walioolewa. Mliooa kuweni makini na wake zenu, wengi ni washenzi sana na wana sophisticated means za kuwaengage wanaume wengine kwenye mahusaiano na wao! Pia najiuliza tatizo lao la kuzoeana na wanaume wengine na kujifanya wana hamu ya kuchat au kuwa karibu nao na sio waume zao ni nini? NB: Nawaasa vijana kukaa mbali na mke wa mtu, maana mke wa mtu ni zigo la madawa ya kulevya. Na si Wote WanaochepukaUSISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍

0 Response to "Wanawake Wengi Walioolewa ni Wepesi wa Kuchepuka..Yaani Simple Kama Kumsukuma Mlevi "

Post a Comment