Utafiti; Mwanaume Akiwa na Mwanamke Mrembo, Anakuwa na Mvuto Kwa Wanawake Wengine. - Bongo Loves

Utafiti; Mwanaume Akiwa na Mwanamke Mrembo, Anakuwa na Mvuto Kwa Wanawake Wengine.

Heshima kwenu wakuu. Utafiti umedhihirisha kwamba mwanaume akiwa na mpenzi mrembo, basi wanawake wengine humwona kuwa mzuri au ana mvuto zaidi. Utafiti ulifanyika katika awamu tatu; Kwanza, Wanawake 148 walionyeshwa picha ya mwanaume wakaambiwa waeleze kama (a)Hana mvuto/sio mzuri kabisa (b)ana mvuto/mzuri wa wastan na (c)ana mvuto sana/mzuri sana. Katika kundi hili wanawake wote walisema huyo mwanaume ana mvuto wa wastan au ni mzuri kiasi. Kundi lingine la wanawake 97 walionyeshwa picha ya huyo mwanaume, lakini pembeni yake akiwa na mwanamke mrembo. Wakaambiwa kuwa huyo ni Dada au Shangazi yake. Sasa wakaambiwa waelezee mvuto/uzuri wa huyo njemba. Kundi hili pia walisema kuwa jamaa ana mvuto wa kawaida tu. Kundi la mwisho lilihusisha wanawake 127. Walionyeshwa ile ile picha ya mwanaume akiwa na mwanamke mrembo. Lakini safari hii waliambiwa huyo mrembo ni MPENZI wake. Waliambiwa waelezee jamaa ana mvuto/mzuri kiasi gani. HAWA WANAWAKE WOTE WALISEMA HUYO MWANAUME ANA MVUTO SANA/MZURI SANA. Sababu walizotoa ni kuwa huyo mwanaume atakuwa na akili sana, mwaminifu, mcheshi, tajiri na msikivu. Watafiti walihitimisha kuwa, wanawake wanaamini kwamba mpaka kufikia mwanaume ammiliki mwanamke mrembo, ni lazima atakuwa "Smart" So, - Men look better when they're a proven commodity. By chifu77 USISAHAU KUSHARE NA KUCOMMENT APPLICATION YETU YA KONA YA MAHABA❤️😘😍

0 Response to "Utafiti; Mwanaume Akiwa na Mwanamke Mrembo, Anakuwa na Mvuto Kwa Wanawake Wengine. "

Post a Comment